Yesu Kristo
Kubariki Mkate


Kubariki Mkate

Ee Mungu, Baba wa Milele,
tunakuomba katika jina la Mwanao, Yesu Kristo,
ubariki na utakase mkate huu
kwa roho za wale wote watakaoula,
ili waweze kuula kwa ukumbusho wa mwili wa Mwanao,
na wakushuhudie, Ee Mungu, Baba wa Milele,
kwamba wako radhi kujichukulia juu yao jina la Mwanao,
na daima kumkumbuka,
na kushika amri zake ambazo amewapa,
ili daima Roho wake apate kuwa pamoja nao.
Amina.