“Ibrahimu na Isaka,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Ibrahimu na Isaka,” Hadithi za Agano la Kale
Mwanzo 17; 21–22
Ibrahimu na Isaka
Baba, mwana, na sadaka
Ibrahimu na Sara walipata mtoto wa kiume, kama vile Bwana alivyoahidi. Walimpa jina Isaka.
Mwanzo 17:9; 21:1–3
Walimpenda Isaka. Walimfunza kuchagua mema na kumwamini Bwana.
Mwanzo 21:8
Bwana aliwaahidi Ibrahimu na Sara kwamba kupitia Isaka familia yao ingekua ili kubariki dunia yote. Lakini siku moja Bwana alimwambia Ibrahimu kumchukua Isaka kwenda Mlima Moria na kumtoa Isaka kama sadaka ya kuteketezwa.
Mwanzo 17:1–8; 22:1–2
Wakiwa njiani kuelekea mlimani, Isaka aliuliza mwana-kondoo wa sadaka ya kuteketezwa alikuwa wapi. Ibrahimu alisema Bwana angetoa mwana-kondoo.
Mwanzo 22:4–8
Juu ya Mlima Moria, Ibrahimu alijenga madhabahu na kuweka kuni juu yake.
Mwanzo 22:8–9
Kama Bwana alivyoamuru, Ibrahimu alimwomba Isaka kulala juu ya madhabahu. Isaka alimwamini Ibrahimu kama vile Mwokozi Yesu Kristo alivyomwamini Baba Yake.
Mwanzo 22:9
Wakati Ibrahimu alipokuwa karibu kumtoa Isaka kama sadaka ya kuteketezwa, malaika wa Bwana alimzuia. Ibrahimu alionyesha imani yake kwa Bwana. Ibrahimu alijua kwamba daima angemfuata Bwana.
Mwanzo 22:10–12
Ibrahimu alitazama na kumwona kondoo dume amenaswa kwenye kichaka. Bwana alimtoa kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.
Mwanzo 22:13
Ibrahimu na Isaka walijifunza kuhusu jinsi ambavyo Baba wa Mbinguni angemtoa Mwana Wake Yesu Kristo kama sadaka. Bwana Yesu Kristo alimwamini Ibrahimu kwa sababu alitii. Ibrahimu aliamini ahadi ya Bwana kwamba siku moja familia yake ingekua kupita idadi ya nyota za angani.
Mwanzo 22:17–18; Yakobo 4:5