2023
Muundo wa Kanisa la Yesu Kristo
Oktoba 2023


“Muundo wa Kanisa la Yesu Kristo,” Liahona, Okt. 2023.

Ujumbe wa Kila mwezi wa Liahona, Oktoba 2023

Muundo wa Kanisa la Yesu Kristo

Picha
mchoro wa Yesu Kristo

Bwana Yesu Kristo, na Del Parson

Yesu Kristo ndiye kiongozi wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Yeye huwapa mwongozo wa kiungu manabii na mitume ili waliongoze Kanisa leo, kama vile Yeye alivyoliongoza katika kipindi cha Agano Jipya. Wanasaidiwa na viongozi wengine wa Kanisa.

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni Kanisa la Mwokozi. Kanisa “limejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Yesu Kristo mwenyewe akiwa jiwe kuu la pembeni” (Waefeso 2:20). Hii inamaanishaa kwamba Yeye ndiye sehemu muhimu ya msingi huo. Analiongoza Kanisa kupitia manabii na mitume ambao Yeye amewachagua ili wawe viongozi.

Picha
Urais wa Kwanza

Urais wa Kwanza

Raisi wa Kanisa ndiye nabii wa Mungu duniani leo. Yeye ni Mtume mkubwa zaidi na mtu pekee duniani anayepokea ufunuo ili kuliongoza Kanisa lote. Bwana humpa mwongozo wa kiungu ili ajue ni mitume gani wawili awaite kuhudumu kama washauri wake. Hawa wanaunda Urais wa Kwanza. Wote watatu ni manabii, waonaji na wafunuzi.

Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

Washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili nao pia ni manabii, waonaji na wafunuzi. Wao huitwa kuwa mashahidi maalumu wa Yesu Kristo. Wanasafiri kote ulimwenguni ili kufundisha na kushuhudia kuhusu Yeye. (Ona Mafundisho na Maagano 107:23, 33.)

Akidi za Sabini

Washiriki wa Sabini nao pia huitwa kuwa mashahidi wa Yesu Kristo (ona Mafundisho na Maagano 107:25). Wanawasaidia wale Akidi ya Kumi na Wawili kufundisha injili na kulijenga Kanisa ulimwenguni kote.

Picha
viongozi wakishauriana pamoja

Picha na Machiko Horii

Viongozi Wenyeji

Urais wako wa kigingi au wilaya, uaskofu au urais wa tawi, na urais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi nao pia wameitwa na Mungu. Wanaweza kukusaidia wewe ujifunze na uishi injili. Unaweza kujifunza kuhusu baadhi ya miito hii katika makala ya Misingi ya Injili ya Machi 2022, “Kuhudumu katika Miito ya Kanisa.”