2017
Wao Walimwona
April 2017


Wao Walimwona

Watu hawa kwa kweli walimwona Mwokozi mfufuka, lakini hata wewe pia unaweza kuwa shahidi wa Kristo kwa njia yako mwenyewe.

Picha
Jesus and Mary in front of the tomb

Amefufuka, na Greg K. Olsen, isinakiliwe

Unafikiria ingekuwaje kumshuhudia Mwokozi mfufuka? Kwani mamia ya watu katika wakati wa Yesu, hawakuhitaji kufikiria—waliuishi. Maandiko yanasimulia kwa kiasi kidogo mifano ipatayo dazani moja iliyoandikwa katika Agano Jipya na mara kadhaa katika Kitabu cha Mormoni wakati Bwana mfufuka alipowatokea watu. Watu hawa binafsi walishuhudia moja ya miujiza mikubwa zaidi katika historia: Yesu Kristo akishinda mauti na kumwezesha kila mmoja wetu kuishi tena. Makubwa yasiosadikika, sawa?

Basi inamaanisha nini haswa kuwa shahidi wa Kristo? Wacha tupeleleze chache ya nyakati hizi katika maandiko na kufikiri jinsi sisi, hata bila ya kumwona kimwili, tunavyoweza pia kuwa mashahidi wa Kristo.

Mariamu Magdalena

Mariamu Magdalena alikuwa shahidi wa kwanza. Asubuhi ya Jumapili baada ya Kusulibiwa Kwake, yeye alikuja kwenye kaburi la mawe na wanawake wachache wengine ili kuupaka mafuta mwili wa Bwana. Wakati Maria alipogundua kaburi liko tupu, alilia. Mtu mmoja alimwendea kutoka nyuma na kumwuliza, “Mama, unalilia nini?” Fikiria mshangao wake wakati alipogundua kwamba alikuwa Yesu, aliyefufuka kutoka kwa wafu. (ona Yohana 20:1–18.)

Wanafunzi wawili wakiwa njiani kwenda Emau

Picha
Christ on the road to Emmaus

Barabara kwenda Emau, na John McNaughton

Cleopa na mwanafunzi mwingine walikuwa wanatembea barabarani kwenda Emau wakati mgeni alipojiunga nao. Wao hawakumtambua mwenza wao mpya, lakini wakati wa mlo wa jioni pamoja, mgeni yule aliumega mkate. Mara macho yao yakafumbuliwa, na wakamtambua kwamba wamekuwa wanasafiri na Mwokozi wakati wote. “Je mioyo yetu haikuwaka ndani yetu?” waliulizana wao kwa wao, wakitafakari uthibitisho ule kwamba walihisi kana kwamba kweli Yeye alikuwa pamoja nao. (Ona Luka 24:13–34.)

Wale Mitume Kumi

Picha
Resurrected Christ with Apostles

Tazameni Mikono na Miguu Yangu, na Harry Anderson

Wanafunzi wawili waliosafiri kwenda Emau na Kristo walirudi Yeruslemu na kuwaambia Mitume kumi kati yao kuhusu tukio lao. Wakati walipokuwa wanazungumza, Mwokozi Mwenyewe aliwatokea, akisema, “Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.” (Ona Luka 24:36–41, 44–49.)

Mtume Tomaso

Picha
Christ with Thomas

Mchoro wa Thomas na Brian Call

Mtume Tomaso hakuwepo wakati Mwokozi alipowatokea mara ya kwanza Mitume, kwa hiyo hakuamini kwamba Kristo amefufuka. Wiki moja baadaye, Kristo tena aliwatokea Mitume. Wakati huu Tomaso alikuwa pale, na kwa sababu alimwona Kristo, aliamini kwamba amefufuka. Mwokozi alimwonya Tomaso dhidi ya kuamini baada ya kuona tu: “Kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki” (Ona Yohana 20:24–29.)

Mitume Kumi na Mmoja Kwenye Bahari ya Tiberia

Picha
Apostles on the Sea of Tiberias

Kristo Mfufuka kwenye Bahari ya Tiberia, na David Lindsley

Siku moja sio muda mrefu baada ya kufufuka, Mitume kadhaa walikwenda kuvua samaki katika bahari ya Tiberia lakini hawakuwa na bahati nzuri. Asubuhi iliyofuata, Bwana aliwatokea na kuwashauri kutupa nyavu upande wa kulia wa boti. Walipofanya hivyo, wavu ulinasa samaki wengi sana kiasi kwamba walishindwa kuuvuta! Baada ya kufurahia pamoja, Mwokozi aliwafundisha kuhusu umuhimu wa kuwahudumia wengine, akisema, “Lisha Kondoo Wangu.” Mitume walitumia muda uliosalia wa maisha yao yote wakifanya hayo tu—kuwafundisha watu kuhusu Kristo—na katika baadhi ya kadhia, walitoa hata uhai wao kwa ajili hii. (Ona Yohana 21:1–22.)

Wanefi katika Amerika

Picha
Christ among the Nephites

Mchungaji Mmoja, na Howard Lyon

Wakati wa kusulubiwa, ardhi katika mabara ya Amerika iliharibiwa kwa tetemeko la nchi, moto, maafa mengine ya asili, na siku tatu za giza ili kuashiria kifo cha Mwokozi. Baadaye, Kristo aliteremka kutoka mbinguni na kuutembelea umati wa watu 2,600 uliokusanyika karibu na hekalu huko Bountiful. Aliwaalika watu kugusa makovu katika mikono Yake na miguuni na ubavuni, alitoa mahubiri, na kuwabariki watoto wa Wanefi mmoja mmoja. Hata watu zaidi walikusanyika siku iliyofuata, na Mwokozi aliwatembelea na aliwafundisha. Wanafunzi hatimaye walianzisha Kanisa la Kristo, na Wanefi walipokea ushuhuda wenye nguvu kama huu kwamba wao na Walamani pia waliongolewa kwa Bwana. (Ona 3 Nefi 11–18; ona pia 3 Nefi 8–10; 4 Nefi 1.)

Mashahidi Wakati ule na Sasa

Kristo pia aliwatokea wengine wengi, pamoja na wanawake kadhaa waliokuja kwenye kaburi la mawe ili kumsaidia Mariamu Magdalena kuupaka mafuta mwili wa Kristo, kundi la zaidi ya wanaume 500, Yakobo na Paulo. (Ona Mathayo 28:9; Matendo ya Mitume 9:4–19; 1 Wakorintho 15:6–7; ona pia 3 Nefi 19; 26:13.)

Yawezekana tusiwe na nafasi ya kumwona Mwokozi kama mashahidi hawa walivyoweza, lakini wewe bado unaweza kuwa shahidi wa Kristo. Unaweza wewe binafsi kumtafuta Kristo, kama Mariamu alivyofanya alipokwenda kaburini, kwa kujifunza zaidi kuhusu Yeye. Au unaweza kutumia imani yako kwake Yeye kwa kutii amri na kufuata ushauri wa manabii. Au ungeweza kutambua baraka za Mwokozi katika maisha yako, kama wanafunzi wale wawili wakitembea kwenda Emau walivyofanya. Majira haya ya Pasaka, fikiria kuhusu nini inamaanisha kuwa shahidi wa Kristo. Watu hawa walikuwa mashahidi halisi ambao kwa kweli walimwona Kristo mfufuka—lakini hiyo sio njia pekee unayoweza kumshuhudia Yeye katika maisha yako.