“Utangulizi,” Kitabukazi cha Sauti cha EnglishConnect 2 (2024)
“Utangulizi,” Kitabukazi cha Sauti cha EnglishConnect 2
Utangulizi
Kitabukazi cha EnglishConnect kimesanifiwa ili kutumika kama nyenzo mwenza wa EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi. Dhumuni la kitabukazi hiki ni kukusaidia wewe ukuze ujuzi wako wa lugha ya Kiingereza na uongeze imani yako kupitia shughuli na hadithi. Pia kitakusaidia kufanyia mazoezi misamiati na miundo kwa ajili ya kila somo la EnglishConnect katika maeneo yote manne ya ujuzi: kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika. Kila somo kwenye kitabukazi limegawanyika katika sehemu zifuatazo zilizoorodheshwa hapo chini.
Conversation(s) (Mazungumzo)
Kila somo linaanza na gumzo moja au zaidi. Lengo ni kutambulisha msamiati, mada, na miundo katika somo na kukuza ufahamu wa kusikiliza na kusoma. Kila sehemu ya “Conversation” hufuata mpangilio huu huu:
-
Listen. Sikiliza mazungumzo yote.
-
Listen and repeat. Sikiliza mazungumzo mstari kwa mstari, na rudia kwa sauti kile unachosikia.
-
Write the missing word. Andika maneno yanayokosekana kwenye mazungumzo. Chagua maneno kutoka kwenye kisanduku kilichotolewa.
-
Read aloud. Soma mazungumzo kwa sauti ili ufanye mazoezi ya kuzungumza.
-
Answer the questions (hayajajumuishwa katika kila somo). Sehemu hii huangalia uwezo wako wa kuelewa mazungumzo.
Activities 2–8 (Shughuli ya 2–8)
Idadi ya shughuli hutofautiana kwa kila somo. Shughuli hizi zinajumuisha chati za sarufi; shughuli za kusoma, kuandika, kusikiliza na kuzungumza; na hadithi. Fuata maelekezo ya kila sehemu ya shughuli. Kwa shughuli za kusikiliza, rejea kwenye nambari ya shughuli inayoshabihiana nayo na herufi kwenye sauti iliyorekodiwa—kwa mfano, “Activity 2B”. Kwa ajili ya shughuli za kuzungumza, kumbuka kuzungumza kwa sauti. Unaweza kuangalia majibu yako kwenye “Answer Key” kwenye sehemu ya nyuma ya kitabu hiki.
Practice Partner Instructions (Maelekezo ya Mwenza wa Mazoezi)
Sehemu hii imesanifiwa ili kukusaidia kufanya mazoezi ya kuzungumza Kiingereza ukitumia kile ulichojifunza kwenye somo. Ukiwa unafanya kazi pamoja na mwenza, rejelea “Vocabulary” kwenye sehemu ya nyuma ya kitabu hiki na fanya shughuli katika sehemu hii. Zungumza mara nyingi uwezavyo kwenye kila shughuli. Tumia muda huu kufanya mazoezi ya kuzungumza Kiingereza kwa dhati.
Expansion Activities (Shughuli za Upanuaji)
Hadithi na shughuli hizi zimesanifiwa ili kupanua uwezo wako wa kusoma, kusikiliza, kuzungumza na kuandika kwa Kiingereza na kukusaidia kukuza imani yako katika Yesu Kristo. Kila sehemu ya “Expansion Activities” imeundwa kulingana na hadithi yenye msukumo. Kwa sehemu hii, fanya yafuatayo:
-
Learn the vocabulary. Jifunze maana ya maneno na virai vya msamiati vilivyotolewa kwenye kipengele hiki kabla ya kusoma hadithi. Hii itakusaidia kujiandaa kusoma hadithi na pia kukusaidia kuelewa maneno na virai muhimu kwenye hadithi.
-
Listen. Sikiliza kila sehemu ya hadithi. Unaweza kufanya hivi mara nyingi kadiri unavyohitaji.
-
Read aloud. Soma hadithi kwa sauti ili kufanyia mazoezi kuzungumza na matamshi na kukusaidia kuielewa hadithi. Unaweza kutaka kusikiliza hadithi tena na kusoma huku ukisikiliza.
-
Learn the vocabulary. Msamiati huu ni kwa ajili ya kukusaidia kuelewa maandiko na nukuu ambazo zinaambatana na hadithi. Jifunze maana ya maneno na virai vya msamiati vilivyotolewa kabla ya kujifunza nukuu na maandiko.
-
Read aloud. Ili kufanyia mazoezi kusoma na kutamka, hakikisha unasoma nukuu na maandiko kwa sauti mara kadhaa.
-
Ponder. Maswali haya yameandaliwa ili yakusaidie kufikiri kuhusu kanuni inayofundishwa kwenye hadithi. Tenga muda wa kutafakari. Ungeweza kutaka kuandika majibu yako ya swali au maswali.
-
Write. Kwa sehemu hii utafanya shughuli ya kuandika iliyosanifiwa ili kukusaidia kutumia kanuni iliyo kwenye hadithi.
-
Speak. Kwa sehemu hii utafanya shughuli ya kuzungumza iliyosanifiwa ili kukusaidia kueleza kwa kina juu ya hadithi uliyosoma na kanuni uliyojifunza. Shughuli kama hizo hujumuisha kusimulia upya hadithi, kusimulia uzoefu binafsi unaofanana na hadithi hiyo au kushiriki na wengine umaizi na malengo yanayohusiana na hadithi.
Mambo Muhimu juu ya Maelekezo kwenye Kitabukazi hiki
Jedwali lifuatalo huonyesha maelekezo ambayo kwa kawaida hutumika katika kitabukazi hiki. Ikoni zinaonesha ujuzi ambao utatumika kwenye shughuli. Angalia tafsiri ya maelekezo kama huyaelewi kwa Kiingereza.
Listening
Kusikiliza
|
Listen. |
Sikiliza. |
|
Listen and repeat. |
Sikiliza na rudia. |
|
Listen to the question / example. |
Sikiliza swali / mfano. |
|
Listen and read. |
Sikiliza na soma. |
|
Listen, and then answer the question. |
Sikiliza na kisha ujibu swali. |
|
You may listen more than once. |
Unaweza kusikiliza zaidi ya mara moja. |
*Sauti kwa ajili ya kitabu hiki inaweza kufikiwa katika Maktaba ya Injili au kwenye englishconnect.org/audio.
Speaking
Kuzungumza
|
Repeat. |
Rudia. |
|
Answer aloud. |
Jibu kwa sauti. |
|
Introduce __________. |
Tambulisha __________. |
|
Retell the story. |
Simulia tena hadithi. |
|
Tell the story / scripture to _________. |
Simulia hadithi / andiko kwa __________. |
|
Practice saying the questions aloud. |
Fanyia mazoezi kuuliza maswali kwa sauti. |
|
Say __________. |
Sema __________. |
|
Practice saying __________. |
Fanyia mazoezi kusema __________. |
Reading
Kusoma
|
Read aloud. |
Soma kwa sauti. |
|
Read aloud, then listen. |
Soma kwa sauti, kisha sikiliza. |
|
Read the question. |
Soma swali. |
|
Study the chart. |
Jifunze chati. |
|
Choose the correct response. |
Chagua jibu sahihi. |
|
Choose all that are correct. |
Chagua yote yaliyo sahihi |
|
Answer the questions. |
Jibu maswali. |
|
Number the pictures. |
Zipe picha namba. |
|
Learn the vocabulary. |
Jifunze msamiati. |
|
Read the scriptures aloud. |
Soma maandiko kwa sauti. |
|
Ponder. |
Tafakari. |
Writing
Kuandika
|
Write the missing / correct word. |
Andika neno linalokosekana / lililo sahihi |
|
Rewrite the complete sentence. |
Andika tena sentensi kamili. |
|
Write what you hear. |
Andika kile unachokisikia. |
|
Fill in the blanks / missing words. |
Jaza nafasi zilizo wazi / maneno yanayokosekana. |
|
Write an / the answer (in a complete sentence). |
Andika / jibu (katika sentensi kamili). |
|
Finish the sentence. |
Malizia sentensi. |
|
Be creative. |
Kuwa mbunifu. |
Kujifunza lugha mpya ni mchakato ambao unahitaji muda, uvumilivu na ari. Mungu anaweza kukusaidia kukamilisha malengo yako. Sali kwa ajili ya msaada. Kwa bidii kamilisha shughuli zilizoko katika kitabukazi hiki. Tumia kile unachojifunza. Unapotenda kwa imani kwa kutafuta msaada wa Mungu na kufanya kwa kadiri uwezavyo, uwezo wako wa kuzungumza, kusikiliza, kusoma na kuandika Kiingereza utaboreka.
Kila la heri katika safari yako ya kujifunza Kiingereza!