2023
Mchukue Roho awe Kiongozi Wako
Oktoba 2023


“Mchukue Roho awe Kiongozi Wako,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Okt 2023.

Ujumbe wa Kila Mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana , Oktoba 2023

Mchukue Roho awe Kiongozi Wako

Baba yetu wa Mbinguni alijua kwamba katika maisha ya duniani tutakabiliana na changamoto, shida, na ghasia; Alijua tungepambana na maswali, kukata tamaa, majaribu na udhaifu. Ili kutupatia nguvu ya maisha ya duniani na mwongozo wa kiungu, Yeye alimtoa Roho Mtakatifu.

Kwa jukumu la kiungu, Roho anatuvuvia, anatushuhudia, anatufundisha na kutushawishi tutembee katika nuru ya Bwana. Tunalo jukumu la kiungu la kujifunza kutambua ushawishi Wake kwenye maisha yetu na kuitikia.

Tunawezaje kufanya hivyo?

Kwanza, tunajitahidi kuishi kwa kustahili kuwa na Roho.

Pili, lazima tuwe radhi kumpokea Roho.

Tatu, lazima tumtambue Roho wakati anapokuja.

Nne, lazima tutendee kazi ushawishi wa kwanza.

Na tuchukulie kwa uzito zaidi wito wa Bwana wa “changamkeni, kwa kuwa nitawaongoza” (Mafundisho na Maagano 78:18). Anatuongoza kwa njia ya Roho Mtakatifu. Na tuishi karibu na Roho, tukiitikia kwa haraka juu ya ushawishi wa kwanza, tukijua ushawishi unakuja kutoka kwa Mungu. Ninatoa ushahidi juu ya nguvu ya Roho Mtakatifu ya kutuongoza, kutulinda, na daima kuwa pamoja nasi.