EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari
Somo la 2: Utangulizi


“Somo la 2: Utangulizi,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Somo la 2,” EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi

wanawake wawili wakitabasamu

Lesson 2

Introductions

Shabaha: Nitajifunza kuzungumza kuhusu mtu fulani anatoka wapi na wanataka kufanya nini.

Personal Study

Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.

ikoni a
Study the Principle of Learning: Exercise Faith in Jesus Christ

Tumia imani katika Yesu Kristo.

Jesus Christ can help me do all things as I exercise faith in Him.

Yesu Kristo anaweza kunisaidia kufanya mambo yote ninapoonyesha imani Kwake.

Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu. Mungu alimtuma Yesu, kutufundisha na kutusaidia. Yesu hutufundisha jinsi ya kuishi kweli kwenye kile tunachotaka kuwa kama watoto wa Mungu. Yesu ana uwezo wa kutusaidia kushinda udhaifu wetu na changamoto zetu. Yeye alitufundisha:

“Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.” (Mathayo 17:20).

Unaweza kuhisi kwamba kujifunza Kiingereza ni mlima mkubwa—kazi isiyo wezekana. Lakini unapofanya hata kiasi kidogo cha imani katika Yesu Kristo, imani yako itakuwa. Imani yako inayokua katika Yeye itakusaidia kushinda changamoto zako.

Yesu akizungumza na Mariamu

Ponder

  • Ni baadhi ya changamoto gani unazoweza kukabiliana nazo katika kujifunza Kiingereza?

  • Ni baadhi ya njia gani unazoweza kukuza imani yako katika Yesu Kristo?

ikoni b
Memorize Vocabulary

Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Mungu atakusaidia kukumbuka kile unachojifunza unapofanya vyema kujifunza.

Nouns

Brazil

Brazil

Ghana

Ghana

India

India

Japan

Japani

Mexico

Mexico

South Korea

Korea ya Kusini

Tonga

Tonga

Verbs

cook

pika

play soccer

cheza soka

play violin

cheza violini

run

kimbia

sew

alishona

shop

nunua

sing

imba

watch shows

tazama maonyesho

ikoni c
Practice Pattern 1

Kiingereza kina mipangilio mingi. Kwa mpangilio mmoja na maneno machache ya msamiati, unaweza kuunda idadi kubwa ya sentensi! Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”

Q: Where are you from?A: I am from (noun).

Questions

swali la mpangilio wa 1 unatokea wapi

Answers

jibu la mpangilio wa 1 nina toka nomino

Examples

Q: Where are you from?A: I am from Ghana.

mvulana akitabasamu huku ameshikila mpira

Q: Where is he from?A: He is from Chile.

ikoni d
Practice Pattern 2

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Kama kitu fulani kinachanganya, sali kwa ajili ya msaada na uendelee kufanyia kazi. Mungu atakusaidia unapofanya vyema uwezavyo katika kujifunza.

Q: What do you like to do?A: I like to (verb).

Questions

swali la mpangilio wa 2 unapenda kufanya nini

Answers

jibu la mpangilio wa 2 mimi napenda kitenzi

Examples

mtu akipika

Q: What do you like to do?A: I like to cook.

Q: What does he like to do?A: He likes to watch TV.

mwanamke akishona nguo

Q: What doesn’t she like to do?A: She doesn’t like to sew.

ikoni e
Use the Patterns

Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.

Additional Activities

Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources au katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 2.

Act in Faith to Practice English Daily

Unahitaji kuwa thabiti, mazoezi ya kila siku ya kuzungumza lugha mpya. Kuwa na lengo kunaweza kukusaidia. Lengo lako halihitaji kuwa lenye utata. Kwa kweli, malengo rahisi kwa kawaida yanafaa sana kwa sababu yatakusaidia wewe kukuza desturi ya kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Endelea Kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi.” Pitia tena lengo lako la kujifunza na utathmini juhudi zako.

Conversation Group

Discuss the Principle of Learning: Exercise Faith in Jesus Christ

(20–30 minutes)

Yesu akizungumza na Mariamu

ikoni ya 1
Activity 1: Practice the Patterns

(10–15 minutes)

Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.

Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:

  • Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.

  • Fanya mazoezi ya kujibu maswali.

  • Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.

Rudia mpangilio wa 2.

ikoni ya 2
Activity 2: Create Your Own Sentences

(10–15 minutes)

Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu kila jina la mtu na kule wanakotoka. Zungumza kuhusu kile wanachopenda na wasichopenda kufanya Tumia kiolezo kutoka kwenye somo hili na somo la 1. Kuwa mbunifu! Chukueni zamu.

Example: Raul

  • mvulana akitabasamu huku ameshikilia mpira
  • A: What’s his name?

  • B: He is Raul.

  • A: Where is he from?

  • B: He is from Chile.

  • A: What does he like to do?

  • B: He likes to play soccer.

  • A: What doesn’t he like to do?

  • B: He doesn’t like to shop.

Image 1: Cho and Ji-Hu

mwanaume na mwanamke wakiimba

Image 2: Heather

mwanamke akimimina rojo ya ngano

Image 3: Kota

mvulana akicheza fidla

Image 4: Sasha and Levi

mwanamume na mwanamke wakikimbia

ikoni ya 3
Activity 3: Create Your Own Conversations

(15–20 minutes)

Uliza na ujibu maswali kuhusu vitu unavyovipenda na kusichopenda kufanya. Sema mengi kadiri uwezavyo. Chukueni zamu.

Example

  • A: What do you like to do?

  • B: I like to travel. Do you like to travel?

  • A: No, I don’t like to travel. What don’t you like to do?

  • B: I don’t like to watch sports. Do you like to watch sports?

  • A: Yes, I like to watch sports.

Evaluate

(5–10 minutes)

Tathmini maendeleo yako juu ya shabaha na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Evaluate Your Progress

I can:

  • Ask where others are from.

    Uliza wengine wanatoka wapi.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Say where I and others are from.

    Sema mimi na wengine tumetoka wapi.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Ask others what they like and don’t like to do.

    Uliza wengine wanapenda nini na hawapendi kufanya nini.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Talk about what I and others like and don’t like to do.

    Zungumza kuhusu nini mimi na wengine tunapenda au hatupendi kufanya nini.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha

Evaluate Your Efforts

Tathmini juhudi zako za:

  1. Kusoma kanuni ya kujifunza.

  2. Kariri Msamiati.

  3. Kufanyia mazoezi mipangilio.

  4. Fanya mazoezi kila siku.

Weka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.”

Shiriki lengo lako na mwenzako.

Act in Faith to Practice English Daily

Anza leo ili kuongeza imani yako. Kupitia imani yako, Yesu Kristo ataongeza uwezo wako wa kuhamisha milima katika maisha yako [ona 1 Nefi 7:12] ingawa changamoto zako za kibinafsi zinaweza kuonekana kama Mlima Everest” (Russell M. Nelson, “Kristo Amefufuka; Imani Kwake Itahamisha Milima,” Liahona, Mei 2021, 102–3).