2012
Mahitaji Maalum na Huduma Zilizotolewa
Septemba 2012


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Septemba 2012

Mahitaji Maalum na Huduma Zilizotolewa

Kwa maombi soma kifaa hiki, na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Picha
Muhuri wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama

Imani • Familia • Usaidizi

“Mahitaji ya wengine yapo daima,” Rais Thomas S. Monson alisema, “na kila mmoja wetu anaweza kufanya kitu ili kumsaidia mtu. Isipokuwa tujiingize katika huduma kwa wengine, kuna madhumuni kidogo kwa maisha yetu wenyewe.”1

Kama waalimu watembelezi kwa uaminifu tunaweza kumjua na kumpenda kila dada tunayemtembelea. Huduma kwa wale tunaowatembelea itatiririka kihalisi kutokana na upendo wetu kwao (ona Yohana 13:34–35).

Tunawezaje kujua mahitaji ya dada zetu ya kiroho na kimwili ili tuweze kutoa huduma wakati inahitajika? Kama waalimu watembelezi, tuna haki ya kupokea maongozi wakati tunapoomba kuhusu wale tunaowatembelea.

Kudumisha uhusiano wa kila mara na dada zetu ni muhimu pia. Matembelezi ya kibinafsi, simu, barua ya kutia moyo, barua pepe, kukaa pamoja na yeye, pongezi za kweli, kushiriki na yeye kanisani, kumsaidia katika wakati wa ugonjwa au mahitaji, na vitendo vya huduma vyovyote hutusaidia kutunza na kuimarishana.2

Waalimu watembelezi wameulizwa kuripoti hali, na mahitaji maalum ya dada, na huduma zilizotolewa kwao. Ripoti kama hizi na huduma yetu kwa dada zetu hutusaidia kuonyesha uanafunzi wetu.3

Kutoka kwa Maandiko

Yohana 10:14–16; 3 Nefi 17:7, 9; Moroni 6:3–4

Kutoka kwa Historia Yetu

Kuhudumia mmoja na mwingine daima kumekuwa kitovu cha ualimu tembelezi. Kupitia huduma iendeleayo tunaleta ukarimu na urafiki ambao ni zaidi ya matembelezi ya kila mwezi. Ni kujali kwetu ndiko kuna maana.

“Hamu yangu ni kuwasihi kina dada zetu kuacha kuwa na hofu kuhusu simu au matembezi za robo mwaka au mila mwezi,” alisema Mary Ellen Smoot, rais mkuu wa 13 wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Alituomba sisi “kushughulika badala ya kulea nafsi ororo.”4

Rais Spencer W. Kimball (1895–1985 alifunza, “Ni muhimu kwamba tuhudumiane katika ufalme.” Hali alitambua kwamba sio huduma zote zinazohitajika kuwa za ujasiri. “Mara nyingi, matendo yetu ya huduma inajumuisha kutumainisha rahisi au kutoa usaidizi wa kazi za kawaida,” alisema, “lakini matokeo matakatifu yanayoweza kutiririka kutoka kwa vitendo vidogo lakini vya kukusudia.5

Muhtasari

  1. Thomas S. Monson, “What Have I Done for Someone Today?” Liahona, Nov. 2009, 85.

  2. Ona Handbook 2: Administering the Church (2010), 9.5.1.

  3. Ona Handbook 2, 9.5.4.

  4. Mary Ellen Smoot, katika Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 117.

  5. Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball (2006), 82.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Je! Mimi natafuta maongozi ya kibinafsi ili kujua jinsi ya kujibu mahitaji ya kiroho na kimwili ya kila dada niliyepangiwa kuwatunza?

  2. Je! Kina dada ninaowatunza waweza kujua vipi kwamba mimi ninawajali wao na familia zao?