Maandiko
Etheri 5
iliyopita inayofuata

Mlango wa 5

Mashahidi watatu na kazi yenyewe watasimama kama ushuhuda wa ukweli wa Kitabu cha Mormoni.

1 Na sasa mimi, Moroni, nimeandika maneno ambayo niliamriwa, kulingana na uwezo wangu wa kukumbuka; na nimekwambia vitu ambavyo animevifungia; kwa hivyo usiviguse ili uvitafsiri; kwani kitu kile kimekatazwa kwako, isipokuwa baadaye itakuwa hekima kwa Mungu.

2 Na tazama, ungekubaliwa kwamba ungeonyesha mabamba kwa awale ambao watasaidia kwa kuileta mbele hii kazi;

3 Na kwa awatatu wataonyeshwa kwa uwezo wa Mungu; kwa hivyo bwatajua kwa hakika kwamba vitu hivi ni vya ckweli.

4 Na kwa vinywa vya amashahidi watatu vitu hivi vitadhihirishwa; na ushuhuda wa watatu, na kazi hii, ambamo kwake kutaonyeshwa uwezo wa Mungu na pia neno lake, ambalo Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu wanashuhudia—na haya yote yatasimama kama ushuhuda dhidi ya dunia katika siku ya mwisho.

5 Na ikiwa itakuwa kwamba watatubu na akurudi kwa Baba katika jina la Yesu, watapokelewa kwenye ufalme wa Mungu.

6 Na sasa, ikiwa sina mamlaka kwa vitu hivi, hukumuni ninyi; kwani mtajua kwamba ninayo mamlaka mtakaponiona, na tutasimama mbele ya Mungu katika siku ya mwisho. Amina.