EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari
Somo la 7: Mahitaji


“Somo la 7: Mahitaji,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Somo la 7,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi

watu wazee wakitabasamu

Lesson 7

Needs

Shabaha: Nitajifunza kuuliza na kujibu maombi ya msaada.

Personal Study

Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.

ikoni a
Study the Principle of Learning: Exercise Faith in Jesus Christ

Tumia imani katika Yesu Kristo.

Jesus Christ can help me do all things when I exercise faith in Him.

Yesu Kristo anaweza kunisaidia kufanya vitu vyote ninapoonyesha imani Kwake.

Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu. Yeye ana uweza wote. Katika maandiko, tunasoma kuhusu mtu ambaye alitumia imani yake katika Yesu Kristo. Mtoto wa mtu huyu alikuwa mgonjwa sana na hakuna mtu angeweza kumsaidia. Baba alimwomba Yesu amponye mtoto wake. Yesu alimwambia.

“Kama unaweza kuamini, kila kitu kinawezekana … Mara babaye yule kijana akapaza sauti akasema akilia, Bwana, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu. … Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama” (Marko 9:23–24, 27).

Kama mtu huyu, unaweza kuanza na tumaini na imani ambayo tayari unayo. Kisha unaweza kukuza imani yako kupitia sala na kujifunza maandiko. Unaweza pia kukuza imani yako unapojaribu kujifunza Kiingereza. Unaweza kuanza na kile unachojua sasa. Fokasi juu ya kile unachoweza kufanya kwa Kiingereza, na ukitumie mara nyingi uwezavyo. Jaribu kusikiliza, kusoma, kusema na kuandika kwa Kiingereza kila siku. Kadiri unavyotenda kwa imani ya kuipa bidii yako yote, Yeye anaweza kusaidia imani yako kukua.

picha ya Yesu Kristo

Ponder

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia imani katika Yesu Kristo?

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kukuza imani yako unapojifunza Kiingereza?

ikoni b
Memorize Vocabulary

Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kutumia maneno kutoka kwenye sehemu ya “Memorize Vocabulary” katika mazoezi yako ya kila siku.

Can you … ?

Je, unaweza … ?

Could you … ?

Je, unaweza … ?

Will you … ?

Je, wewe … ?

Would you … ?

Je, ungeweza … ?

I need you to …

Nahitaji wewe ufanye …

I want you to …

Ninakutaka wewe …

I have to …

Ninahitaji …

I need to …

Ninapaswa …

I want to …

Ninataka …

please

tafadhali

Verbs

carry the groceries

beba hivyo vyakula

clean this room

safisha hiki chumba

cook dinner

pika chakula

do the dishes

osha vyombo vya kulia chakula

do the laundry

fua nguo

drop off food

shusha chakula

fix the computer

Tengeneza hiyo kompyuta

go to the store

nenda dukani

help me

nisaidie mimi

make an appointment

panga miadi

send an email

tuma baruapepe

take Lisa to school

mpeleke Lisa shuleni

ikoni c
Practice Pattern 1

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”

Q: Will you please (verb)?A: No, I can’t (verb) because I need to (verb).

Maombi ya Heshima

swali la mpangilio wa 1 tafadhali kitenzi

Kumbuka: Unapomwomba mtu kufanya kitu, ni heshima kusema “please.”

Answers

jibu la mpangilio wa 1 hapana siwezi kitenzi kwa sababu ninahitaji ku kitenzi

Examples

chumba cha kulala kichafu

Q: Will you please clean this room?A: No, I can’t clean this room because I need to do the laundry.

Q: Would you please do the dishes?A: Yes, I will do the dishes.

Q: Could you please fix the computer?A: Sorry, I can’t fix the computer because I have to go to the store.

Q: Can you please cook dinner?A: Yes, I can.

ikoni d
Practice Pattern 2

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kujifunza zaidi kuhusu mipangilio katika somo hili. Fikiria kutumia vitabu vya sarufi au tovuti.

A: I need you to (verb).B: No, I can’t (verb) because I have to (verb).

Maombi ya Moja kwa Moja

swali la mpangilio wa 2 ninakuhitaji wewe kitenzi

Answers

jibu la mpangilio wa 2 hapana, mimi siwezi kitenzi kwa sababu ninapaswa kitenzi

Examples

wanawake wawili wakiendesha baiskeli moto

A: I need you to take Lisa to school.B: OK, I can take Lisa to school.

A: I want you to cook dinner.B: Sorry, I can’t cook dinner because I have to help Lisa.

A: I need you to make an appointment.B: OK, I will make an appointment.

ikoni e
Use the Patterns

Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.

Additional Activities

Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources au katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 2.

Act in Faith to Practice English Daily

Endelea Kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi.” Pitia tena lengo lako la kujifunza na utathmini juhudi zako.

Conversation Group

Discuss the Principle of Learning: Exercise Faith in Jesus Christ

(20–30 minutes)

picha ya Yesu Kristo

ikoni ya 1
Activity 1: Practice the Patterns

(10–15 minutes)

Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.

Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:

  • Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.

  • Fanya mazoezi ya kujibu maswali.

  • Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.

Rudia mpangilio wa 2.

ikoni ya 2
Activity 2: Create Your Own Sentences

(10–15 minutes)

Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu kila mtu. Chukueni zamu.

Example

mwanamke akifua nguo
  • A: Can you do the laundry?

  • B: No, I can’t do the laundry because I have to go to work.

Image 1

kuchukua maziwa kwenye safu

Image 2

mwanamke akiosha vyombo vya kulia chakula

Image 3

kupiga deni sakafu

Image 4

Wanandoa wanatoa vyakula nje ya gari

Image 5

mama na binti wakipika

ikoni ya 3
Activity 3: Create Your Own Conversations

(15–20 minutes)

Fanya igizo la kila hali. Mwenza A anatoa ombi. Mwenza B anajibu maswali. Sema mengi kadiri uwezavyo. Kuwa mbunifu! Badilishaneni nafasi.

Example

familia inazungumza

Mwenza A ni mzazi. Mwenza B ni mtoto. Mzazi anamuomba mtoto kusafisha chumba chake.

  • A: I need you to clean your room, please.

  • B: OK, I will.

  • A: Thank you.

Situations

  • Mwenza A ni mwanafunzi. Mwenza B ni mwalimu. Mwanafunzi anahitaji msaada na kazi zake za nyumbani.

  • Mwenza A ni katibu. Mwenza B ni bosi. Katibu anahitaji kupanga miadi na bosi wake.

  • Mwenza A ni bosi. Mwenza B ni mfanyakazi wa ofisi. Bosi anahitaji mfanyakazi wa ofisi atume baruapepe muhimu.

  • Mwenza A na mwenza B ni marafiki. Rafiki mmoja anataka rafiki mwingine asaidie kutengeneza gari lake.

  • Mwenza A na mwenza B ni wenza. Mwenza mmoja anataka mwenza mwingine asaidie kupika chakula cha jioni

  • Mwenza A ni mmiliki wa nyumba Mwenza B ni fundi umeme. Mwenye nyumba anahitaji fundi umeme atengeneze taa kadhaa zilizoharibika.

Evaluate

(5–10 minutes)

Tathmini maendeleo yako juu ya nia na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Evaluate Your Progress

I can:

  • Ask for help.

    Omba msaada.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Make requests.

    Fanya maombi.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Understand and respond to requests for help.

    Elewa na jibu maombi ya msaada.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha

Evaluate Your Efforts

Tathmini juhudi zako za:

  1. Kusoma kanuni ya kujifunza.

  2. Kukariri Msamiati.

  3. Kufanyia mazoezi mipangilio.

  4. Kufanya mazoezi kila siku.

Kuweka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.”

Shiriki lengo lako na mwenzako.

Act in Faith to Practice English Daily

“Bwana hahitaji imani kamilifu kwetu ili sisi kufikia uwezo Wake mkamilifu . Lakini Yeye anatutaka sisi tuamini. … Vitu vyote vinawezekana kwa wale wanaoamini” (Russell M. Nelson, “Kristo Amefufuka; Imani Kwake Itahamisha Milima,” Liahona, Mei 2021, 101).