Vitabu vya Maelekezo na Miito
30. Miito katika Kanisa


“30. Miito katika Kanisa,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“30. Miito katika Kanisa,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Picha
watu wakiinua mikono ya kuume

30.

Miito katika Kanisa

30.0

Utangulizi

Miito inawapa waumini fursa kuhisi furaha ya kumhudumia Mungu kwa kuwahudumia watoto Wake (ona Mosia 2:17). Miito pia inawasaidia waumini waongeze imani yao na wamkaribie zaidi Bwana.

Siyo sahihi kutamani miito maalumu katika Kanisa (ona Marko 10:42–45; Mafundisho na Maagano 121:34–37). Wala waumini wa Kanisa “hawapandi cheo” kutoka wito mmoja kwenda mwingine. Kuhudumu kwa uaminifu katika wito ni muhimu zaidi kuliko ni aina gani ya wito. Bwana anaheshimu kujitolea kwa wale wote wanaohudumu katika Kanisa Lake.

30.1

Kuamua Ni Nani wa Kumwita

30.1.1

Maelezo ya Jumla

Wale wanaohudumu katika Kanisa wameitwa na Mungu (ona Waebrania 5:4; Makala ya Imani 1:5). Viongozi wanatafuta mwongozo wa Roho katika kuamua ni nani wa kumwita (ona pia 4.2.6). Pia wanazingatia:

  • Ustahili wa muumini (kama ulivyoamuliwa katika usaili).

  • Vipaji na uwezo muumini alio nao, au ambao angeweza kuukuza, ili awabariki wengine.

  • Hali binafsi ya muumini, pamoja na afya yake na kazi.

  • Athari ambayo wito unaweza kuwa nayo juu ya ndoa na familia ya muumini.

Waumini wanabarikiwa kwa ajili ya dhabihu wanayoifanya ili kuhudumu katika Kanisa. Hata hivyo, wito haupaswi kuweka mizigo mizito isiyo ya lazima juu ya watu binafsi na familia. Wala miito haipaswi kufanya iwe vigumu kwa waumini kukamilisha wajibu wa ajira zao.

Kwa kawaida, kila muumini anaitwa kuhudumu katika wito mmoja pekee kwa wakati mmoja kwa kuongezea kwenye kuwa kaka au dada mhudumiaji.

Wakati wa kutoa wito kwa muumini mwenye ndoa, viongozi wanahakikisha kwamba mume au mke anafahamu na anaunga mkono wito. Kabla ya kutoa wito kwa kijana au msichana, viongozi wapate idhini kutoka kwa wazazi au walezi wake.

Kabla wito haujatolewa, askofu kwa makini anarejea upya kumbukumbu ya mtu ya uumini ili kuthibitisha kwamba haijumuishi maelezo ya ufafanuzi au vizuizi rasmi vya uumini.

30.1.2

Miito Kwa Ajili ya Waumini Wapya

Fursa za kuhudumu zinawasaidia waumini wakue kiroho.

Viongozi wa kata wanawapa waumini wapya fursa ya kuhudumu punde tu baada ya kubatizwa na kuthibitishwa.

30.1.3

Miito kwa ajili ya Wale ambao siyo Waumini

Watu ambao siyo waumini wa Kanisa wanaweza kuitwa kwenye baadhi ya nafasi, kama vile mpiga kinanda, mkurugenzi wa muziki, au wito wa kusaidia kupanga Shughuli. Hata hivyo, hawapaswi kuitwa kama walimu, kama mshiriki wa urais wa akidi au urais wa kikundi au kama viongozi wa muziki katika Msingi.

30.1.4

Usiri

Miito na kupumzishwa ni mambo matakatifu. Kwa sababu ya hili, viongozi wanatunza taarifa kuhusu mapendekezo ya wito na kupumzishwa kwa usiri.

30.1.5

Mapendekezo na uthibitisho kwa ajili ya Miito

Chati ya miito inaonesha nani anaweza kufanya mapendekezo kwa ajili ya kila wito na nani anayetoa idhini (ona 30.8).

Maaskofu na marais wa vigingi kwa umakini wanafikiria kila pendekezo, wakitambua kwamba limefanywa kwa sala. Uaskofu au urais wa kigingi unalo jukumu la mwisho la kupokea mwongozo wa kiungu kuhusu nani wa kuitwa.

30.2

Kutoa Wito

Kupokea wito wa kuhudumu kunapaswa kuwa tukio lenye maana kiroho kwa muumini.

Wakati kiongozi anapotoa wito, anaelezea kwamba wito umekuja kutoka kwa Bwana.

Kiongozi anaweza pia:

  • Kuelezea dhumuni, umuhimu, na majukumu ya wito huo.

  • Kumtia moyo muumini kutafuta Roho wa Bwana katika kukamilisha wito.

  • Kushuhudia kwamba Bwana atamsaidia muumini na atambariki kwa ajili ya kuhudumu kwa uaminifu.

  • Mwambie muumini ni nani watatoa mafunzo na msaada kwa ajili ya wito.

  • Mtaarifu muumini juu ya mkutano wowote ambao yeye anapaswa kuhudhuria na nyenzo zozote ambazo zinapatikana.

30.3

Kuwapigia Kura za Kuwakubali Waumini katika Miito

Wale ambao wameitwa kwenye karibia nafasi nyingi katika Kanisa wanapaswa kutambulishwa rasmi kwa ajili ya kura za kukubaliwa kabla hawajaanza kuhudumu (ona Mafundisho na Maagano 28:13; Mafundisho na Maagano 42:11).

Mtu ambaye anayeendesha zoezi la kura za kukubaliwa kwanza anatangaza nani alikuwa amepumzishwa kutoka katika nafasi hiyo (kama inahusika). Anawaalika waumini watoe dhihirisho la shukrani kwa ajili ya huduma aliyoitoa mtu yule aliyepumzishwa (ona 30.6).

Wakati wa kutambulishwa mtu kwa ajili ya kupigiwa kura ya kukubaliwa, kiongozi wa ukuhani mwenye mamlaka anamwalika mhusika kusimama. Kiongozi anaweza kutumia maneno kama yafuatayo:

“[Jina] ameitwa kama [nafasi]. Wale wanaounga mkono, kumthibitisha [yeye] wanaweza kuonesha kwa kuinua mkono. [Kaa kimya kwa muda mfupi.] Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza pia kuonesha. [Kaa kimya kwa muda mfupi.]”

Kama mshiriki mwenye msimamo mzuri anapinga wito huo, kiongozi anayeongoza au kiongozi mwingine wa ukuhani mwenye jukumu anakutana naye kwa faragha baada ya mkutano.

30.4

Kuwasimika Waumini ili Kuhudumu katika Miito

Kwa maelezo zaidi, ona 18.11.

30.6

Kuwapumzisha Waumini kutokakwenye Miito

Wakati rais au askofu anapopumzishwa washauri wake nao wanapumzishwa wakati huo huo.

Kutoa mapumziko ni fursa muhimu kwa kiongozi kuonesha shukrani na kutambua mkono wa Mungu katika huduma ya muumini. Kiongozi anakutana na muumini kwa faragha kumfahamisha juu ya kupumzishwa huko kabla ya kutangazwa kwa watu wote. Wale tu wanaohitaji kujua wanataarifiwa juu ya kupumzishwa kabla ya kutangazwa.

Kiongozi wa ukuhani mwenye mamlaka anatangaza kupumzishwa katika kikao kile kile ambacho mtu alipigiwa kura ya kukubaliwa. Kiongozi anaweza kutumia maneno kama yafuatayo:

“[Jina] amepumzishwa kama [nafasi]. Wote ambao wangependa kuonesha shukrani zao [kwake] kwa huduma nzuri wanaweza kuonesha kwa kuinua mkono.”

Kiongozi haulizi kama kuna yeyote anayepinga.

30.8

Chati ya Miito

30.8.1

Miito ya Kata

Wito

Amependekezwa na

Ameidhinishwa na

Ameungwa mkono na

Ameitwa na kusimikwa na

Wito

Askofu2

Amependekezwa na

Rais wa Kigingi, akitumia LCR

Ameidhinishwa na

Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

Ameungwa mkono na

Waumini wa Kata

Ameitwa na kusimikwa na

Rais wa kigingi baada ya kupokea idhini kutoka kwa Urais wa Kwanza

Wito

Washauri katika uaskofu2

Amependekezwa na

Askofu

Ameidhinishwa na

Uraisi wa Kigingi na baraza kuu

Ameungwa mkono na

Waumini wa Kata

Ameitwa na kusimikwa na

Rais wa Kigingi au mshauri aliyepangiwa

Wito

Karani wa Kata

Amependekezwa na

Uaskofu

Ameidhinishwa na

Uraisi wa Kigingi na baraza kuu

Ameungwa mkono na

Waumini wa Kata

Ameitwa na kusimikwa na

Rais wa Kigingi au mshauri aliyepewa jukumu au mjumbe wa baraza kuu

Wito

Katibu Mtendaji wa Kata

Amependekezwa na

Uaskofu

Ameidhinishwa na

Uraisi wa Kigingi na baraza kuu

Ameungwa mkono na

Waumini wa Kata

Ameitwa na kusimikwa na

Rais wa Kigingi au mshauri aliyepewa jukumu au mjumbe wa baraza kuu

Wito

Rais wa Akidi ya Wazee

Amependekezwa na

Urais wa kigingi (Ukishauriana na askofu)

Ameidhinishwa na

Uraisi wa Kigingi na baraza kuu

Ameungwa mkono na

Waumini wa Kata

Ameitwa na kusimikwa na

Rais wa kigingi

Wito

Washauri katika urais wa akidi ya wazee

Amependekezwa na

Rais wa akidi (akishauriana na askofu)

Ameidhinishwa na

Uraisi wa Kigingi na baraza kuu

Ameungwa mkono na

Waumini wa Kata

Ameitwa na kusimikwa na

Rais wa Kigingi au mshauri aliyepewa jukumu au mjumbe wa baraza kuu

Wito

Miito mingine ya akidi ya wazee

Amependekezwa na

Urais wa akidi

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Washiriki wa akidi

Ameitwa na kusimikwa na

Rais wa akidi au mshauri aliyepangiwa

Wito

Marais wa vikundi katika kata

Amependekezwa na

Uaskofu

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Waumini wa Kata

Ameitwa na kusimikwa na

Askofu

Wito

Washauri katika urais wa vikundi katika kata

Amependekezwa na

Rais wa kikundi

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Waumini wa Kata

Ameitwa na kusimikwa na

Askofu au mshauri aliyepewa jukumu

Wito

Miito mingine ya Muungano wa usaidizi katika kata

Amependekezwa na

Urais wa Muungano wa Usaidizi

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Washiriki wa Muungano wa Usaidizi

Ameitwa na kusimikwa na

Askofu au mshauri aliyepewa jukumu

Wito

Miito mingine ya Wasichana, Msingi, na Shule ya Jumapili katika Kata

Amependekezwa na

Urais wa kikundi

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Waumini wa Kata

Ameitwa na kusimikwa na

Askofu au mshauri aliyepewa jukumu

Wito

Kiongozi wa kazi ya umisionari katika kata (mshiriki wa urais wa akidi ya wazee anaweza kutimiza jukumu hili, kama ni hivyo, hahitaji kuitwa ,kupigiwa kura ya kukubaliwa, au kusimikwa kwa kipekee)

Amependekezwa na

Uaskofu (kwa kushauriana na marais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi)

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Waumini wa Kata

Ameitwa na kusimikwa na

Askofu au mshauri aliyepewa jukumu

Wito

Wamisionari wa Kata

Amependekezwa na

Uaskofu au marais wa akidi ya wazee na wa Muungano wa Usaidizi

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Waumini wa Kata

Ameitwa na kusimikwa na

Askofu au mshauri aliyepewa jukumu

Wito

Kiongozi wa hekalu na historia ya familia wa kata (mshiriki wa urais wa Akidi ya Wazee anaweza kutimiza jukumu hili; kama ndivyo, hahitaji kuitwa, kupigiwa kura ya kukubaliwa, au kusimikwa kwa kipekee)

Amependekezwa na

Uaskofu (kwa kushauriana na marais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi)

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Waumini wa Kata

Ameitwa na kusimikwa na

Askofu au mshauri aliyepewa jukumu

Wito

Wasaidizi kwa rais wa akidi ya makuhani

Amependekezwa na

Askofu (kama rais wa akidi ya makuhani)

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Washiriki wa akidi

Ameitwa na kusimikwa na

Askofu

Wito

Marais wa akidi za walimu na mashemasi

Amependekezwa na

Uaskofu

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Washiriki wa akidi

Ameitwa na kusimikwa na

Ameitwa na askofu au mshauri aliyepewa jukumu; amesimikwa na askofu

Wito

Washauri katika urais wa akidi ya walimu na mashemasi na makatibu wa akidi

Amependekezwa na

Rais wa akidi

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Washiriki wa akidi

Ameitwa na kusimikwa na

Askofu au mshauri aliyepewa jukumu

Wito

Marais wa darasa la Wasichana

Amependekezwa na

Uaskofu (ukishauriana na urais wa Wasichana)

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Washiriki wa darasa

Ameitwa na kusimikwa na

Askofu au mshauri aliyepewa jukumu

Wito

Washauri katika urais wa darasa la wasichana na makatibu wa darasa

Amependekezwa na

Rais wa Darasa

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Washiriki wa darasa

Ameitwa na kusimikwa na

Askofu au mshauri aliyepewa jukumu

Wito

Miito mingine ya kata

Amependekezwa na

Uaskofu

Ameidhinishwa na

Uaskofu

Ameungwa mkono na

Waumini wa Kata

Ameitwa na kusimikwa na

Askofu au mshauri aliyepewa jukumu

  1. Waunganishaji watendaji katika hekalu hawapaswi kuitwa kuhudumu katika uaskofu. Waunganishaji wanaitwa chini ya maelekezo ya Rais wa Kanisa.

30.8.2

Miito ya Tawi

Wito

Amependekezwa na

Ameidhinishwa na

Ameungwa mkono na

Ameitwa na kusimikwa na

Wito

Rais wa Tawi1

Amependekezwa na

Urais wa kigingi, misheni, au wilaya

Ameidhinishwa na

Urais wa Kigingi na baraza kuu au urais wa misheni

Ameungwa mkono na

Waumini wa tawi

Ameitwa na kusimikwa na

Rais wa Kigingi, au misheni (au rais wa wilaya kama amepewa jukumu)

Wito

Washauri katika urais wa tawi1

Amependekezwa na

Rais wa tawi

Ameidhinishwa na

Urais wa kigingi na baraza kuu au urais wa misheni (au, inapokuwa imeruhusiwa na rais wa misheni, urais wa wilaya)

Ameungwa mkono na

Waumini wa tawi

Ameitwa na kusimikwa na

Kigingi, misheni, au rais wa wilaya au mshauri aliyepewa jukumu

Wito

Karani wa tawi, makarani wasaidizi, na katibu mtendaji

Amependekezwa na

Urais wa tawi

Ameidhinishwa na

Urais wa kigingi na baraza kuu au urais wa misheni (au, inapokuwa imeruhusiwa na rais wa misheni, urais wa wilaya)

Ameungwa mkono na

Waumini wa tawi

Ameitwa na kusimikwa na

Rais wa kigingi au mshauri aliyepewa jukumu au mjumbe wa baraza kuu (kwa ajili ya matawi katika vigingi); rais wa wilaya au kiongozi wa ukuhani anaye mteua (kwa matawi katika misheni)

Wito

Rais wa akidi ya wazee

Amependekezwa na

Kigingi, wilaya, au urais wa wilaya (kwa kushauriana na rais wa tawi)

Ameidhinishwa na

Urais wa kigingi na baraza kuu au urais wa misheni (au, inapokuwa imeruhusiwa na rais wa misheni, urais wa wilaya)

Ameungwa mkono na

Waumini wa tawi

Ameitwa na kusimikwa na

Rais wa Kigingi, au misheni (au rais wa wilaya kama amepewa jukumu)

Wito

Washauri katika urais wa akidi ya wazee

Amependekezwa na

Urais wa akidi (ukishauriana na rais wa tawi)

Ameidhinishwa na

Urais wa kigingi na baraza kuu au urais wa misheni (au, inapokuwa imeruhusiwa na rais wa misheni, urais wa wilaya)

Ameungwa mkono na

Waumini wa tawi

Ameitwa na kusimikwa na

Kigingi au rais wa misheni au mshauri aliyepewa jukumu au mjumbe wa baraza kuu (au rais wa wilaya au kiongozi mwingine wa ukuhani kama amepewa jukumu)

Wito

Miito mingine katika tawi

Amependekezwa na

Ona 30.8.1, kubadili rais wa tawi kuwa askofu na tawi kuwa kata.

Ameidhinishwa na

Ona 30.8.1, kubadili rais wa tawi kuwa askofu na tawi kuwa kata.

Ameungwa mkono na

Ona 30.8.1, kubadili rais wa tawi kuwa askofu na tawi kuwa kata.

Ameitwa na kusimikwa na

Ona 30.8.1, kubadili rais wa tawi kuwa askofu na tawi kuwa kata.

  1. Waunganishaji watendaji katika hekalu hawapaswi kuitwa kuhudumu katika urais wa tawi. Waunganishaji wanaitwa chini ya maelekezo ya Rais wa Kanisa.