2017
Yesu Alitupatia Sakramenti
April 2017


Hadithi za Yesu

Yesu Alitupatia Sakramenti

Picha
Jesus Gave Us the Sacrament 1
Picha
Jesus Gave Us the Sacrament 2
Picha
Jesus Gave Us the Sacrament 3

Yesu alijua muda Wake duniani ulikuwa karibu umekwisha. Aliwakusanya Mitume Wake pamoja kwa ajili ya Karamu ya Mwisho. Aliwapatia sakramenti na kuwaambia daima wamkumbuke Yeye.

Yesu alikwenda kwenye bustani kuomba. Aliumia kwa dhambi zote na mambo ya kuhuzunisha katika maisha ya kila mtu. Kisha alikufa msalabani na alizikwa katika kaburi la kuchongwa.

Asubuhi ya Jumapili baada ya Yesu kufa, baadhi ya wanawake walikuja kaburini. Jiwe mlangoni lilikuwa limebingirishwa mbali, na kaburi lilikuwa tupu! Yesu alikuwa wapi?

Alikuwa hai tena! Mariamu Magdalena alimwona Yesu. Aliwatembelea Mitume wake ili wawe tayari kufundisha injili baada ya Yeye kurudi mbinguni.

Ninapochukuwa sakramenti, mimi humkumbuka Yesu. Ninakumbuka kwamba Yeye aliishi na alikufa na akafufuka kwa ajili yangu ili niweze kuishi tena!