2017
Ninawezaje kuisaidia familia yangu kuwa imara?
April 2017


Majibu kutoka kwa Mtume

Ninawezaje kuisaidia familia yangu kuwa imara?

Kutoka “More Diligent and Concerned at Home, Liahona, Nov. 2009, 17–20.

Picha
How can I help my family be strong

Waambie familia yako kuwa unawapenda na onyesha kwa vitendo.

Toa ushuhuda wako juu ya mambo unayojua kuwa ni ya kweli kwa njia ya Roho Mtakatifu. Shirikiana ushuhuda wako na wale unao wapenda zaidi.

Kwa hiari yako ungana na wana familia yako katika maombi ya familia na katika kujifunza maandiko. Jishughulishe katika jioni ya familia nyumbani na ifanye kuwa ya kupendeza.

Kuwa mwaminifu katika kujifunza, kuishi, na kuipenda injili ya urejesho ya Yesu Kristo.