2017
Kuelewa Baraka Yako ya Kipatriaki
April 2017


Kuelewa Baraka zako za Kipatriaki

Waandishi Wanaishi Illinois, Marekani na New York Marekani.

Kutambua sehemu za baraka yako kutakusaidia kupata mwelekeo wa maisha yako.

Picha
man with a map in a maze

Man in maze © Digital Vision Vections/Getty Images

Maisha yamejaa maji yasiyopimwa: Wapi napaswa kwenda shule? Napaswa kujifunza nini? Je, napaswa kwenda misheni? Nimuoe nani? Kama ungepewa ramani binafsi ili kuongoza maamuzi ya maisha yako, ungeifuata?

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wametupa ramani kama hiyo—baraka za kipatriaki—ili kutupa mwelekeo katika maisha yetu. Ingawa tumepewa kipawa cha haki ya kujiamulia ili kufanya maamuzi kwa hiari yetu wenyewe.

Lakini kuwa tuu na ramani hakutoshi. Lazima tujifunze, kuelewa, na kutumia maana iliyomo katika ramani. Hali kadhalika, unapokuja kuelewa lugha iliyotumika katika baraka yako ya kipatriaki—mwongozo wako binafsi maishani-utaweza kujua kuwa wewe ni nani katika macho ya Mungu na nini unachoweza kuwa.

Gundua Ukoo Wako

Kwanza kabisa, baraka yako ya kipatriaki inatangaza ukoo wako, au kabila mahsusi kati ya makabila kumi na mawili ya Yakobo (ambaye baadaye aliitwa Israeli) ambalo wewe unastahili kuwa. Ingawa sisi sio wote wazawa halisi wa Yakobo, maandiko yanatufundisha kwamba Waumini wa Kanisa wameasiliwa katika nyumba ya Israeli: “kwani kadiri wengi watakavyo ipokea Injili hii wataitwa kwa jina lako, nao watahesabiwa kuwa uzao wako, na watainuka na kukubariki, kama baba yao” (Ibrahimu 2:10).

Shelisa Schroeppel wa Utah, Marekani, anasema, “Kujua kwamba mimi ni wa kutoka nyumba ya Yakobo kunanisaidia kujua makusudi yangu katika maisha haya na kwa nini ninaitwa kwenye wito fulani katika Kanisa.”

Baraka yako ya kipatriaki inaweza pia kueleza baraka zo zote zenye uhusiano ambazo zinafuatana mahsusi na kabila lako. Kwa mfano, waumini wengi wa Kanisa wanahusika na kabila la Efraimu, kabila ambalo lina majukumu ya kipekee kusambaza ujumbe wa injili ya urejesho ulimwenguni (ona Kumbu kumbu ya Torati 33:13–17; M&M 133:26–34).

Tafuta Ushauri Binafsi

Ikitumika vizuri, ramani inamfanya msafiri asipotee. Vile vile, kwenye safari hii ya kidunia, baraka yako ya kipatriaki inaweza kutoa ushauri na mwelekeo kwa maisha yako. Baraka zako za kipatriaki hazikuelezi tu nini cha kufanya, lakini inaweza kutoa utambuzi binafsi kuhusu njia zipi—kama zikifuatwa katika imani—zinaweza kukusaidia wakati unapoyaoanisha maisha yako na mapenzi ya Baba wa Mbinguni. Unapojifunza baraka yako ya kipatriaki na kutaka kuishi kwa namna ambayo inamwalika Roho wa Mungu, unaweza kupata usalama, furaha, na mwongozo.

Gabriel Paredes wa Lima, Peru, anasema, “Baadhi ya ushauri ambao nilipewa katika baraka yangu nimeweza tu kuutuima kikamilifu na familia yangu baada ya kuunganishwa na mke wangu.

“Hivi karibuni tumekuwa tukishangaa nini tungeweza kufanya ili kuimarisha na kujenga familia yetu mpya. Swali letu lilijibiwa kupitia baraka yangu ya kipatriaki. Ndani yake nimeshauriwa kuweka kipaumbele heshima, uvumilivu, na upendo katika familia yangu, kwa sababu hizi ni baadhi ya misingi muhimu ya injili ya Yesu Kristo.

“Kama tulivyo fokasi juu ya hili, mke wangu na mimi tumeweza kuyashinda matatizo. Bado tuna changamoto mara moja moja kama familia, lakini tuna furaha. Nilihisi kama Bwana alikuwa ana nikumbusha jinsi ambavyo ningeweza kuwa na familia ambayo aliniahidi. Najua kwamba Bwana anasema kupitia baraka za kipatriaki na kwamba ushauri ulio ndani yake utumike katika maisha yetu.”

Sikiliza Maonyo

Ramani haitalazimika kuweka alama kila hatari zilizomo katika njia, bali kwa bahati mzuri, baraka za kipatriaki mara kwa mara zinatoa sauti za onyo ili kutulinda tukiwa njiani. Baadhi ya haya maonyo madogo husaidia kutulinda kutokana na ushawishi wa shetani; mengine yanaweza kutuelimisha juu ya jinsi tunavyoweza kushinda utu wa asili ndani yetu.

Kwa Caitlin Carr wa Utah, baadhi ya maonyo madogo katika baraka yake ya kipatriaki haikuwa wazi mara moja, lakini mafunzo yake ya baadaye ya baraka yake yalitoa utambuzi mpya.

“Wakati nilipopokea baraka yangu ya kipatriaki, nilionywa kuhusu watu watakao nijaribu na kuniyumbisha kutoka kwenye ukweli kwa mazungumzo ya kupendeza. Sikufikiria sana kuhusu hilo; nilikuwa na imani thabiti katika mafundisho niliyofundishwa.

“Hata hivyo, mwaka uliofuata nilikabiliwa na mawazo na falsafa ambazo, kwa juu juu zilionekana kujikita katika haki na upendo lakini haikuwa hivyo. Ujumbe huo ulionekana kuja kutokea kila mahali: vyombo vya habari, shuleni, hata marafiki wa karibu. Hata hivyo, nilijua falsafa hizi zilikuwa kinyume na mpango wa Mungu, nilijikuta mwenyewe nikitaka kuunga mkono vyote hivi ambavyo ni mawazo mapya ya kilimwengu na Kanisa. Mara moja nilitambua kwamba ‘hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili’ (Mathayo 6:24) na kwamba nisitegemee hekima ya binadamu. Baba wa Mbinguni alimaliza wasi wasi wangu kupitia maandiko na akazungumza amani akilini na moyoni mwangu. Na matokeo yake, ushuhuda wangu umeimarika na nimekuwa imara zaidi katika kulinda kile ambacho najua kuwa ni cha kweli.”

Kukuza Karama na vipajI

Baraka zako za kipatriaki zinaweza pia kutaja karama za kiroho na vipaji ambavyo Bwana amekupa ili kuujenga ufalme Wake. Kama baraka zako zinataja kipaji ambacho sio cha kawaida kwako, hii inaweza kuwa kwa sababu hujawa bado na nafasi ya kugundua au kukuza kipaji hiki. Kupitia kutafuta kwa bidii na msaada wa Bwana, unaweza kukua ukijumuisha kipaji hiki na vingine zaidi.

Kukuza vipaji vyako kunakusaidia kugundua vitu vya kipekee unavyo changia kwenye kazi ya Bwana. Johanna Blackwell wa California, Marekani, anatafakari karama na vipaji katika baraka zake anapohisi kujaribiwa kujifananisha na wengine: “ninapo yaangalia maneno yote katika baraka yangu ya kipatriaki, nina kumbushwa kwamba nimebarikiwa na karama nilizozihitaji binafsi kushinda majaribu na kushiriki katika uharakishaji wa kazi ya Bwana.

“Baraka zangu zinanieleza juu ya uwezo wangu, wa kupenda, kusamehe, na kuwa na ujasiri wa kuchanganyika na wale wanao nizunguka. Pale nilipozitumia karama hizi, Bwana amenibariki kwa wingi wa hamu ya kukutana na kujumuika na watu wapya na tamaduni mpya. Kwa hiyo, ushuhuda wangu umekua kwamba sisi wote ni watoto wa Baba wa Mbinguni anaye tupenda, na nimeweza kuwaokoa wengine wakati kila mmoja wetu anapotafuta kuwa zaidi kama Kristo.”

Picha
points on the map

Tafuta Baraka Zilizoahidiwa

Mwishowe, baraka zetu za kipatriaki zinaonesha ahadi zilizoahidiwa za Baba wa Mbinguni kwetu kama tutabaki kuwa waaminifu Kwake. Hakuna uhakikisho wa lini ahadi hizi zitatimizwa, lakini tunaweza kujua kwamba ili mradi tunaishi injili kwa utiifu, zitatimizwa, ama katika maisha haya au yajayo.

Sergio Gutierrez wa Nevada, Marekani, anategemea ahadi katika baraka yake ya kipatriaki wakati wo wote anapohisi wasiwasi kuhusu mipango yake ya kazi ya baadaye: “Wakati mwingine nahisi mashaka kuhusu maisha yangu ya baadae, lakini kuna ahadi katika baraka yangu ya kipatriaki ambayo siku zote inatuliza akili zangu. Ahadi hii inanisaidia kujua kwamba ili mradi nafanya kazi kwa bidii na kubaki kuwa mwaminifu, nitakuwa na rasilimali muhimu za kuweza kutunza familia yangu na kulijenga Kanisa. Sijui bado kwa uhakika ni aina gani ya kazi ninataka kuifuata, lakini kuwa na ahadi hii inanipa imani na matumaini.”

Kama umewahi wakati wowote kustaajabu nini mapenzi ya Baba wa Mbinguni yalivyo kwa ajili yako haupo peke yako. Bwana alielewa kwamba utakabiliwa na njia nyingi tofauti ambazo ungeweza kufuata katika maisha yako, kwa hiyo Yeye amekupa ramani binafsi ili uyaweke maisha yako yaoane na injili Yake. Baraka za kipatriaki haziwezi kufanya maamuzi kwa ajili yetu, lakini zinaweza kutuongoza kwenye ufunuo wetu binafsi. Kupitia baraka zetu za kipatriaki,tunaoneshwa jinsi tunavyoingia katika mpango wa Bwana wa kuwakusanya wana wa Israeli kwa kujifunza juu ya kabila letu; tunapewa ushauri binafsi, maonyo madogo madogo, na ahadi; na tumefundishwa kuhusu karama za kipekee na vipaji ambavyo Baba wa Mbinguni ametupa ili kumtumikia Yeye. Ili mradi unajaribu kuishi kufuatana na misingi hii ya baraka zako za kipatriaki, unaweza kujua kwamba maamuzi yako yamekuwa ndani ya mapenzi ya Bwana kwa ajili ya maisha yako.