“Somo la 4: Mambo Mtu Apendayo,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 4,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 4
Hobbies and Interests
Shabaha: Nitajfunza kuzungumza kuhusu vitu nivipendavyo na vitu nisivyovipenda.
Personal Study
Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: Love and Teach One Another
Pendaneni na Fundishaneni
I can learn from the Spirit as I love, teach, and learn with others.
Ninaweza kujifunza kutoka kwa Roho ninapowapenda, kuwafundisha na kujifunza pamoja na wengine.
Katika EnglishConnect, tunajua kwamba Mungu ni mwalimu wa kweli, na Yeye hufundisha kupitia RohoWake. Roho huleta hisia za furaha, amani na upendo. Roho hutusaidia kuelewa ukweli na anaweza kuongeza uwezo wetu kwa kujifunza. Njia mojawapo ambayo tunamwalika Roho kuwa pamoja nasi ni kwa kupendana, kufundishana na kujifunza pamoja. Nabii Alma kutoka Kitabu cha Mormoni alikuwa na wajibu wa kuwafundisha watu. Aliwagawa watu katika vikundi na kuchagua kiongozi wa kila kikundi. Alma aliwafundisha.
“Mhubiri hakuwa bora zaidi kuliko wale ambao walimsikiliza, wala mwalimu hakuwa bora kuliko mwanafunzi; na hivyo wote walikuwa sawa” (Alma 1:26).
Katika EnglishConnect, tunaamini kwamba walimu na wanafunzi wana umuhimu ulio sawa. Sisi sote ni walimu na wanafunzi. Tunaheshimiana na kusikilizana. Tunafundishana. Tunapendana na kuthaminiana. Tunawapongeza wengine wanapofanikiwa na kuwatia moyo wakati wanapofanya makosa. Pia tunaweza kutafuta njia za kusaidiana na kupanga muda wa kufanya mazoezi pamoja katika siku za wiki. Mungu atatubariki na Roho Wake tunapojifunza kupendana na kufundishana.
Ponder
-
Unaweza kufanya nini ili kuwapenda na kuwasaidia wale ambao wana uwezo tofauti wa Kiingereza?
-
Ni kwa jinsi gani uzoefu wa kujifunza katika EnglishConnect unaweza kuwa tofauti kutokana na uzoefu mwingine uliokuwa nao hapo awali?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Fikiria hali ambapo ungeweza kutumia neno hili katika mazoezi yako ya kila siku.
Verbs
|
bike |
baiskeli |
|
cook |
pika |
|
dance |
dansi |
|
garden |
bustani |
|
go to the beach |
nenda ufukoni |
|
listen to music |
sikiliza muziki |
|
paint |
paka rangi |
|
play sports |
cheza michezo |
|
play the piano |
piga kinanda |
|
read |
soma |
|
run |
kimbia |
|
shop |
nunua |
|
sing |
imba |
|
sleep |
lala |
|
study |
jifunze |
|
swim |
ogelea |
|
travel |
safiri |
|
watch movies |
tazama sinema |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
Q: What do you like to do?A: I like to (verb).
Questions
Answers
Examples
Q: What do you like to do?A: I like to cook.
Q: What does he like to do?A: He likes to dance.
Q: What don’t they like to do?A: They don’t like to shop.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kuelewa sheria katika mipangilio. Fikiria jinsi Kiingereza kinavyofanana na au ni tofauti na lugha yako.
Q: Do you like to (verb)?A: Yes, I like to (verb).
Questions
Answers
Examples
Q: Do you like to travel?A: Yes, I like to travel.
Q: Do you like to shop?A: No, I don’t like to shop.
Q: Does she like to paint?A: Yes, she likes to paint.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Additional Activities
Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources au katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 1.
Act in Faith to Practice English Daily
Endelea Kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi.” Pitia tena lengo lako la kujifunza na utathmini juhudi zako.
Conversation Group
Discuss the Principle of Learning: Love and Teach One Another
(20–30 minutes)
-
Soma kanuni ya kujifunza ya somo hili kwa sauti.
-
Jadilini maswali.
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali.
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2.
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu kila mtu. Chukueni zamu.
Example: Malia
Likes
Doesn’t Like
-
A: What does Malia like to do?
-
B: She likes to paint.
-
A: Does Malia like to study?
-
B: No, she doesn’t like to study.
Image Group 1: Thomas
Likes
Doesn’t Like
Image Group 2: Raoul
Likes
Doesn’t Like
Image Group 3: Mei
Likes
Doesn’t Like
Image Group 4: Pamela
Likes
Doesn’t Like
Image Group 5: Nadia
Likes
Doesn’t Like
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Uliza na ujibu maswali kuhusu kile unachopenda na kusichopenda kufanya. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
Example
-
A: What do you like to do?
-
B: I like to dance.
-
A: What don’t you like to do?
-
B: I don’t like to read.
-
A: Do you like to listen to music?
-
B: Yes, I like to listen to music.
Evaluate
(5–10 minutes)
Tathmini maendeleo yako juu ya nia na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.
Evaluate Your Progress
I can:
-
Say what I like to do.
Sema kile mimi ninachopenda kufanya.
-
Say what I don’t like to do.
Sema ni kitu gani mimi nisichopenda kufanya.
-
Ask what someone likes to do.
Uliza ni kitu gani mtu anachopenda kufanya.
Evaluate Your Efforts
Tathmini juhudi zako za:
-
Kusoma kanuni ya kujifunza.
-
Kukariri msamiati.
-
Kufanyia mazoezi mipangilio.
-
Fanya mazoezi kila siku.
Weka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.”
Shiriki lengo lako na mwenzako.
Act in Faith to Practice English Daily
“Roho Mtakatifu ni mwalimu wa kweli. Hakuna mwalimu anayeishi, hata kama ana ujuzi na uzoefu kiasi gani, anayeweza kuchukua nafasi Yake katika kushuhudia juu ya ukweli, kushuhudia juu ya Yesu Kristo na kuibadilisha mioyo. Lakini walimu wote wanaweza kuwa vyombo katika kuwasaidia watoto wa Mungu kujifunza kupitia Roho” (“Fundisha kupitia Roho,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi: Kwa Ajili ya Wote Wanaofundisha Nyumbani na Kanisani [2022], 16).