Vitabu vya Maelekezo na Miito
13. Shule ya Jumapili


“13. Shule ya Jumapili,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“13. Shule ya Jumapili,“ Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
familia ikijifunza maandiko

13.

Shule ya Jumapili

13.1

Dhumuni

Viongozi wa Shule ya Jumapili, walimu, na madarasa:

  • Kuimarisha imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa kufundisha “mafundisho ya ufalme” (Mafundisho na Maagano 88:77).).

  • Inasaidia kujifunza na kufundisha injili kulikojikita nyumbani na kusaidiwa na Kanisa.

  • Inawasaidia waumini wafundishe katika njia ya Mwokozi.

13.2

Uongozi wa Shule ya Jumapili katika Kata

13.2.1

Uaskofu

Uaskofu unasimamia Shule ya Jumapili Kwa kawaida askofu anampangia mmoja wa washauri wake kukamilisha wajibu huu chini ya maelekezo yake.

13.2.2

Rais wa Shule ya Jumapili

13.2.2.1

Kumwita Rais wa Shule ya Jumapili

Askofu anamwita na kumsimika anayeshikilia ukuhani wa Melkizedeki kuwa rais wa Shule ya Jumapili katika kata. Kama washauri wanahitajika, na kama kuna wanaume wa kutosha kuhudumu katika nafasi hizi, rais wa Shule ya Jumapili anaweza kupendekeza mshauri mmoja au wawili.

13.2.2.2

Majukumu

  • Kuhudumu kwenye baraza la kata.

  • Kusimamia juhudi za kuboresha kujifunza na kufundisha injili nyumbani na Kanisani.

  • Kupendekeza kwa uaskofu majina ya waumini watu wazima ili wahudumu kama walimu wa Shule ya Jumapili.

  • Kusaidia, kuhimiza, na kuwaelekeza walimu wa Shule ya Jumapili.

  • Kuongoza mikutano ya baraza la walimu kama itakavyoelekezwa na askofu (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 3).

13.2.3

Walimu wa Shule ya Jumapili

Ili kujiandaa kufundisha, waalimu wa Shule ya Jumapili wanatumia maandiko, Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia, na Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Shule ya Jumapili.

13.3

Madarasa ya Shule ya Jumapili

Madarasa ya Shule ya Jumapili yanafanyika Jumapili ya kwanza na ya tatu ya mwezi.

Kwa idhini ya uaskofu, rais wa Shule ya Jumapili anapanga madarasa kwa ajili ya watu wazima na vijana.

Angalau watu wazima wawili wanaoweza kuwajibika wanapaswa kuwepo katika kila darasa la vijana.

Watu wazima wote wanaofanya kazi na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya ulinzi wa watoto na vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org).

13.4

Kuboresha Kujifunza na Kufundusha katika Kata

Viongozi wa kata wana wajibu kwa ajili ya kuboresha kujifunza na kufundisha katika makundi yao. Wanaweza kumwomba rais wa Shule ya Jumapili wa kata kwa ajili ya msaada kama itahitajika.

13.5

Kuboresha Kujifunza na Kufundisha Nyumbani

Wazazi wanawajibika kuwafundisha injili watoto wao. Wanaweza kumwomba rais wa Shule ya Jumapili awasaidie kujiboresha kama walimu.