EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari
Somo la 17: Katika Jumuiya


“Somo la 17: Katika Jumuiya,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Somo la 17,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi

vijana wakiwa wamekee nje

Lesson 17

In the Community

Shabaha: Nitajfunza kuelezea matukio ya siku zijazo na kufanya mialiko.

Personal Study

Jiandae kwa ajili ya mazungumzo yako na kikundi kwa kukamilisha shughuli A hadi E.

ikoni a
Study the Principle of Learning: Press Forward

Songa Mbele

With God’s help, I can press forward even when I face obstacles.

Kwa msaada wa Mungu, ninaweza kusonga mbele hata wakati ambapo ninakabiliana na vikwazo.

Tunasoma kuhusu mwanamke aliyeitwa Ruthu katika maandiko ambaye alikuwa na changamoto nyingi. Mume wake alifariki, na yeye hakuwa na watoto. Mama mkwe wake, Naomi, alipanga kurudi katika nchi yake na alimwambia Ruthu abakie, lakini Ruthu alijibu,

“Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa; watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu, wako, atakuwa Mungu wangu. … [Naomi] aliona kuwa [Ruthu] ameshikilia nia yake ya kufuatana naye” (Ruthu 1:16, 18).

Ruthu alikuwa amedhamiria na alikuwa mwaminifu. Ruthu alichagua kukaa na Naomi na kuishi katika mahali pa ugeni, mbali na familia yake na utamaduni wake. Alichagua kuwa mwaminifu kwa dini yake mpya. Mambo yalikuwa magumu sana kwa Ruthu na Naomi. Walikuwa masikini sana na walisumbuka kupata chakula cha kutosha. Ruthu aliendelea kusonga mbele na kumwamini Mungu, na alimtunza Naomi. Mungu aliona mapambano yake na alibariki juhudi zake. Baada ya muda, Ruthu aliolewa tena, alipata watoto, na alikuwa na chakula cha kutosha kwa ajili ya familia yake. Unaweza kumwamini Mungu kama Ruthu Unaweza kusonga mbele kwa imani hata wakati mambo ni magumu.

Ruthu na Naomi

Ponder

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kujihusisha na uzoefu wa Ruthu?

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kusonga mbele kwa tumaini katika Mungu?

  • Ni kwa jinsi gani hii inatumika kwa uzoefu wako wa kujifunza Kiingereza?

ikoni b
Memorize Vocabulary

Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo.

What will you do?

Utafanya nini?

I will …

Nita …

Verbs

attend a party

Nitahudhuria tafrija

do a service project

nitafanya mradi wa huduma

go to a concert

nitakwenda kwenye burudani ya muziki

play soccer

nitacheza soka

run a race

nitakimbia mbio

watch a movie

nitaangalia sinema

Nouns

celebration

sherehe

food

chakula

game

mchezo

parade

gwaride

party

tafrija

church

kanisa

park

bustani

stadium

Uwanja wa michezo

Time

at 8:00

saa 2:00

in a few days

katika sikuchache

in two days

katika siku mbili

next week

wikiijayo

on Friday

siku ya Ijumaa

ikoni c
Practice Pattern 1

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali.

Q: What will you do (time)?A: I will (verb) (time).

Questions

swali la mpangilio wa 1 wewe utafanya nini muda

Answers

jibu la mpangilio wa 1 mimi nita kitenzi muda

Examples

mbio za nyika

Q: What will you do next week?A: I will run a race next week.

burudani ya muziki usiku

Q: What will she do at 8:00 p.m.?A: She will go to a concert at 8:00 p.m.

Mpiga ngoma katika bendi ya gwaride

Q: What will they do in a few days?A: They will go to a parade.

ikoni d
Practice Pattern 2

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kuelewa kanuni katika mipangilio. Fikiria jinsi Kiingereza kinavyofanana na au ni tofauti na lugha yako.

Q: When is the (noun)?A: It will be at (time). There will be (noun).

Questions

swali la mpangilio wa 2 lini ni nomino

Answers

jibu la mpangilio wa 2 itakuwa muda

Examples

Familia kwenye tafrija ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya bibi mkongwe

Q: When is the party?A: It will be at 8:00 p.m.

Q: Where is the party?A: It will be at the park.

Q: What will happen at the party?A: There will be games and good food.

ikoni e
Use the Patterns

Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.

Additional Activities

Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources au katika Kitabu Kazi cha EnglishConnect 2.

Act in Faith to Practice English Daily

Endelea kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi.” Rejelea lengo lako la kujifunza na utathmini juhudi zako.

Conversation Group

Discuss the Principle of Learning: Press Forward

(20–30 minutes)

Ruthu na Naomi

ikoni ya 1
Activity 1: Practice the Patterns

(10–15 minutes)

Rejelea orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.

Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:

  • Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.

  • Fanya mazoezi ya kujibu maswali.

  • Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.

Rudia mpangilio wa 2.

ikoni ya 2
Activity 2: Create Your Own Sentences

(10–15 minutes)

Fanya Igizo. Mwenza A anauliza maswali kuhusu tukio. Mwenza B anajibu maswali na anamwalika Mwenza A kwenye tukio. Badilishaneni nafasi.

New Vocabulary

Do you want to come to the concert with me?

Je, unataka kuja kwenye burudani ya muziki pamoja nami?

How much is it?

Ni bei gani kwani?

Example

Event: Concert

Tukio: Burudani ya Muziki

Time: 8:00 p.m.

Muda: 2:00 usiku

Day: Thursday

Siku: Alhamisi

Date: September 14

Tarehe: 14 Septemba

Cost: $15

Kiingilio: Dola za Kimarekani 15

Location: South Stadium

Mahali: Uwanja wa Michezo wa Kusini

Details: A band will play music. There will be a special performance.

Maelezo: Bendi itapiga Muziki. Kutakuwepo na onyesho maalumu.

usiku wa burudani ya muziki
  • A: What will you do on Thursday?

  • B: I will go to a concert.

  • A: Where is the concert?

  • B: It will be at South Stadium.

  • A: When is the concert?

  • B: It’s at 8:00 p.m.

  • A: What will happen at the concert?

  • B: There will be a special performance. Do you want to come to the concert with me?

  • A: Yes! How much is it?

  • B: It’s 15 dollars.

Chart 1

Event: Soccer Game

Tukio: Mchezo wa Soka

Time: 7:00 p.m.

Muda: 1:00 usiku

Day: Saturday

Siku: Jumamosi

Date: June 21

Tarehe: 21 Juni

Cost: $22

Kiingilio: Dola za Kimarekani 22

Location: City Stadium

Mahali: Uwanja wa Michezo wa Jiji

Details: Paint your face. There will be prizes for the best face paint. You can buy food and drinks.

Maelezo: Paka rangi uso wako. Kutakuwa na zawadi kwa uso uliopakwa rangi vizuri zaidi. Unaweza kununua chakula na vinywaji.

Chart 2

Event: Charity Lunch

Tukio: Chakula cha mchana cha Hisani

Time: 12:00 p.m.

Muda: 6:00 mchana

Day: Friday

Siku: Ijumaa

Date: May 4

Tarehe: Mei 4

Cost: $50

Kiingilio: Dola za Kimarekani 50

Location: City Hall

Mahali: Ukumbi wa Jiji

Details: There will be a fundraiser. The mayor will speak. There will be lunch.

Maelezo: Kutakuwa na Mchangisha Pesa. Meya atazungumza. Kutakuwa na chakula cha mchana.

Chart 3

Event: School Picnic

Tukio: Pikniki ya Shule

Time: 6:00 p.m.

Muda: 12:00 jioni

Day: Monday

Siku: Jumatatu

Date: August 20

Tarehe: 20 Agosti

Cost: Free

Kiingilio: Bure

Location: Lakeview Park

Mahali: Bustani ya Lakeview

Details: There will be games. The children will meet their teachers. There will be food.

Maelezo: Kutakuwa na Michezo. Watoto watakutana na walimu wao. Kutakuwa na chakula.

ikoni ya 3
Activity 3: Create Your Own Conversations

(15–20 minutes)

Uliza na ujibu maswali kuhusu tukio hilo. Tumia tukio kutoka kwenye orodha au tukio linalotokea katika maisha yako Sema mengi kadiri uwezavyo. Peaneni zamu.

Example

mikutano ya kanisa
  • A: What will you do next week?

  • B: I will attend a church event.

  • A: When is the church event?

  • B: It is on Tuesday at 6:30 p.m.

  • A: Where is the church event?

  • B: It is at the church on Meadow Parkway.

  • A: What will happen at the church event?

  • B: There will be a speaker, a piano performance, and food.

Events List

birthday party

tafrija ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa

church event

tukio la kanisa

community service project

mradi wa huduma ya jumuiya

dance party

tafrija ya dansi

festival

tamasha

fundraiser

mchangisha fedha

performance

onyesho

picnic

pikniki

wedding

harusi

Evaluate

(5–10 minutes)

Tathmini maendeleo yako juu ya nia na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Evaluate Your Progress

I can:

  • Ask about future events.

    Uliza kuhusu matukio ya siku za usoni.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Talk about future events.

    Zungumzeni kuhusu matukio ya siku za usoni.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Make invitations.

    Fanya mialiko.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha

Evaluate Your Efforts

Tathmini juhudi zako za:

  1. Kusoma kanuni ya kujifunza.

  2. Kukariri Msamiati.

  3. Kufanyia mazoezi mipangilio.

  4. Fanya mazoezi kila siku.

Weka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.”

Shiriki lengo lako na mwenzako.

Act in Faith to Practice English Daily

“Ninashuhudia kwamba tunapoendela kujitahidi daima kushinda changamoto zetu, Mungu atatubariki . … Yeye atafanya kwa ajili yetu kile ambacho hatuna uwezo wa kukifanya wenyewe” (Ulisses Soares, “Kuchukua Msalaba Wetu,” Liahona, Nov. 2019, 114).