Vitabu vya Maelekezo na Miito
9. Muungano wa Usaidizi


“9. Muungano wa Usaidizi,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“9. Muungano wa Usaidizi “ Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
wanawake wakijifunza maandiko

9.

Muungano wa Usaidizi

9.1

Dhumuni na Muundo

9.1.1

Dhumuni

Nabii Joseph Smith alifundisha kwamba dhumuni la Muungano wa Usaidizi ni kuokoa nafsi na kupunguza mateso.

Kauli mbiu ya Muungano wa Usaidizi ni “Hisani haishindwi kamwe” (1 Wakorintho 13:8).

9.1.2

Ushiriki katika Muungano wa Usaidizi

Msichana anaweza kuanza kuhudhuria Muungano wa Usaidizi anapofikia umri wa miaka 18. Katika umri wa miaka 19 au unapohama kutoka nyumbani, kama vile kuhudhuria chuo kikuu au kuhudumu misheni, anapaswa kushiriki katika Muungano wa Usaidizi.

Wanawake walioolewa chini ya miaka 18 nao pia ni washiriki wa Muungano wa Usaidizi.

9.2

Kushiriki katika Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa

9.2.1

Kuishi Injili ya Yesu Kristo

9.2.1.2

Kujifunza Injili katika Mikutano ya Muungano wa Usaidizi

Mikutano inafanyika katika Jumapili ya pili na ya nne ya mwezi. Inadumu kwa dakika 50. Urais wa Muungano wa Usaidizi unapanga mikutano hii. Mshiriki wa urais anaendesha.

Mikutano ya Muungano wa Usaidizi inafokasi kwenye mada moja au zaidi kutoka katika hotuba za mkutano mkuu wa hivi karibuni.

9.2.1.3

Shughuli

Urais wa Muungano wa Usaidizi unaweza kupanga shughuli. Shuguli nyingi zinafanyika katika siku tofauti na Jumapili au Jumatatu.

9.2.2

Kuwajali Wale Wenye Mahitaji

9.2.2.1

Uhudumiaji

Akina dada wanapokea majukumu ya uhudumiaji kutoka kwa urais wa Muungano wa Usaidizi. Kwa maelezo zaidi, ona sura ya 21.

9.2.2.2

Mahitaji ya Muda Mfupi

Akina dada wahudumiaji wanatafuta kuelewa na kushughulikia mahitaji ya wale wanaowahudumia. Waumini wanaweza kuhitaji msaada wa muda mfupi nyakati za ugonjwa, uzazi, vifo, upotevu wa kazi, na hali zingine.

Wanapohitajika, akina dada wahudumiaji wanaomba msaada kwa urais wa muungano wa Usaidizi.

9.2.2.3

Mahitaji ya Muda Mrefu na Kujitegemea

Kama ilivyoratibiwa na askofu, urais wa akidi ya wazee na urais wa Muungano wa Usaidizi wanawasaidia waumini kwa mahitaji ya muda mrefu na kujitegemea.

Rais wa Muungano wa Usaidizi, rais wa akidi ya wazee, au kiongozi mwingine anamsaidia mtu au familia kuanzisha Mpango wa Kujitegemea.

9.2.2.4

Wakati Muumini wa Kata Anapofariki

Wakati muumini wa Kata anapofariki, Urais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidiziwanatoa faraja na msaada. Chini ya mwongozo wa askofu, wanaweza kusaidia kwenye mazishi.

Kwa maelezo zaidi, ona 38.5.8.

9.2.3

Kuwaalika Wote Waipokee Injili

Rais wa Muungano wa Usaidizi anampangia mshiriki wa urais kusaidia kuongoza kazi ya umisionari katika kata. Anafanya kazi na mshiriki wa urais wa akidi ya wazee aliyepangwa kuratibu juhudi hizi.(ona 23.5.1).

9.2.4

Kuziunganisha Familia Milele

Rais wa Muungano wa Usaidizi anampangia mshiriki mmoja wa urais kusaidia kuongoza kazi ya hekaluni na historia ya familia katika kata. Anafanya kazi na mshiriki aliyepangiwa wa urais wa akidi ya Wazee kuratibu juhudi hizi.(ona 25.2.2).

9.3

Viongozi wa Muungano wa Usaidizi

9.3.1

Askofu

Askofu kwa kawaida anakutana na rais wa Muungano wa Usaidizi kila mwezi. Wanajadili kazi ya wokovu na kuinuliwa, ikijumuisha huduma ya akina dada wahudumiaji.

9.3.2

Urais wa Muungano wa Usaidizi

9.3.2.1

Kuita Urais wa Muungano wa Usaidizi

Askofu anamwita mwanamke kuhudumu kama rais wa Muungano wa Usaidizi katika kata. Kama kitengo ni kikubwa vya kutosha, anapendekeza kwake mwanamke mmoja au wawili kuhudumu kama washauri wake.

Baadhi ya vitengo vidogo vinaweza visiwe na rais wa wasichana au rais wa msingi. Kwenye vitengo hivi, rais wa Muungano wa Usaidizi anaweza kuwasaidia wazazi kupanga maelekezo kwa ajili ya vijana na watoto.

9.3.2.2

Majukumu

Rais wa Muungano wa Usaidizi ana majukumu yafuatayo. Washauri wake wanamsaidia.

  • Kuhudumu kwenye baraza la kata.

  • Kuongoza juhudi za Muungano wa Usaidizi ili kushiriki katika kazi ya wokovu na kuinuliwa (ona sura ya 1).

  • Kupanga na kusimamia huduma ya akina dada wahudumiaji.

  • Chini ya mwongozo wa askofu, hushauriana na waumini watu wazima wa kata.

  • Kuratibu juhudi za Muungano wa Usaidizi za kuwaimarisha akina dada vijana wakubwa katika kata, wote waseja na walioolewa.

  • Kukutana na kila mshiriki wa Muungano wa Usaidizi binafsi angalau mara moja kwa mwaka.

  • Kusimamia kumbukumbu za Muungano wa Usaidizi, ripoti, na fedha (ona LCR.ChurchofJesusChrist.org).

9.3.2.3

Mkutano wa Urais

Urais wa Muungano wa Usaidizi na katibu hukutana mara kwa mara. Rais huendesha mikutano hii. Ajenda inaweza kujumuisha mambo yafuatayo:

  • Kupanga jinsi gani ya kuwaimarisha akina dada na familia zao.

  • Kuratibu kazi ya umisionari na kazi ya hekaluni na historia ya familia.

  • Kushughulikia majukumu kutoka katika mikutano ya baraza la kata.

  • Kurejelea upya taarifa kutoka katika mahojiano na wahudumiaji.

  • Kuwafikiria akina dada wa kuhudumu katika miito ya Muungano wa Usaidizi na majukumu mengine.

  • Kupanga mikutano na shughuli za Muungano wa Usaidizi

9.3.3

Katibu

Urais wa Muungano wa Usaidizi unaweza kumpendekaza dada kuhudumu kama katibu wa Muungano wa Usaidizi.

9.4

Kuwasaidia Wasichana Wajiandae ili Kushiriki katika Muungano wa Usaidizi

Urais wa Muungano wa Usaidizi unafanya kazi na wasichana, wazazi wao, na viongozi wa wasichana ili kuwasaidia wasichana wajiandae kushiriki katika Muungano wa Usaidizi.

Viongozi pia wanatoa fursa endelevu kwa ajili ya wasichana na akina dada wa Muungano wa Usaidizi kukuza uhusiano. Kuhudumu pamoja kama akina dada wahudumiaji ni njia moja ya thamani ya kuunganika.

9.6

Miongozo ya Ziada na Sera

9.6.2

Uwezo wa Kusoma na Kuandika

Kadiri inavyohitajika urais wa Muungano wa Usaidizi unafanya kazi na askofu, urais wa akidi ya wazee, na baraza la kata kuwasaidia waumini wajifunze kusoma na kuandika.