“Somo la 1: Somo la Utangulizi,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 1,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 1
Introductory Lesson
Karibu kwenye EnglishConnect! Tumefurahi sana wewe uko hapa. Sisi ni jumuiya ya watu wanaotafuta kupanua fursa zetu kwa kujifunza Kiingereza. Yawezekana kuwa tumetokea asili tofauti, tunaozungumza lugha tofauti, na tuna uwezo wa Kiingereza wa viwango tofauti, lakini pamoja tunaweza kufikia malengo yetu.
EnglishConnect ni tofauti na programu nyingi za kujifunza Kiingereza. EnglishConnect imesanifiwa ili kukusaidia wewe kukuza ujuzi wa Kiingereza katika mazingira ya imani, urafiki na ukuaji. Hiyo humaanisha hautafanya hivyo peke yako. Kila mtu katika kikundi cha EnglishConnect atamsaidia na kumtia moyo kila mmoja. Humaanisha pia kwamba wewe utakuwa ukitumia kanuni za kiroho za kujifunza unaposoma na kujifunza.
Katika somo hili, tutatambulisha mchakato ambao wewe utatumia kwa kila somo katika kujifunza binafsi na katika kikundi chako cha mazungumzo.
Acha tuanze!
Conversation Group
Lengo: Nitajfunza kujitambulisha mwenyewe na kuwatambulisha wengine.
Discuss the Principle of Learning: You Are a Child of God
(10–20 minutes)
Kila somo katika kitabu hiki cha kiada huanza na kanuni ya kujifunza. Hizi ni kanuni za kiroho ambazo zinakusaidia kuboresha kujifunza kwako kupitia kusoma na imani. Katika kila somo, sisi tuta:
-
Soma kanuni ya kujifunza kwa sauti.
-
Jadili maswali.
Wewe Ni Mtoto wa Mungu
Je, ulijua kwamba mojawapo ya mambo muhimu unayoweza kufanya ili kufikia lengo lako ni kufokasi kwenye imani yako kuhusu wewe mwenyewe? Imani yako kuhusu uwezo wako italeta matokeo makubwa juu ya juhudi yako na matokeo. Unaweza kuwa na shaka juu ya uwezo wako kwa sababu ya kushindwa hapo awali. Habari njema ni kwamba unaweza kubadili imani yako! Wakati unapobadili imani yako kuhusu wewe mwenyewe, unaweza kubadili matokeo yako. Nguvu ya kubadili imani yako kuhusu wewe mwenyewe hutokana na kuelewa asili yako ya kweli.
Wewe ni Mtoto wa Mungu. Yeye anakupenda. Kama mtoto Wake, una uwezekano na kusudi la milele. Una uwezo wa kujifunza na kubadilika. Una uwezo wa kukua na kuwa bora. Mungu anataka kukusaidia wewe upate maendeleo. Yeye anataka kuwa na ubia na wewe ili kukusaidia kufikia uwezekano wako. Kuwa na ubia na Mungu katika kujifunza Kiingereza kutakusaidia kumjua Yeye vyema. Yeya pia atakusaidia wewe kujijua vyema.
Unaweza kusali kwa Mungu. Yeye atakusikia. Unaweza kumwomba Yeye akusaidie kujifunza Kiingereza. Unaweza kumshukuru Yeye kwa ajili ya baraka zako. Unaposali, kuwa msikivu kwa mawazo na hisia zako. Unaweza kujua kwamba Mungu yuko, Yeye anakupenda, na Yeye anataka kukusaidia wewe. Unaweza kuchagua kuamini kwamba wewe ni mtoto wa Mungu aliye na uwezekano wa milele, na unaweza kutafuta msaada Wake ili kujifunza Kiingereza.
Ponder
-
Ni jinsi gani kujua wewe ni mtoto wa Mungu kunaipa nguvu imani yako kuhusu wewe mwenyewe?
-
Je, ni kwa jinsi gani kujua wewe ni mtoto wa Mungu kunakusaidia wewe kujifunza Kiingereza?
Activity 1: Practice the Pattern
(10–15 minutes)
Part 1: Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Unapojifunza msamiati, fokasi kwenye maana na matamshi ya kila neno.
|
I/my |
Mimi/yangu |
|
you/your |
wewe/yako |
|
he/his |
yeye/yake |
|
she/her |
yeye/yake |
|
no |
Hapana |
|
yes |
ndiyo |
|
name |
jina |
|
please |
tafadhali |
|
thank you/thanks |
asante |
|
What is … ? |
Ni nini … ? |
|
Nice to meet you. |
Nafurahi kukutana nawe. |
Part 2: Fanyia mazoezi mpangilio wa 1 na mwenzako.
Fanyia mazoezi mipangilio na mwenzako. Lengo lako ni kuuliza na kujibu maswali kwa kujiamini na kuelewa kile kinachosemwa.
Fanya mazoezi kuuliza maswali.
Buni maswali mengi kadiri uwezavyo.
Example 1
What is your name?
Example 2
What’s his name?
Fanya mazoezi ya kujibu maswali
Buni majibu mengi kadiri uwezavyo. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno yako mwenyewe.
Example 1
My name is Rosa.
Example 2
His name is Niko.
Fanya mazoezi ya maongezi ukitumia mipangilio.
Uliza na ujibu maswali ukitumia mipangilio.
Questions
Answers
Example
-
A: Hi! What is your name?
-
B: Hello! My name is .
-
A: Nice to meet you.
-
B: What’s your name?
-
A: My name is .
-
B: Nice to meet you.
-
A: What’s her name?
-
B: Her name is Rosa.
Activity 2: Create Your Own Sentences
(5–10 minutes)
Madhumuni ya shughuli hii ni kwa ajili yako kutumia mipangilio na msamiati kujenga sentensi zako mwenyewe.
Tazama picha. Uliza na kujibu maswali kuhusu jina la kila mtu. Fanyeni zamu.
Example: Talia
-
A: What’s her name?
-
B: Her name is Talia.
Marco
Nat
Mari
Jean
Sam
Activity 3: Create Your Own Conversations
(10–15 minutes)
Dhumuni la shughuli hii ni kuwa na mazungumzo kwa Kiingereza.
Part 1
Kutana na kikundi chako Uliza jina la kila mwanafunzi katika kikundi chako. Kuwa mbunifu. Tumia maneno mengi kadiri unavyojua.
Example
-
A: Hi, what’s your name?
-
B: My name is Mei. What is your name?
-
A: My name is Sione. Nice to meet you.
-
B: Nice to meet you. Goodbye.
-
A: Bye!
Part 2
Tafuta mwenza na mtambulishe mwenza wako kwa kikundi chako.
Example
-
A: Hi, what’s her name?
-
B: Her name is Luna. What is his name?
-
A: His name is Seth.
Evaluate
(5–10 minutes)
Wewe ni mtoto wa Mungu na una uwezekano usio na kikomo wa kujifunza na kukua. Wewe unaweza kujifunza jinsiiya kuwa bora kwa maombi kutathminiutendaji na juhudi zako. Baada ya kila somo, tathmini maendeleo yako katika kutimiza kila nia. Kisha, tathmini juhudi zako kwa kutumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi” na ukichagua njia moja ya kujiboresha kabla ya somo lifuatalo.
Tathmini maendeleo yako juu ya nia na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.
Evaluate Your Progress
I can:
-
Say my name and others’ names.
Sema jina langu na majina ya wengine.
-
Say hello and goodbye.
Sema jambo na kwaheri.
-
Understand how EnglishConnect can help me learn English.
Kuelewa jinsi EnglishConnect inavyoweza kunisaidia kujifunza Kingereza.
Evaluate Your Efforts
Tathmini juhudi zako za:
-
Kusoma kanuni ya kujifunza.
-
Kariri msamiati.
-
Fanyia mazoezi mipangilio.
-
Fanya mazoezi kila siku.
Weka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatliaji cha Kujifunza Binafsi.”
Shiriki lengo lako na mwenzako.
Kujiandaa kwa ajili ya Somo Lifuatalo
(5 minutes)
Mungu daima yuko ili kutusaidia sisi. Yeye pia anatarajia sisi tufanye vyema tuwezavyo. Tutanufaika kutokana na kila juhudi ya kujiandaa kwa ajili ya somo. Hapa kuna vitu vitatu vya kufanya kwa ajili ya kila somo kabla ya kuhudhuria kikundi chako cha mazungumzo.
-
Soma kanuni ya kujifunza.
-
Kariri msamiati.
-
Fanyia mazoezi mipangilio.
Unaweza kupata vitu hivi vitatu katika sehemu ya “Kujifunza Binafsi” hapo mwanzoni wa kila somo. Kumbuka kujifunza na kufanya mazoezi kila siku.
Act in Faith to Practice English Daily
Hapo mwisho wa kila somo, kuna sehemu ya “Tenda kwa Imani ili Kufanya Mazoezi ya Kiingereza Kila Siku.” Tumia dakika moja kusoma nukuu kwa sauti pamoja na kikundi chako.
“Kila mmoja wetu anao uwezekano wa kiungu kwa sababu kila mmoja ni mtoto wa Mungu. Kila mmoja ni sawa machoni Pake. Matokeo ya ukweli huu ni muhimu” (Russell M. Nelson, “Acha Mungu Ashinde,” Liahona, Nov. 2020, 94.