2022
Acha Tutembelee Hekalu
Machi 2022


“Acha Tutembelee Hekalu,” Liahona, Machi./Aprili 2022.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho: Wanawake wa Imani

Acha Tutembelee Hekalu

Wakati nilipoomba kujua ni jinsi gani ninaweza kumsaidia mama mkwe wangu, nilifikiria juu ya hekalu.

Picha
Hekalu la Bogotá Colombia

Picha ya Hekalu la Bogota Colombia na Ivan Ortiz Ponce

Wakati wa janga la ulimwengu la UVIKO-19, Hekalu la Bogotá Colombia lilifungwa. Kwa sababu sikuweza kuhudhuria tena, wakati mwingine niliweza kiakili kutembea kuzunguka hekalu, nikikumbuka huduma ambayo niliifanya huko kama mfanyakazi wa hekaluni.

Mama mkwe wangu aliumwa sana muda mfupi baada ya karantini ya UVIKO-19 kuanza nchini Kolombia. Nilipoomba kujua jinsi ambavyo ningeweza kumsaidia, nilifikiria juu ya Hekalu.

Nilipokuwa nikifikiria juu ya hekalu, nilihisi kusukumwa na Roho Mtakatifu kumuuliza mama mkwe wangu ikiwa angependa kutembelea kiakili “mojawapo ya maeneo mazuri zaidi duniani” pamoja nami.

Kwa sauti ya unyonge, alijibu, “Ndio.”

Tulivuta taswira kuanzia nyumbani kwake huko Medellín, kusafiri kwenda nyumbani kwangu Bogotá, na kisha kufika kwenye hekalu. Tulivuta taswira ya kuingia na kuhudumu hekaluni. Tulivuta taswira ya kukaa pamoja kwenye chumba cha selestia, tukitoa sala ya shukrani kwa Bwana.

Baadaye, tulimsihi Baba wa Mbinguni kwamba mama mkwe wangu, kulingana na mapenzi Yake, apate kurejea kwenye afya yake na mwishowe aruhusiwe kurudi kimwili hekaluni. Lilikuwa ni tukio maalum, lenye utakatifu ambalo lilimtia nguvu na kumtia moyo.

Moja ya hadithi kuhusu Mwokozi ambayo inanigusa zaidi ilitokea katika mji wa Kapernaumu. Hadithi hii inatufundisha kwamba Bwana anaweza kuwabariki na kuwaponya wengine kupitia msaada kutoka kwa wanafamilia na marafiki.

Wakati watu wa Kapernaumu walipogundua ya kuwa Yesu yuko nyumbani, wakamletea mtu mwenye kupooza.

“Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo: na wakiisha kuivunja wakaliteremsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.”

Yesu alipoona imani yao, akamwambia yule mtu, “Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.” (Ona Marko 2:1–11.)

Kama vile mtu mwenye kupooza, mama mkwe wangu aliponywa kwa nguvu ya Mwokozi kupitia baraka ya ukuhani na kupitia imani yake na imani ya familia na marafiki.

Katika nyakati hizi zisizo na uhakika, ninajua tunaweza kupokea mwongozo wa kuimarisha na kuwatia moyo wale walio katika shida. Ikiwa tutamgeukia Baba wa Mbinguni na kumkumbuka Yeye na Mwanawe daima, tunaweza kupata amani, tumaini, na uponyaji.