2021
Je, ni kwa jinsi gani Injili ya urejesho inatubariki sisi?
Januari 2021


Njoo, Unifuate: Mafundisho na Maagano

Je, ni kwa jinsi gani Injili ya urejesho inatubariki sisi?

Mafundisho na Maagano 1

(Desemba 28–Januari 3)

Picha
pdf

Vielelezo na Augusto Zambonato

Katika Mafundisho na Maagano 1, Bwana alitamka, “Amri hizi ni zangu mimi, na zimetolewa kwa watumishi wangu” (Mafundisho na Maagano 1:24). Yeye anaelezea jinsi mkusanyiko huu wa ufunuo, amri, na mafundisho ambayo yangelibariki Kanisa na waumini wake wa mwanzo. Neno lake bado linasimama leo.

Baraka kwa ajili ya waumini

  • Wale wanaotafuta hekima wapate kuelekezwa (ona mstari wa 26)

  • Wale ambao hutenda dhambi “waweze kukemewa, ili waweze kutubu” (mstari wa 27).

  • Walio wanyenyekevu waweze kufanywa imara, na kubarikiwa kutoka juu na kupokea maarifa mara kwa mara (ona mstari wa 28).

Baraka kwa ajili ya Kanisa

  • Imani kuongezeka duniani (ona mstari wa 21)

  • Agano la Bwana lisilo na mwisho litaanzishwa (ona mstari wa 22)

  • “Utimilifu wa injili utatangazwa na watu walio dhaifu na wa kawaida (ona mstari wa 23).

  • Uwezo wa kuweka msingi wa Kanisa na kulitoa kutoka lisikoonekana na gizani (ona mstari wa 30).

Vielelezo na Augusto Zambonato