2022
Kutumikia katika Miito ya Kanisa
Machi 2022


“Kutumikia katika Miito ya Kanisa,” Liahona, Machi./Aprili 2022

Misingi ya Injili

Kutumikia katika Miito ya Kanisa

Viongozi wa kanisa huwaomba waumini kutumikia katika majukumu maalum yanayojulikana kama “miito.” Miito huwapa waumini fursa za kuwatumikia wengine na kuja karibu zaidi na Mungu.

Picha
mwanamume kwenye kiti mwendo akifundisha darasa la Kanisa

Picha na David Bowen Newton

Tunapotumikia katika miito yetu, tunasaidia kutimiza kazi ya Mungu. Tunawafundisha wengine kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na kuwasaidia waje karibu zaidi na Wao. Tunapokea pia baraka tunapotumikia kwa uaminifu.

Kupokea Miito

Picha
mvulana amesimama mbele ya mkutano wa Kanisa

Wale wanaotumikia katika Kanisa wameitwa na Mungu. Viongozi wa Kanisa wanaomba ili kupata mwongozo wa kiungu ili kujua ni nani wa kumwita atumikie katika kila wito. Kiongozi kisha anamwomba muumini kutumikia na kumwelezea majukumu ya wito huo. Kwa miito mingi, waumini wanakubaliwa katika mkutano wa Kanisa. Waumini wa kata au tawi hupiga kura ya kuwakubali. Hii inamaanisha kuwa wako tayari kumuunga mkono mtu yule anayepewa wito. Muumini kisha atapewa baraka na kiongozi wa ukuhani. Hii inaitwa kusimikwa. Muumini atapewa mamlaka ya kutenda katika wito huo na baraka zingine za kumsaidia yeye kutumikia.

Maaskofu

Askofu ni kiongozi wa kata. (Katika tawi, rais wa tawi ni sawa na askofu.) Rais wa kigingi humpendekeza mwanamume anayestahili aliye na ukuhani kuitwa kama askofu. Urais wa Kwanza unaidhinisha wito huo. Kisha askofu anakubaliwa na kusimikwa ili kutumikia. Yeye pia hupokea funguo za ukuhani, ambayo inamaanisha anayo mamlaka ya kuiongoza kata hiyo. Kama askofu, anawatumikia na kuwaongoza waumini wote katika kata.

Urais

Akidi za ukuhani na Muungano wa Usaidizi, Wasichana, Msingi, na vikundi vya madarasa ya Shule ya Jumapili huongozwa na marais, kwa kawaida rais na washauri wawili. Urais wa akidi za wazee huitwa na kusimikwa na urais wa kigingi. Uaskofu huwaomba waumini kutumikia katika urais mwingine katika kata na kuwasimika. Viongozi wote huwatumikia waumini katika akidi au vikundi vyao. Wanawatumikia waumini katika mahitaji yao na kuwasaidia wahisi upendo wa Mungu.

Picha
mwanamke akileta chakula kwa mama aliyembeba mtoto

Miito Mingine

Miito mingine ya Kanisa ni pamoja na kufundisha, kusaidia katika muziki, kutunza kumbukumbu, kupanga shughuli za vijana au watoto, na kutumikia kwa njia zingine. Kila wito katika Kanisa ni muhimu na huwapa waumini nafasi ya kuwatumikia wengine na kumtumikia Mungu. Tunapofanya kazi pamoja kutimiza miito yetu, tunawaimarisha wengine na kulisaidia Kanisa kukua.