“Kipengele cha 1: Hitimisho—Kujitambulisha Mwenyewe,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Kipengele cha 1: Hitimisho,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Unit 1: Conclusion
Introducing Myself
Kazi nzuri katika masomo ya kipengele hiki! Umejifunza jinsi ya kuanza mazungumzo na kushiriki mambo unayopenda kujua. Katika kipengele hiki, ulijifunza zaidi ya maneno 90 na mipangilio 18 ya sentensi. Kwa maneno haya na mipangilio hii, unaweza kuuliza maswali 200 na kuunda sentensi 3,000. Hii ni ya kupendeza!
Evaluate
Evaluate Your Progress
Chukua muda utafakari na kusherehekea yote ambayo wewe umetimiza.
I can:
-
Introduce myself and others.
Jitambulishe mwenyewe na wengine.
-
Ask about personal information.
Uliza kuhusu habari za kibinafsi.
-
Describe my hobbies and interests.
Elezea mambo nipendayo kwa burudani na nipendayo kujua.
Ili kufuatilia maendeleo yako zaidi, nenda kwenye englishconnect.org/assessments na ukamilishe upimaji wa hiyari kwa ajili ya kitengo hiki.
Evaluate Your Efforts
Pitia tena juhudi zako kwa ajili ya kipengele hiki katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.” Je, unafanya maendeleo kuelekea kwenye madhumuni yako? Unaweza kufanya nini tofauti ili kufikia malengo yako?
Endelea kufanya mazoezi ya Kiingereza kila siku unapojiandaa kwa ajili ya EnglishConnect 2.
Ili kujifunza zaidi kuhusu jinsi EnglishConnect inavyoweza kupanua fursa zako, tembelea englishconnect.org.