2017
Nguvu za Mungu.
April 2017


Mpaka Tutakapokutana Tena

Nguvu za Mungu

Kutoka katika hotuba ya kikao kikuu cha ukuhani yenye kichwa cha habari “Mafundisho ya Ukuhani,” Ensign, Mei 1982, 32–34; capitalization standardized.

Imani ni nguvu na nguvu ni ukuhani.

Picha
Enoch and the city of Zion

Mji wa Sayuni Ulitwaliwa, na Del Parson

Mungu ni Mungu kwa sababu Yeye ni mfano wa imani yote na nguvu zote na ukuhani wote. Maisha aishiyo Yeye yanaitwa uzima wa milele.

Na kwa kiasi ambacho sisi tunakuwa kama Yeye ndiyo kiasi ambacho tunapata imani yake, tunapata nguvu Zake, na kuufanyia kazi ukuhani Wake. Na wakati inapokuwa tumekuwa kama Yeye katika ukamilifu na maana ya kweli, hapo nasi pia tutapata uzima wa milele.

Imani na ukuhani vinakwenda pamoja. Imani ni nguvu na nguvu ni ukuhani. Baada ya kuwa na imani, tunapokea ukuhani. Kisha, kupitia ukuhani, tunakua katika imani hadi, kupata nguvu zote, nasi tunakuwa kama Bwana wetu.

Muda wetu hapa katika mwili wenye kufa umetengwa rasmi kama muda wa maandalizi na kujaribiwa. Ni nafasi yetu tukiwa hapa kuikamilisha imani yetu na kukua katika nguvu za ukuhani. …

Ukuhani mtakatifu ulifanya zaidi katika kuwakamilisha wanadamu katika siku za Henoko kuliko wakati mwingine wo wote. Ulijulikana kwa wakati huo kama mfano wa Henoko (ona M&M 76:57), ilikuwa ni nguvu ambayo kwayo yeye na watu wake walihamishwa. Na walichukuliwa hai kwa sababu walikuwa na imani na walitumia nguvu za ukuhani.

Alikuwa Henoko ambaye Bwana aliweka naye agano la milele kwamba wale wote waliopokea ukuhani watakuwa na nguvu, kupitia imani, kuongoza na kusimamia vitu vyote duniani, kuweka ujasili kwa majeshi ya mataifa, na kusimama katika utukufu na kuinuliwa mbele za Bwana.

Melkizedeki alikuwa mtu wa imani ya jinsi hiyo, “na watu wake walitenda haki, na waliipata mbingu, na waliutafuta mji wa Henokoi” (Joseph Smith Tafsiri ya, Mwanzo 14:34). …

Ni nini, basi, mafundisho ya ukuhani? Na jinsi gani tunaweza kuishi kama watumishi wa Bwana?

Mafundisho haya ni kwamba Mungu Baba yetu ametukuka, mkamilifu, na kiumbe aliye inuliwa ambaye ana ukuu wote, nguvu zote, na mamlaka yote, ambaye anajua mambo yote na sifa zake zote hazina mwisho, na ambaye anaishi katika muundo wa familia.

Ni kwamba Baba yetu wa Milele anafurahia hali hii ya juu ya utukufu na ukamilifu na nguvu kwa sababu imani Yake ni kamilifu na ukuhani Wake hauna ukomo.

Ni kwamba ukuhani ni jina halisi la nguvu ya Mungu, na kwamba kama tunahitaji kuwa kama Yeye, lazima tupokee na kuutendea kazi ukuhani Wake au nguvu kama Yeye Anavyozitumia. …

Ni kwamba tuna nguvu, kwa imani, kutawala na kudhibiti mambo yote, vyote kimwili na kiroho; kutenda miujiza na kukamilisha maisha; kusimama mbele ya Mungu na kuwa kama Yeye kwa sababu sisi tumepata imani Yake, ukamilifu Wake, na nguvu Zake, au kwa maneno mengine ukamilifu wa ukuhani Wake.

Haya, basi, ndiyo mafundisho ya ukuhani, kuliko basi hakuna kitu wala hapawezi kuwa na kitu cho chote kilicho zaidi ya huu. Hii ndio nguvu tunayoweza kuipata kupitia imani na haki …

Hakika kuna nguvu katika ukuhani—nguvu ambayo tunaitafuta kuipata ili kuitumia, nguvu ambayo tunaomba kwa bidii juu yetu na juu ya vizazi vyetu milele.