“Usaidizi,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect (2023)
“Usaidizi,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect
Usaidizi
Unaweza kupata majibu ya maswali yanayoulizwa mara nyingi katika sehemu ya “Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara” Unaweza kupata taarifa ya ziada na usasisho wa hivi karibuni kwenye englishconnect.org. Kama unahitaji usaidizi zaidi, unaweza kuwafikia meneja wa ustawi na kujitegemea wa eneo husika au mtaalamu wa ustawi wa kigingi.
Kutengeneza Mtandao wa Usaidizi
Zingatia kuwafikia vikundi vilivyo jirani katika eneo lako ili kujadili changamoto na mafanikio. Viongozi na walimu wanaofanya kazi na vikundi jirani wanaweza kutengeneza mtandao wa usaidizi kwa ajili ya wao wenyewe na watu wengine. Unaweza kupata vikundi vilivyo jirani kwenye quickreg.englishconnect.org.