Vitabu vya Maelekezo na Miito
31. Usaili na Mikutano Mingine na Waumini


“31. Usaili na Mikutano Mingine na Waumini,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“31. Usaili na Mikutano Mingine na Waumini,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
wanaume wakisalimiana kwa mikono

31.

Usaili na Mikutano Mingine na Waumini

31.0

Utangulizi

Yesu Kristo mara nyingi aliwatumikia wengine mmoja baada ya mwingine (ona, kwa mfano, Yohana 4:5–26; 3 Nefi 17:21) Anampenda kila mmoja wa watoto wa Mungu. Anawasaidia kila mtu binafsi.

Sura hii inaweza kuwasaidia viongozi wote ambao wana fursa ya kukutana na waumini binafsi.

31.1

Kanuni Zinazoongoza

31.1.1

Jiandae Kiroho

Jiandae mwenyewe kiroho kupitia sala, kujifunza maandiko, na kuishi kwa haki. Sikiliza minog’ono ya Roho Mtakatifu.

31.1.2

Msaidie muumini Ahisi Upendo wa Mungu

Wakati waumini wanapokujia kwa ajili ya usaili au kwa ajili ya msaada kutokana na changamoto binafsi, mara nyingi kile wanachohitaji zaidi ni kujua kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda.

Maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho humwalika Roho na hufundisha maandiko ya kweli. Yatumie kuwatia moyo na kuwapa tumaini, siyo kulaani, kulazimisha, au kusababisha hofu (ona Lukaa 9:56).

31.1.3

Msaidie Muumini Avute Nguvu ya Mwokozi

Watie moyo waumini wamgeukie Yeye. Wasaidie wavute nguvu Zake za kuimarisha, kufariji, na kukomboa.

31.1.4

Msaidie Muumini Ahisi Faraja na Salama

Siku zote mpe muumini uchaguzi wa uwepo wa mtu mwingine wakati wa usaili au mkutano. Unapokutana na muumini wa jinsia tofauti, mtoto, au kijana, hakikisha kwamba mzazi au mtu mzima mwingine yupo. Mzazi au mtu mzima huyo anaweza kujiunga na mkutano au kungoja nje ya chumba, kutegemeana na matakwa ya muumini ambaye unakutana naye.

Usitoe taarifa za siri kwa mtu yeyote—ikijumuisha mke wako au kiongozi mwingine wa Kanisa—isipokuwa kama muumini anaruhusu.

31.1.5

Uliza Maswali Yenye Mwongozo wa Kiungu na Sikiliza kwa Makini

Unapokutana na muumini, uliza maswali ambayo yatakusaidia uelewe hali yake.

Wakati muumini anapozungumza, sikiliza kwa makini na kwa usikivu.

31.1.6

Himiza Kujitegemea

Kwa sababu ya upendo wako kwa waumini, unaweza kutaka kutoa ufumbuzi kwa matatizo yao papo hapo. Hata hivyo, utawabariki zaidi kwa kuwasaidia wapate ufumbuzi wao wenyewe na wafanye maamuzi yao wenyewe (ona Mafundisho na Maagano 9:8).

31.1.7

Saidia Juhudi za Kutubu

Askofu au rais wa kigingi ndiyo pekee wanaoweza kumsaidia mtu atatue dhambi kubwa. Baadhi ya hizi zimeorodheshwa katika 32.6. Kama muumini amefanya yoyote kati ya dhambi hizi, anapaswa kukutana na askofu au rais wa kigingi mara moja.

31.1.8

Jibu kwa Usahihi kuhusu Unyanyasaji

Unyanyasaji hauwezi kuvumiliwa katika sura yoyote. Chukulia taarifa za unyanyasaji kwa uzito unaostahili. Kama unafahamu kwamba mtu fulani amenyanyaswa, toa taarifa ya unyanyasaji kwa mamlaka ya kiserikali na shauriana na askofu. Mwongozo kwa ajili ya kutoa taarifa na kujibu unyanyasaji umetolewa katika 38.6.2

31.2

usaili

31.2.1

Madhumuni ya Usaili

Kwa ujumla,viongozi wa Kanisa wanawasaili waumini ili kubaini ikiwa wao:

  • Wako tayari kupokea ibada au kushiriki katika ibada.

  • Wanapaswa kuitwa kwenye nafasi katika Kanisa.

31.2.2

Aina za Usaili

Nani anaweza kuendesha usaili

Dhumuni la usaili

Nani anaweza kuendesha usaili

Askofu peke yake

Dhumuni la usaili

  • Anatoa kibali cha hekaluni kwa muumini anayepokea endaumenti yake au kuunganishwa kwa mke au mume (ona 26.3.1

  • Anatoa kibali cha hekaluni kwa mwongofu mpya (ona 26.4.2).

  • Anamtawaza mwanamume mwongofu mpya kwenye ofisi katika ukuhani wa Haruni.

  • Anamtawaza kijana au mwanamume kwenye ofisi ya kuhani (ona 18.10.2).

  • Anampendekeza mwanamume kutawazwa kuwa mzee au kuhani mkuu (ona 31.2.6). Kibali kutoka urais wa kigingi kinahitajika ili kuendesha usaili huu.

  • Anampendekeza muumini kuhudumu kama mmisionari (ona 24.4.2).

  • Anamwita muumini kuhudumu kama rais wa kikundi katika kata.

  • Anamwita kuhani kuhudumu kama msaidizi katika akidi ya makuhani.

  • Anamsaidia muumini atubu dhambi kubwa (ona sura ya 32).

  • Anamuidhinisha muumini kupokea mkopo wa Perpetual Education Fund, mahali ambapo inatolewa.

  • Anamruhusu muumini atangaze msimamo wake kama mlipaji wa zaka (ona 34.3.1.2).

  • Anaidhinisha matumizi ya matoleo ya mfungo (ona 22.6.1).

Nani anaweza kuendesha usaili

Askofu au mshauri anayempa jukumu

Dhumuni la usaili

  • Anatoa kibali kipya cha hekaluni (ona 26.3.1).

  • Anatoa kibali cha hekaluni ili kushiriki katika ubatizo na uthibitisho kwa niaba (ona 26.4.3).

  • Anatoa kibali cha hekaluni ili kuunganishwa kwa wazazi au kushuhudia kuunganishwa kwa ndugu kwa wazazi (ona 26.4.4).

  • Anamwita muumini kuhudumu katika wito wa kata kama ilivyooneshwa katika 30.8

  • Anatoa ruhusa ya ubatizo na uthibitisho wa mwenye umri wa miaka 8 ambaye ni muumini wa rekodi au ana mzazi au mlezi ambaye ni muumini wa Kanisa (ona 31.2.3.1).

  • Anatoa ruhusa ya kutawazwa kwa mvulana kwenye ofisi ya shemasi au mwalimu (ona 18.10.2).

  • Anatoa Kibali cha Baraka ya Patriaki (ona 18.17).

  • Anatoa idhini ya mtu mwenye ukuhani kufanya ibada ya ukuhani katika kata nyingine, kama hana kibali cha hekalu. (Ona Fomu ya Kibali cha Kufanya Ibada.)

31.2.3

Mahojiano ya Ubatizo na Uthibitisho

31.2.3.1

Watoto Ambao Ni Waumini wa Rekodi

Askofu anashikilia funguo za ukuhani kwa ajili ya kuwabatiza waumini wa rekodi wenye umri wa miaka 8 katika katayake. Kwa sababu hii, yeye au mshauri aliyepewa jukumu anawasaili watu wafuatao kwa ajili ya ubatizo:

  • Watoto wenye umri wa miaka 8 ambao ni waumini wa rekodi.

  • Watoto wenye umri wa miaka 8 ambao siyo waumini wa rekodi bali mzazi au mlezi ni muumini.

  • Waumini wa rekodi wenye umri wa miaka 9 na zaidi ambao ubatizo wao ulicheleweshwa kwa sababu ya ulemavu wa afya ya akili.

Katika usaili, mshiriki wa urais anahakikisha kwamba mtoto anaelewa madhumuni ya ubatizo (ona 2 Nefi 31:5-20). Pia anahakikisha kwamba mtoto anaelewa agano la ubatizo na ana msimamo wa kuliishi (ona Mosia 18:8–10). Hahitaji kutumia orodha ya maswali yaliyobainishwa. Huu siyo usaili wa kuamua ustahili, maadam “watoto wadogo hawahitaji kutubu” (Moroni 8:11).

31.2.3.2

Waongofu

Rais wa misheni anashikilia funguo za ukuhani kwa ajili ya kuwabatiza waongofu. Kwa sababu hii, mmisionari wa muda wote anawasaili:

  • Watu wenye umri wa miaka 9 na kuendelea ambao hawajawahi kamwe kubatizwa na kuthibitishwa. Ona 31.2.3.1 kwa ajili ya upekee kwa wale walio na ulemavu wa afya ya akili.

  • Watoto wenye umri wa miaka 8 na kuendelea ambao wazazi wao siyo waumini wa Kanisa.

  • Watu wenye umri wa miaka 8 na kuendelea ambao wana wazazi ambao pia wanabatizwa na kuthibitishwa.

31.2.4

Mahojiano kwa ajili ya Utawazo katika Ofisi husika katika Ukuhani wa Haruni

Kwa maelezo zaidi, ona 18.10.2.

31.2.5

Usaili wa Vibali vya Hekaluni

Hekalu ni nyumba ya Bwana. Kuingia Hekaluni na kushiriki katika ibada ni fursa takatifu. Fursa hii inahifadhiwa kwa ajili ya wale ambao wamejitayarisha kiroho na kujitahidi kuishi viwango vya Bwana kama ilivyoamuliwa na viongozi wa ukuhani wenye mamlaka.

Ili kufanya uamuzi huu, viongozi wa ukuhani wanamsaili muumini wakitumia maswali katika LCR (ona pia miongozo katika 26.3).

31.2.6

Mahojiano kwa ajili ya Utawazo kwenye Ofisi katika Ukuhani wa Melkizedeki

Askofu wa kigingi anashikilia funguo za ukuhani kwa ajili ya kutunukia Ukuhani wa Melkizedeki. Pia anashikilia funguo kwa ajili ya utawazo kwenye ofisi ya mzee na kuhani kuu.

Kwa idhini ya urais wa kigingi askofu anamsaili muumini kwa kutumia maswali yaliyotolewa kwenye Kumbukumbu ya Utawazo katika Ukuhani wa Melkizedeki.

31.3

Fursa Zingine kwa ajili ya Viongozi Kukutana na Waumini

  • Waumini wanaweza kuomba kukutana na kiongozi wa Kanisa wakati wanapohitaji mwongozo wa kiroho au wana matatizo mazito ya binafsi.

  • Askofu au mtu mwingine anayempa jukumu anakutana na waumini walio na mahitaji ya kimwili (ona 22.6).

  • Mshiriki wa uaskofu anakutana na kila mwenye umri wa miaka11pale anapohama kutoka Msingi kwenda katika akidi ya mashemasi au darasa la wasichana.

31.3.1

Kukutana na Vijana

Askofu au mmoja wa washauri wake hukutana na kila kijana mara mbili kwa mwaka. Angalau moja ya mikutano hii kila mwaka askofu anapaswa kuwepo. Kuanzia mwaka ambao kijana anafikisha miaka16, mikutano yote miwili kwa kipindi chote cha mwaka askofu anapaswa kuwepo kama inawezekana.

Rais wa Wasichana pia ana jukumu la kumtumikia kila msichana binafsi. Anaweza kufanya hivi kwa kukutana na wasichana mmoja mmoja (au akiwepo mtu mzima mwingine).

31.3.1.2

Mada za Kujadiliana

Dhumuni kubwa la mikutano na vijana ni kujenga imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na kuwasaidia vijana Wawafuate Wao. Mikutano hii inapaswa kuwa tukio lenye kuinua kiroho.

31.3.2

Kukutana na Vijana Wakubwa Waseja

Askofu anaweka kipaumbele cha juu kwenye maendeleo ya kiroho ya vijana wakubwa waseja katika kata yake. Yeye au mshauri aliyepewa jukumu hukutana na kila kijana mkubwa mseja angalau mara moja kwa mwaka.

31.3.3

Kukutana na waumini Kujadili Miito na Majukumu Yao

Urais wa kigingi, uaskofu, na viongozi wengine wanakutana binafsi na waumini wanaoripoti kwao kuhudu miito yao.

Kiongozi anaelezea shukrani kwa huduma ya muumini na kuwatia moyo.

31.3.6

Ushauri wa kitaalamu na Matibabu

Viongozi wa Kanisa hawaitwi kuwa washauri wenye weledi au kutoa matibabu. Msaada wanaotoa ni wa kiroho, wakilenga kwenye nguvu ya kukomboa, kuimarisha, kufariji, ya Yesu Kristo. Kwa kuongezea kwenye msaada huu muhimu na wenye uvuvio, baadhi ya waumini wanaweza kunufaika kutokana na ushauri wa watu wenye weledi pale unapopatikana.

31.4

Kukutana na Waumini kwa njia ya Mtandao

Kwa kawaida, viongozi hukutana na waumini ana kwa ana kwa ajili ya usaili na kutoa msaada wa kiroho na kuhudumu. Hata hivyo, kama ni jambo lenye upekee, wanaweza kukutana kwa njia ya mtandao (si ana kwa ana) pale ambapo kukutana ana kwa ana hakuwezekani.