Yesu Kristo

Maombi ya Sakramenti

  • Yaliyomo

  • Kubariki Mkate

  • Kubariki Maji

Maombi ya Sakramenti


Maombi ya Sakramenti

  • Kubariki Mkate

    Ee Mungu, Baba wa Milele, tunakuomba katika jina la Mwanao, Yesu Kristo, ubariki na utakase mkate huu kwa roho za wale wote watakaoula, ili waweze kuula kwa ukumbusho wa mwili wa Mwanao, na wakushuhudie, Ee Mungu, Baba wa Milele, kwamba wako radhi kujichukulia juu yao jina la Mwanao, na daima kumkumbuka, na kushika amri zake ambazo amewapa; ili daima Roho wake apate kuwa pamoja nao. Amina.


  • Kubariki Maji

    Ee Mungu, Baba wa Milele, tunakuomba katika jina la Mwanao, Yesu Kristo, ubariki na utakase maji haya kwa roho za wale wote watakaoyanywa, ili waweze kufanya hivi kwa ukumbusho wa damu ya Mwanao, ambayo ilimwagwa kwa ajili yao; kwamba washuhudie kwako, Ee Mungu, Baba wa Milele, kwamba daima wamkumbuke, ili Roho wake apate kuwa pamoja nao. Amina.