2012
Kushiriki Injili Moyo Hadi Moyo
Septemba 2012


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Septemba 2012

Kushiriki Injili Moyo Hadi Moyo

Picha
Na Rais Henry B. Eyring

Mungu atawaweka watu walio tayari katika njia ya watumishi Wake walio tayari ambao wanataka kushiriki injili. Wewe umeshapata hayo kutokea katika maisha yako mwenyewe. Mara ngapi yanatokea kwako inategemea na matayarisho ya akili yako na moyo wako.

Nina rafiki ambaye kila siku huomba ili kukutana na mtu ambaye yuko tayari kupokea injili. Yeye hubeba nakala ya Kitabu cha Mormoni. Usiku mmoja kabla ya safari fupi, yeye aliamua asiende na nakala bali aende na kadi ya kepeana. Lakini alipokuwa akijitayarisha kuondoka, alipata msukumo wa kiroho: “Beba Kitabu cha Mormoni” Akaweka kimoja kwenye mkoba wake.

Wakati mwanamke anayemjua alikaa karibu naye safarini, akajiuliza, “Ni huyu?” Alisafiri pamoja naye katika safari ya kurejea. Akafikiria, “Nitaanzisha vipi kushiriki injili?”

Badala yake, huyu mwanamke alimuuliza, “Je! Wewe unalipa fungu la kumi kanisani kwako, ama sivyo?” Na yeye akasema anafanya hivyo. Huyu mwanamke akasema alikuwa anafaa kulipa fungu la kumi kanisani kwake lakini hakufanya hivyo, kisha akauliza, “Unaweza kuniambia chochote kuhusu Kitabu cha Mormoni?”

Yeye akaeleza kwamba kitabu hicho ni maandiko, ushuhuda mwingine wa Yesu Kristo, kilitafsiriwa na Nabii Joseph Smith. Huyu mwanamke alionekana kuwa na hamu, kwa hivyo aliingia mkobani mwake na kusema, “Mimi nilipata msukumo nije na hiki kitabu. Nadhania ni kwa sababu yako.”

Naye akaanza kukisoma. Walipokuwa wakiangana, alisema, “Wewe na mimi tutakuwa na mazungumzo zaidi kuhusu haya.”

Kile rafiki yangu hakujua—lakini Mungu alikuwa anajua—ni kwamba yeye alikuwa anatafuta kanisa. Mungu alijua kuwa alitazama rafikiye na kushangaa kwa nini kanisa lake lilimfanya yeye kuwa na furaha sana. Mungu alijua kuwa yeye atauliza kuhusu Kitabu cha Mormoni na kwamba yeye angekuwa tayari kufunzwa na wamisionari. Yeye alikuwa tayari. Hivyo pia rafiki yangu. Wewe nami pia tunaweza kujitayarisha.

Matayarisho tunayohitaji ni katika akili zetu na mioyo yetu. Huyu mwanamke alikuwa amesikia na kukumbuka maneno kuhusu Kitabu cha Mormoni, Kanisa la Bwana la urejesho, na amri ya kulipa fungu la kumi kwa Mungu. Na yeye alikuwa amehisi mwanzo wa ushahidi wa kweli katika moyo wake.

Bwana amesema Atafunua kweli kwenye akili yetu na mioyo yetu kwa Roho Mtakatifu (ona M&M 8:2). Watu wengi mtakaokutana nao wamepata mwanzo wa haya matayarisho. Wamesikia ama kusoma kuhusu Mungu na neno Lake. Kama mioyo yao ni laini ya kutosha, wamehisi, ingawaje kwa mbali, uthibitisho wa kweli.

Huyu mwanamke alikuwa tayari. Vivyo hivyo rafiki yangu, Mtakatifu wa Siku za Mwisho ambaye alikuwa amejifunza Kitabu cha Mormoni. Alikuwa amehisi ushahidi kwamba ni kweli, na akatambua maelekezo kutoka kwa Roho abebe nakala. Yeye alikuwa tayari katika akili yake na moyo wake.

Mungu anatayarisha watu kupokea ushuhuda wako wa kweli zilizorejeshwa. Anahitaji imani yako na kisha matendo yako ya kushiriki kwa ujasiri kile kimekuwa cha thamani sana kwako na kwa wale unaowapenda.

Jitayarishe kushiriki kwa kujaza akili yako kila siku na kweli za injili. Mnapoweka amri na kuheshimu maagano yenu, mtajazwa na ushuhuda wa Roho na wingi wa upendo wa Mwokozi kwenu na kwa wale mnaokutana nao.

Kama mtatenda upande wenu, mtaongezeka kuwa na uzoefu mzuri wa kukutana na watu ambao wako tayari kusikia ushuhuda wenu wa kweli—zinazotolewa kutoka moyo hadi moyo, wenu hadi wao.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Fikiria kusoma ujumbe huu na familia na ujadili aya ifuatayo hadi ya mwisho, pale Rais Eyring anajadili njia za kuimarisha ushuhuda wa mtu. Jadili na familia umuhimu wa kutoa ushuhuda wakati unashiriki injili. Watoto katika familia wanaweza kupata usaidizi katika nafasi ya kuigiza jinsi ya kutoa ushuhuda kwa marafiki.