2012
Kujua Kile cha Kusema
Septemba 2012


Vijana

Kujua Kile cha Kusema

Kama unahisi kama haujui ya kutosha kuhusu injili, cha kishiriki na wengine, pata faraja katika ahadi hizi kutoka kwa maadiko:

“Pazeni sauti zenu kwa watu hawa; yasemeni mawazo nitakayoyaweka mioyoni mwenu, na ninyi hamtashindwa mbele za watu;

“Kwani mtapewa katika saa ile ile, ndiyo, katika wakati ule ule, kile mtakachosema” (M&M 100:5–6)

“Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” (Yohana 14:26).

Hizi ni ahadi kuu, lakini ili kuzipokea, itabidi tutenda sehemu yetu. Katika ujumbe huu, Rais Eyring alitufunza sisi: “Jitayarishe kushiriki [injili] kwa kujaza akili yako kila siku na kweli za injili.” Unaweza kufanya nini ili kujaza akili yako na kweli za injili?