“Kipengele cha 4: Hitimisho—Kuelezea Kazi na Chakula,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Kipengele cha 4: Hitimisho,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Unit 4: Conclusion
Describing Jobs and Food
Hongera! Umekamilisha kipengele cha 4. Wewe sasa unaweza kuzungumza kuhusu kazi yako na kuuliza maswali ili kujifunza kuhusu kazi za watu unaokutana nao. Unaweza pia kuzungumza kuhusu chakula na kuelezea maoni yako kuhusu chakula. Huu ni ujuzi wenye thamani. Endelea kujifunza na kufanya kazi kwa bidii. Bwana atakubariki.
Evaluate
Evaluate Your Progress
Chukua muda utafakari na usherehekea yote ambayo wewe umetimiza.
I can:
-
Talk about my job.
Zungumza kuhusu kazi yangu.
-
Describe foods I like and dislike.
Elezea vyakula ninavyopenda na vile nisivyopenda.
-
Explain why I like or dislike foods.
Elezea kwa nini ninapenda au sivipendi vyakula.
-
Order food and take someone’s order.
Agiza chakula na uchukue agizo la mtu.
-
Apply principles of learning by study and by faith.
Tumia kanuni za kujifunza kwa kusoma na kwa imani.
Ili kufuatilia maendeleo yako zaidi, nenda kwenye englishconnect.org/assessments na ukamilishe upimaji wa hiyari kwa ajili ya kipengele hiki.
Evaluate Your Efforts
Pitia tena juhudi zako kwa ajili ya kipengele hiki katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.” Je, unafanya maendeleo kuelekea kwenye madhumuni yako? Unaweza kufanya nini tofauti ili kufikia malengo yako?
Endelea kufanya mazoezi ya Kiingereza kila siku unapojiandaa kwa ajili ya EnglishConnect 2.
Ili kujifunza zaidi kuhusu jinsi EnglishConnect inavyoweza kupanua fursa zako, tembelea englishconnect.org.