2023
Akina Kaka na Akina Dada katika Kristo
Novemba 2023


Akina Kaka na Akina Dada katika Kristo

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Injili ya Yesu Kristo inafundisha kwamba sisi sote tu wana na mabinti wa kiroho wa wazazi wa mbinguni ambao hakika wanatupenda na kwamba tuliishi kama familia katika uwepo wa Mungu kabla ya kuzaliwa katika dunia hii. Injili pia inafundisha kwamba sote tuliumbwa katika sura na mfano wa Mungu. Kwa hiyo, sisi ni sawa mbele Zake. …

Kama wafuasi wa Kristo, tunaalikwa kuongeza imani yetu na upendo kwa akina kaka na dada zetu wa kiroho kwa dhati kuifuma mioyo yetu pamoja katika umoja na upendo, bila kujali tofauti zetu, hivyo kuongeza uwezo wetu wa kukuza heshima kwa ajili ya utu wa wana na mabinti wote wa Mungu. …

… Hakuna nafasi kwa ajili ya mawazo au matendo ya kibaguzi katika jumuiya zetu za Watakatifu. …

Na tuiweke mioyo na mawazo yetu sambamba na ufahamu na ushuhuda kwamba sisi sote ni sawa mbele za Mungu, kwamba sisi sote tumepewa endaumenti kamili pamoja na uwezekano na urithi wa milele. Na tufurahie zaidi uhusiano wetu wa kindugu wa kiroho ambao upo kati yetu na kuthamini sifa tofauti na vipaji tofauti sote tulivyonavyo. …

Ninawashuhudia kwamba tunapoendelea kutiririka kwa njia hii wakati wa maisha yetu duniani, siku mpya itaanza ambayo itayaangaza maisha yetu na kumulika fursa za kipekee za kuthamini zaidi, na kubarikiwa kwa ukamilifu zaidi kwa tofauti hizi zilizoumbwa na Mungu miongoni mwa watoto Wake. Hakika tutakuwa vyombo mikononi Mwake ili kuhamasisha heshima na utu miongoni mwa wana na mabinti Zake.