“Mifano,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect (2023)
“Mifano,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect
Mifano
Hapa chini ni baadhi ya mifano ya jinsi ya kuunda makundi kukidhi mahitaji ya eneo husika.
Makundi Yanayoongozwa na Wamisionari
Makundi Endelevu
Baraza la kigingi linataka kutoa kikundi cha EnglishConnect ambacho waumini wa kigingi na jumuiya wanaweza kujiunga wakati wowote. Wanatumaini makundi ya EnglishConnect yatatoa fursa za kuhudumu kwa waumini wa Kanisa. Pia wanatumaini makundi haya yatatoa fursa kwa washiriki wa jumuiya kujifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo na kupata uzoefu wa upendo wa waumini wa Kanisa.
Wanachagua jengo ambalo liko karibu zaidi na watu wengi walio na uwezekano wa kuhudhuria. Wanaamua kuwa na makundi yanayokutana kila Jumanne usiku kutoka saa 1.00 hadi saa 2:30. Wanawaita walimu wanne, wawili kwa ajili ya EnglishConnect 1 na wawili kwa ajili ya EnglishConnect 2. Wanamwomba mmoja wa walimu kuwa mratibu wa programu nzima na kumpa mwalimu huyo wito wa mtaalamu wa Ustawi na Kujitegemea kwenye Nyenzo za Kiongozi na Karani. Kwa wito huu, mratibu anaweza kuandikisha makundi katika QuichReg.
Baraza la kigingi kisha linatangaza makundi kwa kugawa vipeperushi kanisani, kuweka katika majukwa ya mitandao ya kijamii na kuwaomba wamisionari kuwaalika watu wanaokutana nao. Mwanzoni, kigingi kinawafanya wanafunzi kujiunga na kundi la mtandaoni la EnglishConnect 3 kwa ajili ya eneo lao wanapokuwa tayari kuvuka darasa la EnglishConnect 2. Baada ya muda kigingi kinapokuwa na washiriki wa kutosha kufanya kikundi cha EnglishConnect 3 kwenye jengo hilo hilo kama vikundi vyao vya EnglishConnect 1 na 2. Wanafanya kazi na mwakilishi wao wa BYU–Pathway Worldwide ili kuwaita wamisionari wa PathwayConnect kusimamia kikundi cha EnglishConnect 3.
Makundi ya Masomo Mawili
Baraza la kata linataka kutoa kwa waumini katika kata na jumuiya fursa ya kujifunza Kiingereza. Limejaribu kuendesha kikundi cha EnglishConnect mwanzoni, lakini washiriki wengi waliona ni vigumui kuhudhuria masomo ya wiki 25. Wanajaribu kutoa makundi ambayo yanafanya masomo mawili tu.
Viongozi wanapanga makundi kukutana siku za Jumanne na Ijumaa usiku kuanzia saa 1.30 hadi saa 3:00 usiku. Wanawaita walimu wanne, wawili kwa ajili ya EnglishConnect 1 na wawili kwa ajili ya EnglishConnect 2. Wanasajili makundi katika QuickReg na kuyatangaza makundi kwa kuweka tangazo nje ya jengo la Kanisa. Pia wanatengeneza vipeperushi ambavyo waumini wanaweza kuwapatia marafiki zao au kushiriki kwenye mitandao ya kijamii.
Mwishoni mwa mwezi, viongozi wanahitimisha makundi katika QuickReg na kufanya mpango wa kufanya masomo mawili katika wakati mfupi ujao.
Makundi ya Vijana
Baraza la kigingi linataka kuwasaidia vijana kufikia fursa za kielimu na ajira baada ya kumaliza programu za ujana na kurudi nyumbani kutoka katika misheni zao. Viongozi pia wana matumaini kwamba kujifunza Kiingereza na EnglishConnect kutamsaidia kijana kujifunza jinsi ya kuingia ubia na Mungu ili kufikia malengo muhimu. Wao wanaamua kuanzisha makundi ya EnglishConnect kwa ajili ya vijana katika kigingi chao.
Vijana wanaishi umbali mrefu miongoni mwao, hivyo viongozi wanaamua kuwa makundi yakutane mtandaoni siku ya Jumanne kuanzia saa 2:00 hadi saa 3:00 usiku. Wanamwita mmisionari aliyerudi kutoka misheni na kijana anayejua baadhi ya Kiingereza ili kukifundisha kikundi. Viongozi wanahakikisha kwamba wanafuata Sera za Kanisa kwa ajili ya kumlinda kijana. Kwa mfano, wanahakikisha kwamba watu wazima wawili waliomaliza mafunzo ya kumlinda kijana wanakuwepo katika kila mkutano wa mtandaoni na kwamba kila kijana amesainisha fomu ya ridhaa ya wazazi.
Viongozi pia wanamweka mwalimu au kikundi cha WhatsApp kinachaangaliwa na kiongozi ili vijana waweze kufanyia mazoezi Kiingereza chao kila siku. Kikundi cha WhatsApp kinasaidia kijana asiyeweza kujiunga na mikutano ya Jumanne.
Viongozi wanafanya kazi na meneja wao wa ustawi na kujitegemea ili kuanzisha kikundi cha vijana cha EnglishConnect 3 katika eneo lao kwa ajili ya wale ambao wanao uwezo wa lugha ya Kiingereza ya zaidi ya darasa la EnglishConnect 2.
Makundi Yanayoongozwa na Wamisionari
Viongozi wa misheni wangependa kutumia EnglishConnect ili kushiriki injili ya Yesu Kristo. Wanajua kwamba makundi ya EnglishConnect yanafanya kazi vyema zaidi yanapoendeshwa na muumini na kusaidiwa na mmisionari. Katika baraza na marais wa vigingi katika misheni, wao wanaamua kwamba misheni itaanzisha makundi ya EnglishConnect na kufanyia kazi ya kuyakabidhi kwa vigingi.
Wamisionari wanaamua juu ya nyakati za kukutana ambazo zitakuwa vyema kwa ratiba zao za kufundisha injili na kukuza ufikiaji wa kiwango cha juu kwa watu katika jumuiya. Wakati wamisionari wanaanza kama walimu wa EnglishConnect, pia wanafanya kazi pamoja na viongozi wa ukuhani ili kuwapata waumini wa eneo husika ili kuchukua nafasi zao, baadhi yao wanaweza kuwa wanafunzi wa zamani wa EnglishConnect 1 na 2. Baada ya muda, wamisionari wanageukia kazi ya kuwa wasaidizi. Wamisionari wanaendelea kusaidia makundi kwa kuhudhuria kila mara, kuwaleta wanafunzi wapya na kuwahimiza wanafunzi kutafuta msaada wa Mungu ili kujifunza Kiingereza.