Vitabu vya Maelekezo na Miito
Uongozi wa Kigingi


“6. Uongozi wa Kigingi,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“6. Uongozi wa Kigingi, “ Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
kiongozi akizungumza na familia

6.

Uongozi wa Kigingi

6.1

Madhumuni ya Kigingi

Isaya alielezea Sayuni ya siku za mwisho kama hema au maskani iliyohifadhiwa kwa vigingi (ona Isaya 33:20; 54:2).

Bwana alianzisha vigingi kwa ajili ya “ukusanyaji wa pamoja” wa watu Wake na “kwa ajili ya ulinzi, na …kimbilio” kutoka ulimwenguni (Mafundisho na Maagano 115:6).

6.2

Urais wa Kigingi

Rais wa kigingi anashikilia funguo za ukuhani ili kuongoza kazi ya Kanisa katika kigingi (ona 3.4.1). Yeye na washauri wake wanaunda urais wa kigingi. Wanawajali waumini wa kigingi kwa upendo, wakiwasaidia wawe wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo.

Rais wa kigingi ana majukumu manne makuu:

  1. Yeye ndiye kuhani mkuu kiongozi katika kigingi.

  2. Anaongoza kazi ya wokovu na kuinuliwa katika kigingi.

  3. Yeye ni mwamuzi wa wote.

  4. Anasimamia rekodi, fedha, na mali za Kanisa

6.3

Tofauti kati ya Mamlaka ya Marais wa Wilaya na Yale ya Marais wa Vigingi

Katika kila wilaya, mshiriki anayeshikilia Ukuhani wa Melkizedeki anaitwa kuwa rais wa wilaya. Anahudumu zaidi kama rais wa kigingi lakini kwa tofauti zifuatazo:

  • Yeye siyo rais wa akidi ya makuhani wakuu. Akidi kama hizo zinaundwa tu katika vigingi.

  • Kwa idhini ya rais wa misheni, rais wa wilaya anaweza kumsaili kaka anayetawazwa kuwa mzee. Rais wa wilaya au mtu yoyote chini ya maelekezo yake anaweza pia (1) kumleta kaka kwa ajili ya kura ya kukubaliwa na (2) kufanya utawazo (ona 18.10.1.3, 18.10.3, na 18.10.4). Hata hivyo, rais wa wilaya hawezi kuwatawaza mapatriaki, makuhani wakuu, au maaskofu.

  • Kwa idhini ya rais wa misheni, rais wa wilaya anaweza kuwasimika maraisi wa matawi (ona 18.11).

  • Yeye hawapumzishi wamisionari.

  • Yeye haendeshi usaili wa kibali cha hekaluni au kusaini vibali vya hekaluni (ona 26.3.1).

  • Haitishi baraza la uumini isipokuwa ameruhusiwa na rais wa misioni.

6.5

Baraza Kuu

Rais wa kigingi anawaita makuhani wakuu 12 kuunda baraza kuu la kigingi (ona Mafundisho na Maagano 102:1; 124:131).

6.5.1

Linawakilisha Urais wa Kigingi

Urais wa kigingi unateua mjumbe wa baraza kuu kwa kila kata katika kigingi.

Urais wa kigingi pia unateua mjumbe wa baraza kuu kwa kila akidi ya wazee kwenye kigingi.

Urais wa kigingi unaweza kuteua wajumbe wa baraza kuu kuwafundisha watu wafuatao kwenye wajibu wao kwa ajili ya kazi ya hekaluni na historia ya familia na kazi ya umisionari:

  • Urais wa Akidi ya Wazee

  • Viongozi wa kazi ya umisionari katika kata

  • Viongozi wa kazi za hekaluni na historia ya familia katika kata

6.7

Vikundi katika Kigingi

Muungano wa Usaidizi, Wasichana, Msingi, Shule ya Jumapili na Wavulana, kila kikundi kinaongozwa na rais. Marais hawa anahudumu chini ya maelekezo ya rais wa kigingi.

Wajibu mkuu wa viongozi hawa ni kusaidia urais wa kigingi na kuelekeza na kusaidia urais wa kikundi hicho katika kata.

6.7.1

Urais wa Muungano wa Usaidizi, Wasichana, Msingi, na Urais wa Shule ya Jumapilli katika Kigingi

Washiriki wa urais huu wanayo majukumu yafuatayo:

  • Kuhudumu kwenye baraza la kigingi (marais pekee).

  • Kuwaelekeza marais wapya wa vikundi walioitwa kwenye kata.

  • Kutoa misaada endelevu na maelekezo. Kuwasiliana na urais wa kikundi katika kata mara kwa mara ili kujua juu ya mahitaji yao, kujadili mahitaji ya waumini wanao wahudumia, na kuwasilisha taarifa kutoka urais wa kigingi.

  • Kuelekeza urais wa kikundi katika kata wakati wa mikutano ya uongozi ya kigingi (ona 29.3.4).

6.7.2

Urais wa Wavulana katika Kigingi

Urais wa Wavulana katika Kigingi una majukumu yafuatayo:

  • Kuhudumu kama nyenzo kwa uaskofu katika majukumu yao kwa ajili ya akina kaka wa Ukuhani wa Haruni.

  • Kuhudumu kwenye kamati ya uongozi ya vijana katika kigingi (ona 29.3.10).

  • Chini ya maelekezo ya urais wa kigingi, unapanga na kuratibu shughuli za Ukuhani wa Haruni na makambi katika kigingi.