2013
kuongoka kwa Bwana
Februari 2013


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi Februari 2013

Kuongoka kwa Bwana

Soma kifaa hiki kwa maombi na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe. Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.

Picha
Alama ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama

Imani, Familia, Usaidizi

Akina dada wapya wa Kanisa— pamoja na Wasichana wanaojiunga na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, akina dada wanaorudi katika ushiriki, na waongofu wapya—wanahitaji msaada na urafiki wa walimu watembelezi. “Kuhusika kwa washiriki ni muhimu katika kuongoa, kuhifadhi na kuleta washiriki wasioshiriki kikamilifu kurudi katika ushirika mkamilifu,” Alisema Mzee M. Russell Ballard wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili. “Shika ono kuwa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama unaweza kuwa [moja ya] nyenzo za nguvu za kushirikiana ambazo tunazo katika Kanisa. Wafikie mapema wanaofundishwa na wanaorudishwa katika ushiriki, wapende katika Kanisa kupitia shirika lenu.”1

Kama washiriki wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, tunaweza kuwasaidia washiriki kujifunza desturi za kimsingi za Kanisa, kama vile:

  • Kutoa hotuba

  • Kutoa ushuhuda

  • Kuishi sheria ya mfungo

  • Kulipa fungu la kumi na sadaka zingine

  • Kushiriki katika kazi ya historia ya familia

  • Kufanya ubatizo na udhibitisho kwa mababu zao waliofariki.

“Inahitaji marafiki makini kuwafanya washiriki wapya wahisi huru na kukaribishwa Kanisani,” alisema Mzee Ballard.2 Sisi wote, lakini hasa walimu watembelezi, tuna majukumu muhimu kujenga urafiki na washiriki wapya kama njia ya kuwasaidia wawe imara “kumgeukia Bwana” (Alma 23:6).

Kutoka kwa Maandiko

2 Nephi 31:19–20; Moroni 6:4

Kutoka kwa Historia Yetu

“Na idadi inayozidi kuongezeka ya waongofu,” alisema Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008), “lazima tutie bidii zaidi kuwasaidia katika kupata njia yao. Kila mmoja wao anahitaji vitu vitatu: rafiki, jukumu, na kulishwa na ‘neno nzuri la Mungu’ (Moroni 6:4).”3

Walimu Watembelezi wamo katika nafasi ya kusaidia wale wanaowalinda. Urafiki kwa mara nyingi huja kwanza, kama ilivyokuwa kwa dada mchanga wa Muungano wa Usaidizi wa kina mama ambaye alikuwa mwalimu mtembelezi wa dada mzee. Walikuwa na ugumu kujenga urafiki hadi walipofanya kazi bega kwa bega kwenye mradi wa kusafisha. Wakawa marafiki, na walipozungumza kuhusu Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, walilishwa wote wawili na “neno nzuri la Mungu.”

Rais Joseph Fielding Smith (1876–1972) alisema Muungano wa Usaidizi wa kina mama “ni sehemu muhimu ya Ufalme wa Mungu duniani na unasaidia washiriki wake waaminifu kupata uzima wa milele katika ufalme wa Baba yetu”4

Muhtasari

  1. M. Russell Ballard, “Members Are the Key,” Liahona, Sept. 2000, 18.

  2. M. Russell Ballard, Liahona, Sept. 2000, 17.

  3. Gordon B. Hinckley, “Every Convert Is Precious,” Liahona, Feb. 1999, 9.

  4. Joseph Fielding Smith, katika Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 97.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Naweza kumuombea mwenzangu na kuuliza kwamba Roho atuongoze tunapowatumikia akina dada zetu?

  2. Tunawahudumia kwa njia gani kila dada tunayelinda ili ajue kwa kweli tunamjali?