“30. Miito katika Kanisa,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).
“30. Miito katika Kanisa,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla.
30.
Miito katika Kanisa
30.0
Utangulizi
Miito inawapa waumini fursa kuhisi furaha ya kumhudumia Mungu kwa kuwahudumia watoto Wake (ona Mosia 2:17). Miito pia inawasaidia waumini waongeze imani yao na wamkaribie zaidi Bwana.
Siyo sahihi kutamani miito maalumu katika Kanisa (ona Marko 10:42–45; Mafundisho na Maagano 121:34–37). Wala waumini wa Kanisa “hawapandi cheo” kutoka wito mmoja kwenda mwingine. Kuhudumu kwa uaminifu katika wito ni muhimu zaidi kuliko ni aina gani ya wito. Bwana anaheshimu kujitolea kwa wale wote wanaohudumu katika Kanisa Lake.
30.1
Kuamua Ni Nani wa Kumwita
30.1.1
Maelezo ya Jumla
Wale wanaohudumu katika Kanisa wameitwa na Mungu (ona Waebrania 5:4; Makala ya Imani 1:5). Viongozi wanatafuta mwongozo wa Roho katika kuamua ni nani wa kumwita (ona pia 4.2.6). Pia wanazingatia:
-
Ustahili wa muumini (kama ulivyoamuliwa katika usaili).
-
Vipaji na uwezo muumini alio nao, au ambao angeweza kuukuza, ili awabariki wengine.
-
Hali binafsi ya muumini, pamoja na afya yake na kazi.
-
Athari ambayo wito unaweza kuwa nayo juu ya ndoa na familia ya muumini.
Waumini wanabarikiwa kwa ajili ya dhabihu wanayoifanya ili kuhudumu katika Kanisa. Hata hivyo, wito haupaswi kuweka mizigo mizito isiyo ya lazima juu ya watu binafsi na familia. Wala miito haipaswi kufanya iwe vigumu kwa waumini kukamilisha wajibu wa ajira zao.
Kwa kawaida, kila muumini anaitwa kuhudumu katika wito mmoja pekee kwa wakati mmoja kwa kuongezea kwenye kuwa kaka au dada mhudumiaji.
Wakati wa kutoa wito kwa muumini mwenye ndoa, viongozi wanahakikisha kwamba mume au mke anafahamu na anaunga mkono wito. Kabla ya kutoa wito kwa kijana au msichana, viongozi wapate idhini kutoka kwa wazazi au walezi wake.
Kabla wito haujatolewa, askofu kwa makini anarejea upya kumbukumbu ya mtu ya uumini ili kuthibitisha kwamba haijumuishi maelezo ya ufafanuzi au vizuizi rasmi vya uumini.
30.1.2
Miito Kwa Ajili ya Waumini Wapya
Fursa za kuhudumu zinawasaidia waumini wakue kiroho.
Viongozi wa kata wanawapa waumini wapya fursa ya kuhudumu punde tu baada ya kubatizwa na kuthibitishwa.
30.1.3
Miito kwa ajili ya Wale ambao siyo Waumini
Watu ambao siyo waumini wa Kanisa wanaweza kuitwa kwenye baadhi ya nafasi, kama vile mpiga kinanda, mkurugenzi wa muziki, au wito wa kusaidia kupanga Shughuli. Hata hivyo, hawapaswi kuitwa kama walimu, kama mshiriki wa urais wa akidi au urais wa kikundi au kama viongozi wa muziki katika Msingi.
30.1.4
Usiri
Miito na kupumzishwa ni mambo matakatifu. Kwa sababu ya hili, viongozi wanatunza taarifa kuhusu mapendekezo ya wito na kupumzishwa kwa usiri.
30.1.5
Mapendekezo na uthibitisho kwa ajili ya Miito
Chati ya miito inaonesha nani anaweza kufanya mapendekezo kwa ajili ya kila wito na nani anayetoa idhini (ona 30.8).
Maaskofu na marais wa vigingi kwa umakini wanafikiria kila pendekezo, wakitambua kwamba limefanywa kwa sala. Uaskofu au urais wa kigingi unalo jukumu la mwisho la kupokea mwongozo wa kiungu kuhusu nani wa kuitwa.
30.2
Kutoa Wito
Kupokea wito wa kuhudumu kunapaswa kuwa tukio lenye maana kiroho kwa muumini.
Wakati kiongozi anapotoa wito, anaelezea kwamba wito umekuja kutoka kwa Bwana.
Kiongozi anaweza pia:
-
Kuelezea dhumuni, umuhimu, na majukumu ya wito huo.
-
Kumtia moyo muumini kutafuta Roho wa Bwana katika kukamilisha wito.
-
Kushuhudia kwamba Bwana atamsaidia muumini na atambariki kwa ajili ya kuhudumu kwa uaminifu.
-
Mwambie muumini ni nani watatoa mafunzo na msaada kwa ajili ya wito.
-
Mtaarifu muumini juu ya mkutano wowote ambao yeye anapaswa kuhudhuria na nyenzo zozote ambazo zinapatikana.
30.3
Kuwapigia Kura za Kuwakubali Waumini katika Miito
Wale ambao wameitwa kwenye karibia nafasi nyingi katika Kanisa wanapaswa kutambulishwa rasmi kwa ajili ya kura za kukubaliwa kabla hawajaanza kuhudumu (ona Mafundisho na Maagano 28:13; Mafundisho na Maagano 42:11).
Mtu ambaye anayeendesha zoezi la kura za kukubaliwa kwanza anatangaza nani alikuwa amepumzishwa kutoka katika nafasi hiyo (kama inahusika). Anawaalika waumini watoe dhihirisho la shukrani kwa ajili ya huduma aliyoitoa mtu yule aliyepumzishwa (ona 30.6).
Wakati wa kutambulishwa mtu kwa ajili ya kupigiwa kura ya kukubaliwa, kiongozi wa ukuhani mwenye mamlaka anamwalika mhusika kusimama. Kiongozi anaweza kutumia maneno kama yafuatayo:
“[Jina] ameitwa kama [nafasi]. Wale wanaounga mkono, kumthibitisha [yeye] wanaweza kuonesha kwa kuinua mkono. [Kaa kimya kwa muda mfupi.] Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza pia kuonesha. [Kaa kimya kwa muda mfupi.]”
Kama mshiriki mwenye msimamo mzuri anapinga wito huo, kiongozi anayeongoza au kiongozi mwingine wa ukuhani mwenye jukumu anakutana naye kwa faragha baada ya mkutano.
30.4
Kuwasimika Waumini ili Kuhudumu katika Miito
Kwa maelezo zaidi, ona 18.11.
30.6
Kuwapumzisha Waumini kutokakwenye Miito
Wakati rais au askofu anapopumzishwa washauri wake nao wanapumzishwa wakati huo huo.
Kutoa mapumziko ni fursa muhimu kwa kiongozi kuonesha shukrani na kutambua mkono wa Mungu katika huduma ya muumini. Kiongozi anakutana na muumini kwa faragha kumfahamisha juu ya kupumzishwa huko kabla ya kutangazwa kwa watu wote. Wale tu wanaohitaji kujua wanataarifiwa juu ya kupumzishwa kabla ya kutangazwa.
Kiongozi wa ukuhani mwenye mamlaka anatangaza kupumzishwa katika kikao kile kile ambacho mtu alipigiwa kura ya kukubaliwa. Kiongozi anaweza kutumia maneno kama yafuatayo:
“[Jina] amepumzishwa kama [nafasi]. Wote ambao wangependa kuonesha shukrani zao [kwake] kwa huduma nzuri wanaweza kuonesha kwa kuinua mkono.”
Kiongozi haulizi kama kuna yeyote anayepinga.
30.8
Chati ya Miito
30.8.1
Miito ya Kata
Wito |
Amependekezwa na |
Ameidhinishwa na |
Ameungwa mkono na |
Ameitwa na kusimikwa na |
---|---|---|---|---|
Wito | Amependekezwa na Rais wa Kigingi, akitumia LCR | Ameidhinishwa na Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili | Ameungwa mkono na Waumini wa Kata | Ameitwa na kusimikwa na Rais wa kigingi baada ya kupokea idhini kutoka kwa Urais wa Kwanza |
Wito | Amependekezwa na Askofu | Ameidhinishwa na Uraisi wa Kigingi na baraza kuu | Ameungwa mkono na Waumini wa Kata | Ameitwa na kusimikwa na Rais wa Kigingi au mshauri aliyepangiwa |
Wito | Amependekezwa na Uaskofu | Ameidhinishwa na Uraisi wa Kigingi na baraza kuu | Ameungwa mkono na Waumini wa Kata | Ameitwa na kusimikwa na Rais wa Kigingi au mshauri aliyepewa jukumu au mjumbe wa baraza kuu |
Wito | Amependekezwa na Uaskofu | Ameidhinishwa na Uraisi wa Kigingi na baraza kuu | Ameungwa mkono na Waumini wa Kata | Ameitwa na kusimikwa na Rais wa Kigingi au mshauri aliyepewa jukumu au mjumbe wa baraza kuu |
Wito | Amependekezwa na Urais wa kigingi (Ukishauriana na askofu) | Ameidhinishwa na Uraisi wa Kigingi na baraza kuu | Ameungwa mkono na Waumini wa Kata | Ameitwa na kusimikwa na Rais wa kigingi |
Wito | Amependekezwa na Rais wa akidi (akishauriana na askofu) | Ameidhinishwa na Uraisi wa Kigingi na baraza kuu | Ameungwa mkono na Waumini wa Kata | Ameitwa na kusimikwa na Rais wa Kigingi au mshauri aliyepewa jukumu au mjumbe wa baraza kuu |
Wito Miito mingine ya akidi ya wazee | Amependekezwa na Urais wa akidi | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Washiriki wa akidi | Ameitwa na kusimikwa na Rais wa akidi au mshauri aliyepangiwa |
Wito Marais wa vikundi katika kata | Amependekezwa na Uaskofu | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Waumini wa Kata | Ameitwa na kusimikwa na Askofu |
Wito Washauri katika urais wa vikundi katika kata | Amependekezwa na Rais wa kikundi | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Waumini wa Kata | Ameitwa na kusimikwa na Askofu au mshauri aliyepewa jukumu |
Wito Miito mingine ya Muungano wa usaidizi katika kata | Amependekezwa na Urais wa Muungano wa Usaidizi | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Washiriki wa Muungano wa Usaidizi | Ameitwa na kusimikwa na Askofu au mshauri aliyepewa jukumu |
Wito Miito mingine ya Wasichana, Msingi, na Shule ya Jumapili katika Kata | Amependekezwa na Urais wa kikundi | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Waumini wa Kata | Ameitwa na kusimikwa na Askofu au mshauri aliyepewa jukumu |
Wito | Amependekezwa na Uaskofu (kwa kushauriana na marais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi) | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Waumini wa Kata | Ameitwa na kusimikwa na Askofu au mshauri aliyepewa jukumu |
Wito | Amependekezwa na Uaskofu au marais wa akidi ya wazee na wa Muungano wa Usaidizi | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Waumini wa Kata | Ameitwa na kusimikwa na Askofu au mshauri aliyepewa jukumu |
Wito | Amependekezwa na Uaskofu (kwa kushauriana na marais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi) | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Waumini wa Kata | Ameitwa na kusimikwa na Askofu au mshauri aliyepewa jukumu |
Wito | Amependekezwa na Askofu (kama rais wa akidi ya makuhani) | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Washiriki wa akidi | Ameitwa na kusimikwa na Askofu |
Wito | Amependekezwa na Uaskofu | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Washiriki wa akidi | Ameitwa na kusimikwa na Ameitwa na askofu au mshauri aliyepewa jukumu; amesimikwa na askofu |
Wito Washauri katika urais wa akidi ya walimu na mashemasi na makatibu wa akidi | Amependekezwa na Rais wa akidi | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Washiriki wa akidi | Ameitwa na kusimikwa na Askofu au mshauri aliyepewa jukumu |
Wito | Amependekezwa na Uaskofu (ukishauriana na urais wa Wasichana) | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Washiriki wa darasa | Ameitwa na kusimikwa na Askofu au mshauri aliyepewa jukumu |
Wito Washauri katika urais wa darasa la wasichana na makatibu wa darasa | Amependekezwa na Rais wa Darasa | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Washiriki wa darasa | Ameitwa na kusimikwa na Askofu au mshauri aliyepewa jukumu |
Wito Miito mingine ya kata | Amependekezwa na Uaskofu | Ameidhinishwa na Uaskofu | Ameungwa mkono na Waumini wa Kata | Ameitwa na kusimikwa na Askofu au mshauri aliyepewa jukumu |
30.8.2
Miito ya Tawi
Wito |
Amependekezwa na |
Ameidhinishwa na |
Ameungwa mkono na |
Ameitwa na kusimikwa na | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Wito | Amependekezwa na Urais wa kigingi, misheni, au wilaya | Ameidhinishwa na Urais wa Kigingi na baraza kuu au urais wa misheni | Ameungwa mkono na Waumini wa tawi | Ameitwa na kusimikwa na Rais wa Kigingi, au misheni (au rais wa wilaya kama amepewa jukumu) | ||||||||||||
Wito | Amependekezwa na Rais wa tawi | Ameidhinishwa na Urais wa kigingi na baraza kuu au urais wa misheni (au, inapokuwa imeruhusiwa na rais wa misheni, urais wa wilaya) | Ameungwa mkono na Waumini wa tawi | Ameitwa na kusimikwa na Kigingi, misheni, au rais wa wilaya au mshauri aliyepewa jukumu | ||||||||||||
Wito | Amependekezwa na Urais wa tawi | Ameidhinishwa na Urais wa kigingi na baraza kuu au urais wa misheni (au, inapokuwa imeruhusiwa na rais wa misheni, urais wa wilaya) | Ameungwa mkono na Waumini wa tawi | Ameitwa na kusimikwa na Rais wa kigingi au mshauri aliyepewa jukumu au mjumbe wa baraza kuu (kwa ajili ya matawi katika vigingi); rais wa wilaya au kiongozi wa ukuhani anaye mteua (kwa matawi katika misheni) | ||||||||||||
Wito | Amependekezwa na Kigingi, wilaya, au urais wa wilaya (kwa kushauriana na rais wa tawi) | Ameidhinishwa na Urais wa kigingi na baraza kuu au urais wa misheni (au, inapokuwa imeruhusiwa na rais wa misheni, urais wa wilaya) | Ameungwa mkono na Waumini wa tawi | Ameitwa na kusimikwa na Rais wa Kigingi, au misheni (au rais wa wilaya kama amepewa jukumu) | ||||||||||||
Wito | Amependekezwa na Urais wa akidi (ukishauriana na rais wa tawi) | Ameidhinishwa na Urais wa kigingi na baraza kuu au urais wa misheni (au, inapokuwa imeruhusiwa na rais wa misheni, urais wa wilaya) | Ameungwa mkono na Waumini wa tawi | Ameitwa na kusimikwa na Kigingi au rais wa misheni au mshauri aliyepewa jukumu au mjumbe wa baraza kuu (au rais wa wilaya au kiongozi mwingine wa ukuhani kama amepewa jukumu) | ||||||||||||
Wito Miito mingine katika tawi | Amependekezwa na Ona 30.8.1, kubadili rais wa tawi kuwa askofu na tawi kuwa kata. | Ameidhinishwa na Ona 30.8.1, kubadili rais wa tawi kuwa askofu na tawi kuwa kata. | Ameungwa mkono na Ona 30.8.1, kubadili rais wa tawi kuwa askofu na tawi kuwa kata. | Ameitwa na kusimikwa na Ona 30.8.1, kubadili rais wa tawi kuwa askofu na tawi kuwa kata. |