Liahona
Maneno ya Ukweli
Machi 2024


“Maneno ya Ukweli,” Liahona, Machi 2024.

Taswira za Imani

Maneno ya Ukweli

Nilikuwa na maswali mengi, lakini mchumba wangu na Kanisa walinisaidia kupata majibu.

Picha
mwanamke na mwanamume katika mavazi ya ubatizo wakiwa wamesimama mbele ya picha ya Mwokozi.

Picha kwa hisani ya mwandishi

Nikikulia katika utamaduni usio wa Kikristo nchini Taiwani, sikulelewa kuwa mtu wa dini. Nilimwamini Mungu, lakini sikujua lolote kuhusu Yesu Kristo. Dini yangu ilikuwa kazi yangu na maisha ya kijamii ambayo yaliendana nayo. Hiyo ilijumuisha kunywa sana na kuvuta sigara. Nilikuwa pia mnywaji mkubwa wa kahawa na chai Hii yote ni sehemu ya shughuli yetu ya kitamaduni.

Nilikuja kulifahamu Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kupitia, mchumba wangu na familia yake. Chase alikuwa Mmarekani. Alilelewa katika Kanisa na alihudumu misheni, lakini hakuwa akihudhuria kikamilifu wakati ule. Mwanawe mkubwa, hata hivyo, alikuwa akijitayarisha kuhudumu misheni, na Chase aliunga mkono uamuzi wake.

Wakati wa mlipuko wa janga la UVIKO‑19, tulihudhuria mkutano wa sakramenti nyumbani kwa wazazi wa Chase, tukiangalia matangazo yatokayo kutoka nyumba ya mikutano ya Kanisa lao. Wakati mazungumzo yalipokwisha, wana wawili wa Chase walibariki na kupitisha mkate na maji.

Nilikuwa na maswali mengi. Mchumba wangu alijibu kila mmoja kwa subira. Yesu alikuwa nani? Nini ilikuwa hisia hii ndani ya moyo wangu kila wakati tulipokutana kwenye mikutano ya Kanisa? Ilikuwa hisia ambayo kamwe sijawahi kuihisi hapo awali. Mkate na maji viliwakilisha nini? Kwa nini machozi yalinitoka wakati nilipopokea sakramenti? Nini ilikuwa amani hii niliyokuwa naihisi?

Usiku mmoja nilipata tovuti katika lugha yangu ambayo ilielezea Yesu ni nani na hiyo ilielezea kuhusu maisha Yake. Siku iliyofuata, nilimwambia mama wa mchumba wangu kwamba nilielewa Yesu Kristo ni nani na kwamba niliamini katika Yeye.

Jumapili moja askofu alikuja nyumbani kwa sababu kijana mkubwa wa Chase alikuwa anaenda kumtawaza ndugu yake mdogo kuwa kuhani. Wakati kijana mkubwa alipoweka mikono yake juu ya kichwa cha ndugu yake, sikuweza kujizuia kulia. Nilihisi mshituko mkubwa ndani ya moyo wangu, sikuweza kuzuia machozi. Baadaye, mchumba wangu alieleza kwamba nilimhisi Roho Mtakatifu na kwamba yeye pia alihisi hivyo.

Niliweza kujua kwamba upendo wa mchumba wangu kwa kanisa lake ulikuwa unamrudia. Kwa namna moja ama nyingine, nilijua kwamba kila kitu nilichokuwa nahisi kilikuwa kimeunganishwa kwa Mungu na kwa kitu kilicho cha kweli. Nilihisi upendo ambao kamwe sikuwahi kuuhisi.

“Nilimlilia Mungu”

Visa yangu ya utalii ilikwisha na ilinibidi kurudi Taiwani. Wakati wa miezi iliyofuata nikiwa peke yangu, nilikosa kile nilichokihisi. Kwa muda, nilijazwa na kukata tamaa na giza. Hisia hizo zilikuwa zinanizidi mno kiasi kwamba nilitaka kusalimu amri. Kwa kweli sikujua jinsi ya kusali, lakini nilimlilia Mungu na nilimwambia kila kitu nilichokuwa nahisi na kufikiri. Hisia ya imani ilikuja—hisia ile ile niliyoipata wakati nilipohudhuruia kanisa letu la nyumbani. Najua alikuwa ni Roho Mtakatifu. Alinituliza.

Baada ya hili, mchumba wangu aliwatuma wamisionari kunifundisha. Niliwaambia tayari nilijua injili ya urejesho ilikuwa ya kweli na kwamba nilijua jinsi ilivyo kumhisi Roho Mtakatifu. Lakini nilikuwa na shaka kwamba itakuwa vigumu kwa mimi kuacha kuvuta sigara na kunywa kahawa na chai.

Nilianza kuhudhuria kanisani, kusoma Kitabu cha Mormoni, na kukutana na akina dada wamisionari mara tatu au nne kwa wiki. Hatimaye, Roho Mtakatifu alinisaidia niche kuvuta sigara na niache kunywa kahawa na chai.

Rafiki yangu wa utotoni alianza kuona mabadiliko ndani yangu wiki baada ya wiki. Nilimwalika kwenye mikutano yangu na wamisionari. Alipokuwa anasikiliza, yeye pia alimhisi Roho Mtakatifu na alipata ushuhuda. Wakati janga la UVIKO‑19 lilipopungua, mchumba wangu, sasa akiwa mwenye kuhudhuria kikamilifu Kanisani, hatimaye aliweza kuja Taiwani. Tulifunga ndoa na alinibatiza mimi. Nilikuwa mtu mpya.

Picha
kikundi cha watu kimesimama mbele ya picha ya Mwokozi

Dada Weiling Chen Canfield (Winnie) pamoja na akina dada wamisionari na waumini wa kata waliomfundisha na kumwonesha urafiki. “Bado tunazungumza kila wiki na kufanya kazi pamoja katika wito wangu mpya wa Kanisa katika Muungano wa Usaidizi.

Rafiki zangu wa muda mrefu na wafanyabiashara washirika wangu, ikijumuisha baadhi ya wafanyakazi wa benki na madalali wa soko la hisa, walisema walikuwa wanaona nilikuwa tofauti na mwenye furaha. Niliwaalika kwenye ubatizo wangu, na walikuja. Baada ya hapo, waliniambia walihisi kitu fulani ambacho kamwe hawajawahi kukihisi kabla ya hapo.

Siogopi kuwaeleza wengine kile ninachojua na kuhisi kuhusu Yesu Kristo—kwamba kile ninachojua ni kweli. Ninajua kwamba ushuhuda wangu unang’ara. Wengine waliowahi kunijua mimi maisha yangu yote wanaona hili. Heshima yao kwenye imani yangu hata imewaachisha kuvuta sigara na kunywa wakati wa mikutano ya kazi na vyakula vya usiku. Hiki ni kitu cha kipekee katika utamaduni wetu wa kazi.

Picha
wanawake wawili wamesimama mbele ya jengo la Kanisa

Dada Canfield pamoja na Jin Hua, marafiki wa muda mrefu walikuwa wamevutiwa na Kanisa kupitia uongofu wa Dada Canfield.

Siogopi kuwaruhusu wengine waone, wasikie, na wahisi ushuhuda wangu. Ninaamini kwamba watu wengi ambao hawajui jinsi ya kumpata Mungu na Yesu Kristo watahisi mambo yale yale niliyoyahisi wakati watakaposikia maneno ya ukweli. Siku zote nitakuwa tayari kushiriki maneno ambayo yalibadili maisha yangu.