“Kijana Daudi,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Kijana Daudi,” Hadithi za Agano la Kale
1 Samweli 16
Kijana Daudi
Kijana mchungaji aliyeitwa kuwa mfalme
Bwana alimtuma nabii Samweli kumtafuta mfalme mpya. Sauli ambaye alikuwa mfalme wakati huo, alikuwa ameacha kumfuata Bwana. Bwana alimwambia Samweli asafiri kwenda Bethlehemu na amtafute mtu aliyeitwa Yese. Mfalme mpya angekuwa mmoja wa watoto wa Yese.
1 Samweli 16:1–5
Wana wakubwa wa Yese walikuwa warefu na wenye nguvu. Lakini Bwana alimwambia Samweli asiwahukumu kwa mwonekano wao.
1 Samweli 16:6–10
Samweli alimwuliza Yese kama ana wana wengine. Yese alisema mwanawe mdogo, Daudi, alikuwa akichunga kondoo. Daudi akaletwa kwa Samweli.
1 Samweli 16:11
Daudi alikuwa mdogo zaidi kuliko kaka zake na alikuwa mvulana mchungaji tu. Lakini Bwana hakujali Daudi alionekanaje. Bwana alijua moyo wa Daudi ulijaa imani. Yeye alimwambia Samweli kwamba Daudi angekuwa mfalme. Samweli akambariki Daudi. Roho wa Bwana alimtayarisha Daudi kuwa mfalme.
1 Samweli 16:12–13