Vitabu vya Maelekezo na Miito
23. Kushiriki Injili na Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi


“23. “Kushiriki Injili na Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2013).

“23. “Kushiriki Injili na Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Picha
watu wakiangalia simu

23.

23. Kushiriki Injili na Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi

23.0

Utangulizi

Kuwaalika wote waipokee injili ni sehemu ya kazi ya wokovu na kuinuliwa (ona 1.2 katika kitabu hiki cha maelezo; Mathayo 28:19–20). Inajumuisha:

  • Kushiriki katika kazi ya umisionari na kuhudumu kama wamisionari.

  • Kuwasaidia waumini wa Kanisa wapya na wanaorudi waendelee kusonga kwenye njia ya agano.

23.1

Shiriki Injili

23.1.1

Upendo

Njia mojawapo tunayoonesha upendo wetu kwa Mungu ni kwa kuwapenda na kuwahudumia watoto Wake (ona Mathayo 22:36–39; 25:40). Tunajitahidi kuwapenda na kuwahudumia kama Yesu alivyofanya. Upendo huu unatuhimiza tuwafikie watu wa dini, mbari, na tamaduni zote (ona Matendo 10:34; 2 Nefi 26:33).

23.1.2

Shiriki

Kwa sababu tunampenda Mungu na watoto Wake, ni kawaida kwamba sisi tunataka kushiriki na wengine baraka ambazo Yeye ametupatia (ona Yohana 13:34-35.) na kusaidia kuikusanya Israeli. Tunajitahidi kuwasaidia watu wahisi furaha ambayo sisi tunaihisi (ona Alma 36:24). Tunazungumza kwa uwazi juu ya Mwokozi na ushawishi Wake katika maisha yetu (ona Mafundisho na Maagano 60:2). Tunashiriki mambo haya katika njia za kawaida na za asili kama sehemu ya mchangamano wetu na watu binafsi, mtandaoni na katika michangamano mingine.

23.1.3

Alika

Tunaomba kwa ajili ya mwongozo wa kiungu na maelekezo juu ya jinsi ya kuwaalika wengine:

  • Waje na kuona baraka zinazopatikana kupitia Yesu Kristo, injili Yake, na Kanisa Lake (ona Yohana 1:37–39, 45–46).

  • Waje na watusaidie kuwahudumia watu wenye shida.

  • Waje na wastahili kuwa wa Kanisa la urejesho la Yesu Kristo.

Mara kwa mara, mwaliko kwa kawaida unamaanisha kuijumuisha familia yetu, marafiki, na majirani katika kile ambacho tayari tunakifanya.

23.2

Kuwaimarisha Waumini Wapya

Kila muumuni mpya anahitaji urafiki, fursa ya kuhudumu, na kurutubishwa kiroho. Kama waumini wa Kanisa, tunawapa waumini wapya upendo wetu na msaada wetu (ona Mosia 18:8–10). Tunawasaidia wahisi hisia za kufahamu kuwa wao ni sehemu ya Kanisa. Tunawasaidia waendelee kwenye njia ya agano na kuwa “waongfu zaidi kwa Bwana” (Alma 23:6).

23.3

Kuwaimarisha Waumini Wanaorudi

Baadhi ya waumini huchagua kuacha kushiriki katika Kanisa. “Kwa hawa,” alisema Mwokozi, mtaendelea kuwahudumia; kwani hamjui kama watarudi na kutubu, na kuja kwangu kwa moyo wa lengo moja, na nitawaponya; na ndipo mtakuwa njia ya kuwaletea wokovu.”(3 Nefi 18:32).

Waumini ambao hawashiriki kikamilifu wana uwezekano mkubwa zaidi wa kurudi kama wana mahusiano imara na waumini wa Kanisa. Kama vile waumini wapya, wao pia wanahitaji urafiki, fursa za kuhudumu, na kurutubishwa kiroho.

23.4

Viongozi wa Kigingi

23.4.1

Uraisi wa Kigingi

Rais wa kigingi anashikilia funguo katika kigingi kwa ajili ya kushiriki injili na kuwaimarisha waumini wapya na wanaorudi. Yeye na washauri wake wanatoa mwongozo kwa ajili ya juhudi hizi.

Kwa kawaida kila mwezi, rais wa kigingi hukutana na rais wa misheni kuratibu juhudi kati ya viongozi wa kigingi na kata na wamisionari.

23.4.3

Wajumbe wa Baraza Kuu

Urais wa kigingi unaweza kuteua wajumbe wa baraza kuu kuelekeza na kusaidia urais wa Akidi ya Wazee na viongozi wa kazi ya umisionari katika kata. Mjumbe mmoja au zaidi wa baraza kuu anaweza kuteuliwa kuongoza juhudi hizi. Hata hivyo, wajumbe wa baraza kuu wote wana majukumu haya kwa ajili ya kata na akidi ambazo wamepangiwa.

23.4.4

Urais wa Muungano wa Usaidizi katika Kigingi

Chini ya maelekezo ya rais wa kigingi, urais wa Muungano wa Usaidizi katika kigingi unawafundisha na kuwasaidia urais wa Muungano wa Usaidizi katika kata katika wajibu wao kwa ajili ya kushiriki injili na kuwaimarisha waumini wapya na wanaorudi.

23.5

Viongozi wa Kata

23.5.1

Uaskofu

Uaskofu unaratibu pamoja na urais wa akidi ya wazee na urais wa Muungano wa Usaidizi pale wanapoongoza juhudi za kata katika kushiriki injili na kuwaimarisha waumini wapya na wanaorudi. Viongozi hawa wanashauriana pamoja mara kwa mara.

Uaskofu unahakikisha kwamba juhudi hizi zinajadiliwa na kuratibiwa katika baraza la kata na mikutano ya baraza la vijana katika kata.

Askofu anahojiana na waumini wapya wa umri unaofaa kwa ajili ya kibali cha hekaluni ili kufanya ubatizo na uthibitisho kwa niaba ya wafu (ona 26.4.2). Pia anawasaili akina kaka wa umri unaofaa kupokea Ukuhani wa Haruni. Kwa kawaida anaendesha mahojiano haya ndani ya wiki ya kuthibitishwa kwa muumini.

23.5.2

Urais wa Akidi ya Wazee na Urais wa Muungano wa Usaidizi

Urais wa akidi ya wazee na wa Muungano wa Usaidizi wanaongoza juhudi za siku kwa siku za kata katika kushiriki injili na kuwaimarisha waumini wapya na wanaorudi (ona 8.2.3 na 9.2.3).

Viongozi hawa wana majukumu yafuatayo:

  • Kusaidia kuwatia moyo waumini wawapende watoto wa Mungu, washiriki injili, na wawaalike wengine wapokee baraka za Mwokozi.

  • Kuwapangia kazi akina kaka na akina dada wahudumiaji ya kuwahudumia waumini wapya na wanaorudi 21.2.1).

  • Kuongoza kazi ya kiongozi wa kazi ya umisionari katika kata.

Rais wa akidi ya wazee na rais wa muungano wa Usaidizi kila mmoja anamteua mshiriki mmoja wa urais kusaidia kuongoza juhudi hizi. Washiriki hawa wawili wa urais wanafanya kazi pamoja. Wanahudhuria mikutano ya uratibu ya kila wiki (ona 23.5.7).

23.5.3

Kiongozi wa Kazi ya Umisionari katika kata

Uaskofu unashauriana na rais wa kigingi kuamua ikiwa wamwite kiongozi wa kazi ya umisionari katika kata. Mtu huyu anapaswa kuwa mwenye Ukuhani wa Melkizedeki: Kama kiongozi huyu hajaitwa, mshiriki wa urais wa Akidi ya Wazee anajaza jukumu hili.

Kiongozi wa kazi ya umisionari katika kata anausaidia urais wa akidi ya wazee na urais wa Muungano wa Usaidizi katika wajibu wao wa kazi ya umisionari. Pia ana majukumu yafuatayo:

  • Kuratibu kazi ya washiriki wa kata na viongozi, wamisionari wa kata, na wamisionari wa muda wote.

  • Kuongoza mikutano ya uratibu ya kila wiki (ona 23.5.7).

23.5.4

Wamisionari wa Kata

Wamisionari wa kata huwasaidia waumini wa kata wapate uzoefu wa furaha ya kushiriki injili kama ilivyoekezwa katika 23.1. Wanahudumu chini ya maelekezo ya kiongozi wa kazi ya umisionari katika kata au mshiriki wa urais wa akidi ya wazee ambaye anatimiza jukumu hili.

23.5.5

Baraza la Kata na Baraza la Vijana la Kata

Kushiriki Injili na kuwaimarisha waumini wapya na wanaorudi, kunapaswa kujadiliwa kila mara katika mikutano ya baraza la kata. Askofu anaweza kumwalika kiongozi wa kazi ya umisionari katika kata kuhudhuria mikutano ya baraza la kata.

Fomu kama zinazofuata zinaweza kusaidia katika majadiliano haya:

Katika kujadili mahitaji ya vijana katika kata, baraza la Vijana la Kata linatoa angalizo maalumu kwa waumini wapya na wanaorudi na kwa vijana wanaofundishwa na wamisionari.

23.5.7

Mikutano ya Uratibu

Kila wiki, mikutano mifupi isiyo rasmi inafanyika kuratibu juhudi za kushiriki injili na kuwaimarisha waumini wapya na wanaorudi. Kama kiongozi wa kazi ya umisionari katika kata ameitwa, anaendesha mikutano hii. Ama sivyo, mshiriki wa urais wa akidi ya wazee ndiye anachukua jukumu hili la kuendesha.

Wengine ambao wanaalikwa ni pamoja na:

  • Washiriki walioteuliwa wa urais wa Muungano wa Usaidizi na urais wa Akidi ya Wazee.

  • Wamisionari wa Kata.

  • Msaidizi katika akidi ya makuhani (au walimu au rais wa akidi ya mashemasi ikiwa hakuna makuhani katika kata).

  • Mshiriki wa urais wa darasa la wasichana wakubwa.

  • Wamisionari wa muda wote.