Maktaba
Bustanini Tukufu


Bustanini Tukufu

Kwa makini

1Bustanini tukufu,

Nilipata wokovu.

Gethsemane Bwana,

Yesu kuniombea.

Yesu kuniombea.

Chukua wangu moyo;

Nitende mapenzi yako,

Gethsemane Bwana,

Yesu kuniombea.

Yesu kuniombea.

2Mwili walijeruhi,

Ukajitoa Zawadi.

Kwa wote uliteswa,

Yesu ulinifia.

Yesu ulinifia.

Chukua wangu moyo;

Nitende mapenzi yako,

Kwa wote uliteswa,

Yesu ulinifia.

Yesu ulinifia.

3Na niyanywapo maji,

Nanyenyekea mimi.

Mwili uliutoa,

Nitakushuhudia.

Nitakushuhudia.

Chukua wangu moyo;

Nitende mapenzi yako,

Hautateswa tena:

Nitakufuata Bwana.

Nitakufuata Bwana.

Maneno na Muziki na Tammy Simister Robinson

© 2003 Tammy Simister Robinson. Haki zote zimehifadhiwa. Wimbo huu unaweza kunakiliwa kwa ajili ya mahitaji, yasiyo ya kibiashara ya matumizi kanisani ama nyumbani. Notisi hii lazima ijumuishwe katika nakala inayotengenezwa.