“Kiambatisho B: Usaili wa Uhodari wa Kunena kwa ajili ya Kupangwa katika Makundi ya EnglishConnect 1 na 2,” EnglishConnect kwa ajili ya Walimu (2023)
“Kiambatisho B,” EnglishConnect kwa ajili ya Walimu
Kiambatisho B
Usaili wa Uhodari wa Kunena kwa ajili ya Kupangwa katika Makundi ya EnglishConnect
Kwa ajili ya Wale Wanaosimamia Usaili wa Kunena
Mtihani huu ni usaili mfupi ambao unapaswa kuchukua sio zaidi ya dakika tano. Usaili huu wa kunena utasaidia kuamua kama mwanafunzi anapaswa kuwekwa katika EnglishConnect 1 au EnglishConnect 2. Tumia karatasi hii kuendesha usaili huu na pima majibu ya msailiwa.
Ya kuchapishwa “Usaili wa Uhodari wa Kunena”
Kufafanua Matokeo ya Usaili wa Kunena
Kila jibu linapaswa kupimwa kwenye mizani ifuatayo:
-
0 = hawezi kujibu swali kabisa
-
1 = ana uwezo kidogo au hana uwezo wa kujibu, anajibu kwa neno moja moja tu
-
2 = anaweza kujibu kwa virai vilivyokaririwa kwa makosa mengi
-
3 = anatoa majibu yaliyounganika yakiwa na virai ambayo havikukaririwa, japo kunaweza kuwa na makosa
-
4 = anatoa majibu yaliyounganika yakiwa na makosa machache
-
Jumla Alama: 0–7 = EnglishConnect 1
-
Jumla Alama: 8–11 = EnglishConnect 2
-
Jumla Alama: 12+ = EnglishConnect 2 na mwalike kutuma maombi ya EnglishConnect 3
Kama wanafunzi wanapata sana 1, wanapaswa kuwekwa katika EnglishConnect 1. Kama wanafunzi wanapata sana 2 au 3, wanapaswa kuwekwa katika English Connect 2. Kama wanafunzi wanapata sana 3 au 4, wanaweza bado kuhudhuria EnglishConnect 2 kama wanapenda lakini wanaweza pia kualikwa kutuma maombi ya EnglishConnect 3 (ona englishconnect.org/join).
Usaili wa Kunena
Msaidie msailiwa kuhisi faraja ya kutosha kwa kuanzisha mazingira ya urafiki. Msalimie msailiwa na jitambulishe mwenyewe kwa urahisi. Kwa mfano: “Hi. My name is . What’s your name?”
Muulize yeye maswali yaliyoorodheshwa katika jedwali hapo chini.
|
Swali |
Alama (0–4) |
|---|---|
Swali 1. Tell me about yourself. What do you like to do? (Kama mwanafunzi haelewi hili, unaweza kujaribu kuuliza, “What are your hobbies?”) | |
Swali 2. Tell me about your family. Who is in your family? | |
Swali 3. Where are you from? Tell me about your city. | |
Swali 4. What did you do last weekend? (Kuzungumza katika wakati uliopita ni vigumu sana, kwa hiyo uliza swali hili tu kama mwanafunzi amefanya vyema kwa maswali mengine.) | |
Swali Jumla Alama |