“31. Usaili na Mikutano Mingine na Waumini,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).
“31. Usaili na Mikutano Mingine na Waumini,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla
31.
Usaili na Mikutano Mingine na Waumini
31.0
Utangulizi
Yesu Kristo mara nyingi aliwatumikia wengine mmoja baada ya mwingine (ona, kwa mfano, Yohana 4:5–26; 3 Nefi 17:21) Anampenda kila mmoja wa watoto wa Mungu. Anawasaidia kila mtu binafsi.
Sura hii inaweza kuwasaidia viongozi wote ambao wana fursa ya kukutana na waumini binafsi.
31.1
Kanuni Zinazoongoza
31.1.1
Jiandae Kiroho
Jiandae mwenyewe kiroho kupitia sala, kujifunza maandiko, na kuishi kwa haki. Sikiliza minog’ono ya Roho Mtakatifu.
31.1.2
Msaidie muumini Ahisi Upendo wa Mungu
Wakati waumini wanapokujia kwa ajili ya usaili au kwa ajili ya msaada kutokana na changamoto binafsi, mara nyingi kile wanachohitaji zaidi ni kujua kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda.
Maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho humwalika Roho na hufundisha maandiko ya kweli. Yatumie kuwatia moyo na kuwapa tumaini, siyo kulaani, kulazimisha, au kusababisha hofu (ona Lukaa 9:56).
31.1.3
Msaidie Muumini Avute Nguvu ya Mwokozi
Watie moyo waumini wamgeukie Yeye. Wasaidie wavute nguvu Zake za kuimarisha, kufariji, na kukomboa.
31.1.4
Msaidie Muumini Ahisi Faraja na Salama
Siku zote mpe muumini uchaguzi wa uwepo wa mtu mwingine wakati wa usaili au mkutano. Unapokutana na muumini wa jinsia tofauti, mtoto, au kijana, hakikisha kwamba mzazi au mtu mzima mwingine yupo. Mzazi au mtu mzima huyo anaweza kujiunga na mkutano au kungoja nje ya chumba, kutegemeana na matakwa ya muumini ambaye unakutana naye.
Usitoe taarifa za siri kwa mtu yeyote—ikijumuisha mke wako au kiongozi mwingine wa Kanisa—isipokuwa kama muumini anaruhusu.
31.1.5
Uliza Maswali Yenye Mwongozo wa Kiungu na Sikiliza kwa Makini
Unapokutana na muumini, uliza maswali ambayo yatakusaidia uelewe hali yake.
Wakati muumini anapozungumza, sikiliza kwa makini na kwa usikivu.
31.1.6
Himiza Kujitegemea
Kwa sababu ya upendo wako kwa waumini, unaweza kutaka kutoa ufumbuzi kwa matatizo yao papo hapo. Hata hivyo, utawabariki zaidi kwa kuwasaidia wapate ufumbuzi wao wenyewe na wafanye maamuzi yao wenyewe (ona Mafundisho na Maagano 9:8).
31.1.7
Saidia Juhudi za Kutubu
Askofu au rais wa kigingi ndiyo pekee wanaoweza kumsaidia mtu atatue dhambi kubwa. Baadhi ya hizi zimeorodheshwa katika 32.6. Kama muumini amefanya yoyote kati ya dhambi hizi, anapaswa kukutana na askofu au rais wa kigingi mara moja.
31.1.8
Jibu kwa Usahihi kuhusu Unyanyasaji
Unyanyasaji hauwezi kuvumiliwa katika sura yoyote. Chukulia taarifa za unyanyasaji kwa uzito unaostahili. Kama unafahamu kwamba mtu fulani amenyanyaswa, toa taarifa ya unyanyasaji kwa mamlaka ya kiserikali na shauriana na askofu. Mwongozo kwa ajili ya kutoa taarifa na kujibu unyanyasaji umetolewa katika 38.6.2
31.2
usaili
31.2.1
Madhumuni ya Usaili
Kwa ujumla,viongozi wa Kanisa wanawasaili waumini ili kubaini ikiwa wao:
-
Wako tayari kupokea ibada au kushiriki katika ibada.
-
Wanapaswa kuitwa kwenye nafasi katika Kanisa.
31.2.2
Aina za Usaili
Nani anaweza kuendesha usaili |
Dhumuni la usaili |
---|---|
Nani anaweza kuendesha usaili Askofu peke yake | Dhumuni la usaili
|
Nani anaweza kuendesha usaili Askofu au mshauri anayempa jukumu | Dhumuni la usaili
|
31.2.3
Mahojiano ya Ubatizo na Uthibitisho
31.2.3.1
Watoto Ambao Ni Waumini wa Rekodi
Askofu anashikilia funguo za ukuhani kwa ajili ya kuwabatiza waumini wa rekodi wenye umri wa miaka 8 katika katayake. Kwa sababu hii, yeye au mshauri aliyepewa jukumu anawasaili watu wafuatao kwa ajili ya ubatizo:
-
Watoto wenye umri wa miaka 8 ambao ni waumini wa rekodi.
-
Watoto wenye umri wa miaka 8 ambao siyo waumini wa rekodi bali mzazi au mlezi ni muumini.
-
Waumini wa rekodi wenye umri wa miaka 9 na zaidi ambao ubatizo wao ulicheleweshwa kwa sababu ya ulemavu wa afya ya akili.
Katika usaili, mshiriki wa urais anahakikisha kwamba mtoto anaelewa madhumuni ya ubatizo (ona 2 Nefi 31:5-20). Pia anahakikisha kwamba mtoto anaelewa agano la ubatizo na ana msimamo wa kuliishi (ona Mosia 18:8–10). Hahitaji kutumia orodha ya maswali yaliyobainishwa. Huu siyo usaili wa kuamua ustahili, maadam “watoto wadogo hawahitaji kutubu” (Moroni 8:11).
31.2.3.2
Waongofu
Rais wa misheni anashikilia funguo za ukuhani kwa ajili ya kuwabatiza waongofu. Kwa sababu hii, mmisionari wa muda wote anawasaili:
-
Watu wenye umri wa miaka 9 na kuendelea ambao hawajawahi kamwe kubatizwa na kuthibitishwa. Ona 31.2.3.1 kwa ajili ya upekee kwa wale walio na ulemavu wa afya ya akili.
-
Watoto wenye umri wa miaka 8 na kuendelea ambao wazazi wao siyo waumini wa Kanisa.
-
Watu wenye umri wa miaka 8 na kuendelea ambao wana wazazi ambao pia wanabatizwa na kuthibitishwa.
31.2.4
Mahojiano kwa ajili ya Utawazo katika Ofisi husika katika Ukuhani wa Haruni
Kwa maelezo zaidi, ona 18.10.2.
31.2.5
Usaili wa Vibali vya Hekaluni
Hekalu ni nyumba ya Bwana. Kuingia Hekaluni na kushiriki katika ibada ni fursa takatifu. Fursa hii inahifadhiwa kwa ajili ya wale ambao wamejitayarisha kiroho na kujitahidi kuishi viwango vya Bwana kama ilivyoamuliwa na viongozi wa ukuhani wenye mamlaka.
Ili kufanya uamuzi huu, viongozi wa ukuhani wanamsaili muumini wakitumia maswali katika LCR (ona pia miongozo katika 26.3).
31.2.6
Mahojiano kwa ajili ya Utawazo kwenye Ofisi katika Ukuhani wa Melkizedeki
Askofu wa kigingi anashikilia funguo za ukuhani kwa ajili ya kutunukia Ukuhani wa Melkizedeki. Pia anashikilia funguo kwa ajili ya utawazo kwenye ofisi ya mzee na kuhani kuu.
Kwa idhini ya urais wa kigingi askofu anamsaili muumini kwa kutumia maswali yaliyotolewa kwenye Kumbukumbu ya Utawazo katika Ukuhani wa Melkizedeki.
31.3
Fursa Zingine kwa ajili ya Viongozi Kukutana na Waumini
-
Waumini wanaweza kuomba kukutana na kiongozi wa Kanisa wakati wanapohitaji mwongozo wa kiroho au wana matatizo mazito ya binafsi.
-
Askofu au mtu mwingine anayempa jukumu anakutana na waumini walio na mahitaji ya kimwili (ona 22.6).
-
Mshiriki wa uaskofu anakutana na kila mwenye umri wa miaka11pale anapohama kutoka Msingi kwenda katika akidi ya mashemasi au darasa la wasichana.
31.3.1
Kukutana na Vijana
Askofu au mmoja wa washauri wake hukutana na kila kijana mara mbili kwa mwaka. Angalau moja ya mikutano hii kila mwaka askofu anapaswa kuwepo. Kuanzia mwaka ambao kijana anafikisha miaka16, mikutano yote miwili kwa kipindi chote cha mwaka askofu anapaswa kuwepo kama inawezekana.
Rais wa Wasichana pia ana jukumu la kumtumikia kila msichana binafsi. Anaweza kufanya hivi kwa kukutana na wasichana mmoja mmoja (au akiwepo mtu mzima mwingine).
31.3.1.2
Mada za Kujadiliana
Dhumuni kubwa la mikutano na vijana ni kujenga imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na kuwasaidia vijana Wawafuate Wao. Mikutano hii inapaswa kuwa tukio lenye kuinua kiroho.
31.3.2
Kukutana na Vijana Wakubwa Waseja
Askofu anaweka kipaumbele cha juu kwenye maendeleo ya kiroho ya vijana wakubwa waseja katika kata yake. Yeye au mshauri aliyepewa jukumu hukutana na kila kijana mkubwa mseja angalau mara moja kwa mwaka.
31.3.3
Kukutana na waumini Kujadili Miito na Majukumu Yao
Urais wa kigingi, uaskofu, na viongozi wengine wanakutana binafsi na waumini wanaoripoti kwao kuhudu miito yao.
Kiongozi anaelezea shukrani kwa huduma ya muumini na kuwatia moyo.
31.3.6
Ushauri wa kitaalamu na Matibabu
Viongozi wa Kanisa hawaitwi kuwa washauri wenye weledi au kutoa matibabu. Msaada wanaotoa ni wa kiroho, wakilenga kwenye nguvu ya kukomboa, kuimarisha, kufariji, ya Yesu Kristo. Kwa kuongezea kwenye msaada huu muhimu na wenye uvuvio, baadhi ya waumini wanaweza kunufaika kutokana na ushauri wa watu wenye weledi pale unapopatikana.
31.4
Kukutana na Waumini kwa njia ya Mtandao
Kwa kawaida, viongozi hukutana na waumini ana kwa ana kwa ajili ya usaili na kutoa msaada wa kiroho na kuhudumu. Hata hivyo, kama ni jambo lenye upekee, wanaweza kukutana kwa njia ya mtandao (si ana kwa ana) pale ambapo kukutana ana kwa ana hakuwezekani.