2012
Maombi Yangu ya Imani
Februari 2012


Vijana

Maombi Yangu ya Imani

Nilipokuwa umri wa miaka 18, nilifanya kazi katika duka za samani kama muuzaji. Ratiba yangu ilikuwa ngumu sana. Nilifanya kazi kutoka saa 2:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku, Jumatatu hadi Jumamosi. Nilihuzunika kwa sababu singeweza kushiriki katika shughuli za chuo na Kanisa.

Nilianza kumwomba Baba wa Mbinguni kwa imani nyingi sana ili kumuuliza Yeye anisaidie kupata kazi ambapo sitafanya kazi siku za Jumamosi ili niweze kuenda kwenye shughuli za chuo na zingine.

Siku moja kazini nilikuwa nikimsaidia mtu mmoja. Tulianza kuongea, na aliniambia alikuwa anafanya kazi katika benki kubwa. Nilimuuliza jinsi ningeweza kupata kazi katika benki hii. Alinipatia jina lake na nambari ya simu na akaniambia kama ningempigia simu msajili na kusema nilikuwa namjua. Nilienda kwenye benki hii na nikafanya mitihani iliohitajika. Nilipita na kuanza kufanya kazi masaa sita kila siku Jumatatu hadi Ijumaa, nikipata mshaara mara tatu ya ule nilipata hapo awali.

Najua Bwana hutuongoza sisi tunapokuwa na hamu ya kumweka Yeye mbele. Yeye ananiongoza mimi hata leo. Mimi najua kanuni ya maombi ni ya kweli.