2012
Walezi wa Nyumba
Februari 2012


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi Februari 2012

Walezi wa Nyumba

Soma kifaa hiki, na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Imani, Familia, Usaidizi

“Ninyi ni walezi wa nyumba,” alisema Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008) alipokuwa akitambulisha “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” katika mkutano mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama katika mwaka wa 1995. “Ninyi wazazi wa watoto. Ninyi ndio mnaowatunza wao na kuanzisha miongoni mwao tabia za maisha yao. Hamna kazi yotote inayofikia karibu hivyo na uungu kama vile kutunza wana na mabinti wa Mungu”1

Kwa karibu miaka 17 sasa haya matangazo yamethibitisha kwamba majukumu yetu muhimu sana yanalenga kuimarisha familia na nyumba—bila kujali hali zetu za sasa. Barbara Thompson, mshauri wa pili katika urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alikuwa katika Tabenakulo la Salt Lake wakati Rais Hinckley aliposoma mara ya kwanza tangazo hili. “Ilikuwa ni wakati mkuu sana,” yeye anakumbuka. “Mimi nilihisi umuhimu wa ujumbe huu. Pia nilijipata nikiwaza mwenyewe, ‘Huu ni mwongozo mkuu kwa wazazi. Pia ni jukumu kubwa kwa wazazi.’ Niliwaza kwa muda mchache kwamba kihalisi haikunihusu sana mimi kwa kuwa mimi sikuwa nimeolewa na sikuwa na watoto wowote. Lakini ghafula nilivyokuwa nikifikiria, ‘Lakini inanihusu mimi. Mimi ni mwanafamilia. Mimi ni binti, dada, shangazi, binamu, mpwa, na mjukuu wa kike. Mimi nina majukumu—na baraka—kwa sababu mimi ni mwanafamilia. Hata kama ningekuwa mwanafamilia pekee aliye hai, mimi bado ni mwanafamilia wa familia ya Mungu, na nina jukumu la kusaidia kuimarisha familia zingine.’”

Bahati nzuri, hatujawachwa peke yetu katika wajibu wetu. “Usaidizi mkubwa,” anasema Dada Thompson, “tunaoweza kupata katika kuimarisha familia ni kujua na kufuata mafundisho ya Kristo na kumtegemea Yeye ili kutusaidia sisi.”2

Kutoka kwa Maandiko

Mithali 22:6;1 Nefi 1:1;2 Nefi 25:26;Alma 56:46–48;Mafundisho na Maagano 93:40

Kutoka kwa Historia Yetu

“Wakati Dada Bathsheba W. Smith alihudumu kama rais mkuu wa nne wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama [kutoka 1901 hadi 1910], yeye aliona haja ya kuimarisha familia, na kwa hivyo alianzisha masomo ya elimu kwa kina mama kwa kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama. Masomo haya yanajumuisha ushauri juu ya ndoa, utunzaji wa kabla kuzaa, na ulezi wa mtoto. Haya masomo yalihimili mafunzo ya Rais Joseph F. Smith kuhusu Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwasaidia wanawake katika wajibu wao nyumbani:

“‘Panapokuwa na ujinga au hata upungufu wa uelewa kuhusu familia, wajibu wa familia, katika kuhusu masharti ambayo yanafaa kuwa na yale yaliyopo kihaki kati ya mume na mke na kati ya wazazi na watoto, kuna hiki kikundi kilichopo au kipo karibu, na kwa majaliwa halisi na maongozi ambayo yanahusiana na cha toread kikundi cha waliojitayarisha na wapo tayari kutoa mafunzo kwa marejeleo ya huu wajibu muhimu.’”3

Muhtasari

  1. Gordon B. Hinckley, “Stand Strong against the Wiles of the World,” Ensign, Nov. 1995, 101..

  2. Barbara Thompson, “I Will Strengthen Thee; I Will Help Thee,”LiahonanaEnsign, Nov. 2007,117.

  3. Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society(2011), 153.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Je! Ninaweza kuwasaidia kina dada kutunza ili kuimarisha familia vipi?

  2. Je! Ninaweza kuwa ushawishi mwema katika familia yangu vipi?