Liahona
Ujumbe wa Pasaka kutoka kwa Urais wa Kwanza
Machi 2024


“Ujumbe wa Pasaka kutoka kwa Urais wa Kwanza” Liahona, Machi 2024.

Ujumbe wa Pasaka kutoka kwa Urais wa Kwanza

Picha
Yesu Kristo akitazama juu mbinguni akiwa ameinua mikono Yake juu

Kwa Sababu hii Nimekuja, na Yongsung Kim kwa heshima ya Havenlight

Msimu huu wa Pasaka, tunawaalikeni kutafakari juu ya dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi na Ufufuko mtukufu, ambao unatubariki sisi sote.

Kupitia Mkombozi wetu, Yesu kristo, tunapokea ujumbe huu wa tumaini: “Ulimwenguni mnayo dhiki: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu” (Yohana 16:33). Mwokozi anaahidi kwamba tunaposhika amri na ibada Zake, tutakuwa na “amani katika ulimwengu huu, na uzima wa milele katika ulimwengu ujao” (Mafundisho na Maagano 59:23).

Tunashuhudia kwamba Yesu Kristo yu hai! “Amefufuka” (Mathayo 28:6). Kwa sababu Yake, sisi tunaweza kuongozwa na kuimarishwa tunapobeba mizigo tunayokabiliana nayo katika maisha ya hapa duniani. Kupitia imani yetu katika dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi, vifungo vya dhambi haviwezi kutuzuia na majaribu ambayo tunayapitia katika maisha haya hayatakuwa na nguvu ya kudumu juu yetu. “Uchungu wa kifo umemezwa katika Kristo” (Mosia 16:8).

Picha
saini za washiriki wa Uraisi wa Kwanza

Urais wa Kwanza