2017
Jiandae kwa ajili ya Hekalu Kila Siku
April 2017


Jiandae kwa ajili ya Hekalu Kila Siku

Picha
Prepare for the Temple Every Day

Nilipokuwa na umri wa miaka tisa, nilikuwa na mwalimu mzuri sana wa Watoto aitwaye Dada Kohler. Nilikuwa na aibu sana, na alikuwa mpole sana kiasi kwamba nilipenda kuwa pamoja naye. Siku moja alimpa kila mmoja wetu kipande cha karatasi. Sisi wote tuliandika kile tulichotaka kufanya tutakapokuwa wakubwa. Niliandika: “Kwenda chuoni na kufunga ndoa hekaluni.” Nilibandika karatasi yangu juu ya mlango wa kabati. Nyakati za usiku, mwanga kutoka taa za mtaani ulimulika kupitia dirisha langu. Niliangalia juu kwenye kipande changu cha karatasi. Kilinikumbusha mimi kwamba nilitaka kwenda hekaluni.

Wakati huo, palikuwa na mahekalu 12 tu ulimwenguni. Nilitaka kwenda kwenye kila moja ya hayo.

Wakati wo wote mama na baba yangu walipopanga mapumziko, kila mara waliichukua familia yetu hekaluni. Tuliishi Oregon, Marekani. Hekalu la karibu lilikuwa maili 600 (965 km) mbali huko Cardston, Alberta, Canada. Gari letu halikuwa na kiyoyozi. Kaka, dada yangu na mimi tulikaa katika kiti cha nyuma. Tulining’iniza kitambaa nje ya mlango wa gari. Kisha tunakiweka katika shingo zetu ili kujipoza.

Ulikuwa ni msisimko wakati tulipoliona hekalu. Sikujua sana kuhusu nini kilifanyika humo, lakini wazazi wangu kila mara walikuwa na furaha walipotoka nje. Nilijua hekalu lilikuwa muhimu sana. Nilijua ilikuwa ni nyumba ya Bwana. (Katika picha, mimi ni huyo niliyevaa shati jeupe.)

Baada ya kufikisha miaka 12, niliweza kufanya ubatizo hekaluni katika mahekalu kadha wa kadha. Kisha nilipokutana na mume wangu mtarajiwa, niligundua kwamba alilipenda hekalu pia! Tulioana katika Hekalu la Manti Utah.

Unaweza kujianda kwa ajili ya hekalu kila siku. Nenda hekaluni wakati uwezapo. Gusa kuta zake. Wakati mjukuu wangu Jarret alipokuwa na umri wa miaka 11, alifanya kazi ya historia ya familia kila Jumapili pamoja na baba yake. Alipata majina mengi ya mababu. Sasa kwamba ana umri wa miaka 12, anafanya ubatizo humo hekaluni kwa ajili ya mababu hao!

Wakati ukiwa hekaluni, unaweza kutembea mahali Yesu anapotembea. Ni nyumba Yake. Nina tumaini utaomba kila siku kwa Baba wa Mbinguni ili akusaidie kujiandaa kuingia hekaluni na kuhisi upendo Wake.