Vitabu vya Maelekezo na Miito
12. Msingi


“12. “Msingi,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“12. Msingi,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
familia ikiwa imeshikilia maandiko

12.

Msingi

12.1

Dhumuni na Muundo

Msingi ni kikundi chenye kiini-nyumbani kikisaidiwa na Kanisa. Ni kwa ajili ya watoto wa umri wa miezi 18 hadi miaka 11.

12.1.1

Dhumuni

Msingi huwasaidia watoto:

  • Wahisi upendo wa Baba yao wa Mbinguni na wajifunze kuhusu mpango Wake wa furaha.

  • Wajifunze kuhusu Yesu Kristo na wajibu wake katika mpango wa Baba wa Mbinguni.

  • Wajifunze na waishi injili ya Yesu Kristo.

  • Wahisi, watambue, na wafanyie kazi ushawishi wa Roho Mtakatifu.

  • Wajiandae kwa ajili ya, kufanya, na kuyashika maagano matakatifu.

  • Washiriki katika kazi ya wokovu na kuinuliwa.

12.1.3

Madarasa

Wakati kuna watoto wa kutosha, wanagawanywa kwenye madarasa kutegemea umri wao.

Watoto kwa kawaida wanasonga mbele kutoka Msingi kwenda wasichana au akidi ya mashemasi katika Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 12.

12.1.4

Muda wa Kuimba

Muda wa kuimba unawasaidia watoto wahisi upendo wa Baba wa Mbinguni na wajifunze kuhusu mpango Wake wa furaha. Wakati watoto wanapoimba kuhusu kanuni za injili, Roho Mtakatifu atashuhudia juu ya ukweli wa kanuni hizo.

Urais wa Msingi na kiongozi wa muziki huchagua nyimbo kwa kila mwezi ili kuimarisha kanuni watoto wanazojifunza katika madarasa na nyumbani.

12.1.5

Darasa la Watoto Wadogo

Darasa la watoto wadogo linawasaidia watoto wenye umri wa miezi 18 hadi miaka 3 wahisi upendo wa Baba wa Mbinguni na wajifunze kuhusu mpango Wake wa furaha.

12.2

Kushiriki katika Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa

12.2.1

Kuishi Injili ya Yesu Kristo

12.2.1.2

Kujifunza Injili

Mikutano ya Msingi ya Jumapili. Mshiriki wa urais wa Msingi anaendesha ufunguzi.

Ratiba ni kama ifuatavyo:

Sehemu ya Mkutano

Urefu

Sehemu ya Mkutano

Ufunguzi (sala, maandiko au Makala ya Imani, na mazungumzo—vyote vikitolewa na watoto)

Urefu

Dakika 5

Sehemu ya Mkutano

Muda wa kuimba

Urefu

Dakika 20

Sehemu ya Mkutano

Mabadiliko kwenda Madarasani

Urefu

Dakika 5

Sehemu ya Mkutano

Madarasa na sala ya kufunga

Urefu

Dakika 20

Darasa la watoto wadogo kwa ajili ya watoto wa umri wa miezi 18 hadi miaka 3.linadumu kwa dakika 50. Tazama Watoto Wenu inatoa ratiba iliyopendekezwa.

Mawasilisho ya Watoto kwenye Mkutano wa Sakramenti Mawasilisho ya mwaka ya watoto kwenye mkutano wa sakramenti yanafanyika kipindi cha miezi michache ya mwisho ya mwaka.

Urais wa Msingi na kiongozi wa muziki kwa sala hupanga mawasilisho hayo. Uaskofu unatoa maelekezo. Watoto wanaweza kuimba, kuzungumza, na kushiriki hadithi, maandiko, au shuhuda.

Mkutano wa Maandalizi ya Hekaluni na Ukuhani. Urais wa Msingi unapanga mkutano wa Maandalizi ya Hekaluni na Ukuhani kila mwaka. Uaskofu unatoa maelekezo. Mkutano ni kwa ajili ya watoto wa umri wa miaka 10. Wazazi wanaalikwa.

12.2.1.3

Huduma na Shughuli

Kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 8, watoto wanaweza kuanza kuhudhuria shughuli za Msingi.

Shughuli za Msingi zinafanyika wakati wowote isipokuwa jioni za Jumapili au Jumatatu.

  • Shughuli za Msingi zinafanyika mara mbili kwa mwezi pale inapowezekana.

  • Wavulana na wasichana kwa kawaida hukutana mahali tofauti. Hata hivyo, wanaweza kuungana kwa shughuli fulani au katika sehemu zenye watoto wachache.

Uaskofu unahakikisha kwamba bajeti na shughuli kwa ajili ya wavulana na Wasichana katika Msingi zinatosha na zina usawa.

12.2.1.4

Maendeleo Binafsi

Katika juhudi zao za kuwa zaidi kama Mwokozi, watoto—kuanzia katika mwaka wanapofikisha miaka 8—wanaalikwa kuweka malengo ya kukua kiroho, kijamii, kimwili na kiakili (ona Luka 2:52).

Wanaweza kutumia Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo kwa Watoto ili kuweka na kurekodi malengo.

12.3

Uongozi wa Msingi katika Kata

12.3.1

Uaskofu

Wajibu muhimu zaidi kwa askofu ni kwa ajili ya kizazi kinachoinukia, ikijumuisha watoto. Askofu anaweza kumpangia mshauri ili amsaidie katika wajibu wake huo kwa ajili ya Msingi. Askofu au mshauri aliyempangia anakutana mara kwa mara na rais wa Msingi.

Askofu na Washauri Wake mara kwa mara wanahudhuria Msingi.

12.3.2

Urais wa Msingi

Askofu anamwita na kumsimika mwanamke mtu mzima kuhudumu kama rais wa Msingi katika kata.

Katika kitengo kidogo, rais wa Msingi anaweza kuwa kiongozi pekee aliyeitwa katika Msingi. Katika hali kama hii, anafanya kazi na wazazi kupanga masomo, muda wa kuimba na shughuli. Kama kitengo ni kikubwa vya kutosha, miito ya ziada inaweza kujazwa katika utaratibu huu: washauri, kiongozi wa muziki, walimu na viongozi wa darasa la watoto wadogo, katibu, na viongozi wa shughuli.

Urais wa msingi unawasaidia wazazi wawaandae watoto kuingia na kuendelea kwenye njia ya agano.

Ili kukamilisha hili rais wa Msingi anaweza kumpangia mshiriki wa urais awasaidie wazazi wawaandae watoto wao kubatizwa na kuthibitishwa. Rais wa Msingi anaweza kumpangia mshiriki mwingine wa urais kuwasaidia wazazi kwenye maandalizi ya hekaluni na ukuhani kwa ajili ya watoto wao.

Rais wa Msingi ana majukumu ya ziada yafuatayo. Washauri wake wanamsaidia.

  • Kuhudumu kwenye baraza la kata.

  • Mara kwa mara kufanya mikutano ya urais wa msingi na kukutana na askofu au mshauri wake aliyempanga.

  • Kusaidia kupanga huduma za ubatizo kwa watoto wa rekodi wakati atakapoombwa kufanya hivyo (ona 18.7.2).

  • Kupanga na kuendesha ufunguzi wa mikutano ya Msingi ya Jumapili.

  • Kumhudumia kila mtoto binafsi, walimu, na viongozi katika Msingi.

  • Kuwafundisha viongozi wa Msingi na walimu wajibu wao na kuwasaidia katika wajibu huo kwa kuwatambulisha kwenye miito yao (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi [2016], 38).

  • Kusimamia rekodi, ripoti, bajeti na fedha za Msingi.

12.3.4

Kiongozi wa Muziki na Mpiga Kinanda

Kiongozi wa muziki na mpiga kinanda wanawafundisha watoto injili ya Yesu Kristo kupitia muziki wakati wa muda wa kuimba.

Kama mpiga kinanda hayupo au kinanda hakipo, viongozi wanaweza kutumia muziki uliorekodiwa.

12.3.5

Walimu na Viongozi wa Watoto Wadogo sana

Urais wa Msingi hupendekeza kwa uaskofu wanaume na wanawake wa kuhudumu kama walimu wa Msingi. Waumini hawa wanaitwa kufundisha na kuhudumia kundi la watoto wenye umri maalumu.

Waalimu wa Msingi na viongozi wa shule ya watoto wadogo sana wanafundisha kutoka Njoo,Unifuate—Kwa ajili ya Msingi (umri miaka 3–11) na Tazama Watoto Wenu (watoto wadogo sana).

12.3.6

Viongozi wa Shughuli

Viongozi wa shughuli za Msingi wanawahudumia watoto pale wanapopanga huduma na shughuli kuanzia Januari ya mwaka watoto hao wanapofikisha umri wa miaka 8 (ona 12.2.1.3). Huduma na shughuli vinafokasi kwenye kazi ya wokovu na kuinuliwa. Ni za kuleta burudani na za kuvutia.

12.5

Miongozo ya Ziada na Sera

12.5.1

Kuwalinda Watoto

Wakati watu wazima wanapochangamana na watoto katika mipangilo ya Kanisa, angalau watu wazima wawili wanaoweza kuwajibika wanapaswa kuwepo.

Watu wazima wote wanaofanya kazi na watoto lazima wakamilishe mafunzo ya ulinzi wa watoto na vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org).