“Auckland, New Zealand,” Liahona,, Jan. 2023.
Kanisa Liko Hapa
Auckland, New Zealand
Aukland ni mji wenye eneo lenye watu wengi mno nchini. Mwongofu wa kwanza wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho nchini New Zealand alibatizwa mnamo mwaka 1854. Leo, Kanisa katika nchi ya New Zealand lina:
-
Waumini 116,900 (kwa makadirio)
-
Vigingi 30, kata na matawi 229, misheni 3
-
Hekalu 1 linakarabatiwa huko Hamilton, 1 linajengwa huko Auckland
Mambo yote Yanashuhudia
Fabian na Adrienne Kehoe na binti yao wanafurahia maisha kwenye shamba katika bonde la Maromaku. “Tuna shukrani kwa neema ya nchi hii,” Adrienne anasema. “Na mambo haya yote yanashuhudia juu ya muumbaji mwenye upendo.”
Zaidi kuhusu Kanisa New Zealand
-
Ukweli, takwimu, na historia ya Kanisa ndani ya New Zealand.
-
Rais Russell M. Nelson na Mzee Gerrit W. Gong wanatembelea New Zealand.
-
Vijana wanne wa New Zealand wanashiriki shuhuda zao katika video ya dhima ya vijana.
-
Hadithi za imani miongoni mwa waumini wa mwanzo wa Kanisa huko New Zealand.
-
Shahidi anaeleza hadithi ya “huduma ya wamisionari” huko New Zealand.
Mama na binti huko New Zealand wanashiriki muda wa upendo pamoja.
Baba na mwana wanajiunga na familia yao kwa ajili ya usiku wa wiki ya kujifunza Njoo, Unifuate.
Hekalu la Hamilton New Zealand, kwa sasa likiwa kwenye ukarabati, liliwekwa wakfu mwaka 1958. Hekalu lingine linajengwa huko Auckland.
Watoto huko New Zealand, kama vile watoto ulimwenguni kote, wanafurahia kusoma gazeti la Rafiki.
Mama na baba wanawafundisha watoto wao jinsi ya kuwalisha kondoo. Leo huko New Zealand, kuna karibia kondoo watano kwa kila mtu, kushuka kutoka kilele cha ishirini na mbili kwa kila mmoja mwaka 1982.
Wenye ukuhani wa Haruni wanajifunza injili pamoja wakati wa mkutano wao wa akidi.
Ragbi na ufukwe ni maarufu kote nchini New Zealand.