Vitabu vya Maelekezo na Miito
17. Kufundisha Injili


“17. Kufundisha Injili,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“17. Kufundisha Injili,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
mama akimfundisha mwanaye

17.

Kufundisha Injili

Tunafundisha Injili ili kuwasaidia watu waimarishe imani kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

17.1

Kanuni za Kufundisha Kama Kristo

Wanapofundisha injili, wazazi, walimu, na viongozi wanafuata mfano wa Yesu Kristo, ambaye ni Mwalimu Mkuu.

Viongozi wanashiriki na walimu kanuni zifuatazo za Kufundisha Kama Kristo katika makundi yao. Kanuni hizi zimeelezwa kwa kina zaidi katika Kufundisha katika Njia ya Mwokozi.

3:45

17.1.1

Wapende Wale Unaowafundisha

Kila kitu Mwokozi anachofanya ni dhihirisho la upendo Wake (ona 2 Nefi 26:24).

3:20

17.1.2

Fundisha kwa njia ya Roho

Walimu wanatafuta mwongozo wa Roho pale wanapojiandaa na kufundisha, na wanajitahidi kuishi kwa kustahili ushawishi Wake kila siku.

3:47

17.1.3

Fundisha Mafundisho

Wakifuata mfano wa Mwokozi, walimu wanafokasi juu ya kweli za injili zenye kuokoa. Wanafundisha wakitumia maandiko, mafundisho ya manabii wa siku za mwisho, na nyenzo za mitaala iliyoidhinishwa.

3:33

17.1.4

Alika Kujifunza kwa Bidii

Walimu wanawahimiza washiriki wa darasa wawajibike kwa ajili ya kujifunza kwao wenyewe.

17.2

Kujifunza na Kufundishia kuliko na Kiini-Nyumbani

Viongozi wa Kanisa na walimu wanahimiza na kusaidia kujifunza na kufundisha injili ambako kiini chake ni nyumbani.

Viongozi na walimu wanawahimiza waumini kutafuta mwongozo wa kiungu wao wenyewe kuhusu jinsi gani ya kujifunza na kufundisha injili. Nyenzo zao kuu zinapaswa kuwa maandiko na jumbe za mkutano mkuu.

3:35

17.3

Majukumu ya Viongozi

  • Kuonesha mfano kwa kujifunza injili na kufundisha katika njia ya Mwokozi.

  • Kuhakikisha kwamba mafundisho katika makundi yao yanajenga imani na ni sahihi kimafundisho.

  • Kutoa msaada endelevu kwa walimu katika makundi yao.

17.4

Mikutano ya Baraza la Walimu

Katika mikutano ya baraza la walimu, walimu wanashauriana pamoja kuhusu kanuni za kufundisha kama Kristo. Pia wanashauriana kuhusu jinsi ya kuboresha kujifunza injili na kufundisha. Wanatumia Kufundisha katika Njia ya Mwokozi kama nyenzo.

Mikutano ya baraza la walimu inafanyika kila robo mwaka wakati wa darasa la dakika 50 siku ya Jumapili.

6:7