2023
Falme za Utukufu
Novemba 2023


Falme za Utukufu

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Mafundisho yaliyofunuliwa ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho lililorejeshwa yanafundisha kwamba watoto wote wa Mungu—isipokuwa wachache sana kuwafikiria hapa—hatimaye watarithi mojawapo ya falme tatu za utukufu, hata falme ndogo zaidi kati yake “zinapita ufahamu wote.”[Mafundisho na Maagano 76:79]. …

Fundisho lingine la kipekee na desturi ya Kanisa lililorejeshwa ni amri na maagano yaliyofunuliwa ambayo yanawapa watoto wote wa Mungu fursa takatifu ya kufuzu daraja la juu zaidi la utukufu katika ufalme wa selestia. Hatma hiyo ya juu zaidi—kuinuliwa katika ufalme wa selestia—ndio lengo la Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

… Katika utukufu wa “selestia” kuna madaraja matatu, ambapo la juu zaidi ni kuinuliwa katika ufalme wa selestia.

Mpango wa Mungu, uliojengwa juu ya ukweli wa milele, unahitaji kwamba kuinuliwa kuweze kupatikana tu kupitia uaminifu kwa maagano ya ndoa ya milele kati ya mwanamume na mwanamke katika hekalu takatifu, ndoa ambayo hatimaye itapatikana kwa waaminifu wote. …

Hukumu ya Mwisho si tu tathmini ya majumuisho ya matendo mema na mabaya—yale tuliyofanya. Inazingatia athari ya mwisho ya matendo na mawazo—kile ambacho tumekuwa. Tunastahili kupata uzima wa milele kupitia mchakato wa uongofu. …

Kwa sababu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake, tunapokosea katika maisha haya, tunaweza kutubu na kujiunga tena na njia ya agano ambayo inaongoza kwenye kile ambacho Baba yetu wa Mbinguni anatamani kwa ajili yetu.