“Hajiri,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Hajiri,” Hadithi za Agano la Kale
Mwanzo 16
Hajiri
Mpango wa Bwana kwa ajili ya binti Wake
Hajiri alikuwa mtumishi wa Sara. Sara alikuwa mzee na hakuwa na watoto. Alimwambia mume wake, Ibrahimu, amwoe Hajiri ili waweze kuwa na watoto. Ibrahimu na Hajiri wakaoana, na punde Hajiri alitarajia kuwa na mtoto.
Mwanzo 16:1–3
Hajiri na Sara wakaanza kutofautiana. Hajiri alichagua kukimbilia jangwani.
Mwanzo 16:4–6
Hajiri alipokuwa akisafiri, akawa amechoka sana na mwenye kiu. Mwishowe, akafika mahali penye maji na akapumzika hapo.
Mwanzo 16:7
Bwana alijua kuhusu matatizo ya Hajiri na alikuwa na mpango wa kumsaidia. Alimtuma malaika kumwambia arudi tena kwa Ibrahimu na Sara. Aliahidi kwamba familia ya Hajiri ingekua. Alisema kwamba mtoto atakaye kuwa naye alikuwa mvulana na kwamba angemwita Ismaili
Mwanzo 16:7–14
Hajiri alimtumaini Bwana na alimtii malaika. Alirudi kwa Ibrahimu na Sara. Hajiri alipata mtoto wake wa kiume, na jina lake lilikuwa Ismaili. Hajiri alijua kwamba Bwana anamlinda.
Mwanzo 16:11, 15